Mkurugenzi wa Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uamizi wake wa kujitoa na kutoshiriki tena mashindano ya urembo ya Miss International na kuiomba serikali za Tanzania, Japan na China kutotoa ushirikiano wowote kwa shirika la International Cultural Association (ICA) ambao ni waandaji wa mashindano hayo nchini Japani kutokana na ubaguzi wa rangi ambao wameundeleza kwa miaka 51 tokea shindano hili lilipoanza.Kulia ni Mshiriki wa Shindano hilo Nelly Kamwelu wakati walipokuwa wakiwasili nchini kutokea China yalikofanyika mashindano hayo.
Compass Communications yenye leseni ya mashindano ya urembo ya Miss International tokea mwaka 2005 imetangaza kujitoa rasmi katika shindano hilo na kuiomba serikali za Tanzania, Japan na China kutotoa ushirikiano wowote kwa shirika la International Cultural Association (ICA) ambao ni waandaji wa mashindano haya nchini Japani kutokana na ubaguzi wa rangi ambao wameendeleza kwa miaka 51 tokea shindano hili lilipoanza.
Msimamo huu umetolewa na mkurugenzi wa Compass, Maria Sarungi Tsehai ambaye amerudi kutoka mashindano haya na mrembo Nelly Kamwelu ambaye alishindana na warembo wengine 65. Fainali ya mashindano haya yaliyofanyika mji wa Chengdu China tarehe 6 Novemba na katika fainali hiyo hakukuwa na mwakilishi kutoka Afrika katika 15 bora.
“Tanzania tuliwaandikia waandaji (ICA) mwaka 2009 kuwa tunajitoa katika mashindano haya kutokana na ukweli ya kuwa kwa miaka 50 hawajawahi kumpa taji mwafrika na hata 15 bora hawajawahi kuweka mwafrika.” Alieleza mkurugenzi huyu. “ICA walitujibu kuwa watafanya mabadiliko kuanzia mwaka 2010 na kutoa ushindi wa kila bara ambao wataweza kuingia katika fainali yaani hatua ya 15 bora”.
Mwaka 2010 Tanzania haikushiriki katika Miss International kutokana na kile alichoeleza Sarungi kuwa ni hatua ya kutaka kuangalia maendeleo. Hata hivyo mwaka 2010 bado hakukuwa na mabadaliko na hivyo nchi ya Kenya na nchi zingine za kiafrika zilijitoa mwaka huu. Mwaka huu kulikuwa na washiriki 3 wa Afrika ingawa katika mtandao wao awali walionyesha wasichana 6 wa kiafrika, alieleza Sarungi.
“Hata hivyo tulielezwa ya kuwa katika shindano la mwaka huu tutaona maboresho. Na hivyo tulijiamini na kumtuma mshindi wetu wa mwaka huu katika mashindano haya”
Kwa upande wake mwakilishi wa Tanzania, Nelly Kamwelu ambaye pia aliwakilisha Tanzania katika shindano la Miss Universe alieleza ya kuwa anaamini kuwa alishiriki vizuri na alikuwa moja wa washiriki waliopigwa sana picha na kuoneshwa katika televisheni, pia alikuwa mstari wa mbele katika shindano dogo la vipaji.
Miss Universe Tanzania,Nelly Kamwelu |
“Zaidi ya siku yenyewe ya shindano, niliombwa mara 5 zaidi kucheza katika tafrija mbalimbali na nilikuwa mshiriki wa pekee ambaye alichezeshwa mara nyingi” alieleza mrembo huyu ambaye alionyesha kipaji cha kucheza miondoko ya kiarabu yaani bellydancing “Baada ya hayo yote, nilipatwa na mshangao mkubwa kuona tuzo ya vipaji anapewa Miss China. Lakini kilichonishangaza zaidi ni kuwa katika 15 bora wameingizwa wasichana ambao hawakushiriki kikamilifu katika shindano dogo wala kuonyesha ucheshi wowote na hawakuwa na vigezo vya urembo ninavyovijua’
Nelly Kamwelu anashikilia mataji ya Miss Universe Tanzania, Miss Southern Africa International na pia alishiriki katika mashindano makubwa kupita yote duniani – Miss Universe.
Mkurugenzi wa Compass alisisitiza kuwa sababu nyingine kuu ya malalamiko yao kwa waandaji ilikuwa kukosekana kwa vigezo vya kueleweka vya kutafuta washindi na kuonekana kuwa waandaji walikuwa wanabadilisha masharti siku ya mwisho. “Warembo hawakufanyiwa usahili na majaji hivyo haieleweki hawa 15 bora waliwatafutaje!”
Maria Sarungi amesihi serikali ya Japan kusitisha msaada wowote kwa ICA kwani hawazingati kanuni na misingi ya ushirikiano wa kiutamaduni (cultural exchange) kutokana na kuwabagua waafrika. Pia ameiomba serikali ya China ambayo imedhamini mashindano haya kupitia serikali ya jiji la Chengdu kutodhamini tena mashindano haya. “Kuendelea kudhamini na kutoa ruzuku kwa shirika la ICA inaweza kueleweka kwetu sisi waafrika ya kuwa serikali hizi hazijali ubaguzi wa rangi unaoendelezwa na ICA kwa miaka 51 sasa”
Maria peleka watu wenye viwango sio huyo Nelly kamwelu!Watu wanaopelekwa hawana viwango vyovyote.Siku zote unatumia "watu ambao wameshindwa mashindano ya ndani ndo wanapelekwa. Acha hizo mama...
ReplyDeleteMtajiju!
ReplyDeleteAsiekubali kushindwa si mshindani. Kila siku tunatafuta visingizo kwanini hatuwezi kushinda.
ReplyDeletePoleni sana ndio dunia na watu walivo.Lakini mkumbuke hizo sio mila zenu ni bora kukuza utamaduni wenu kuliko kuingia ktk mambo yasiyoingiliana na tamaduni zenu.Waacheni wenyewe na watachaguana wenyewe huku ni ngoma tu banaaaa.Jaribuni kubuni mambo ya maana kuliko kwenda kuonyesha mwili wako na vichupi tu hamjui kama mnajidhalilisha.
ReplyDeleteHehehhheee nicheke mieee. Hayo ni mambo ya 'teknolojiko no hu'. Maria unapekeka watu wako na huko uendako wana watu wao. simpo ikweshen. Utashinda??
ReplyDeleteNakuuga mkono kwa msimamo wako wa kishujaa kutetea africa
ReplyDeleteMaria unafanya kazi nzuri, bahati mbaya ubaguzi bado unaendelea mpaka sasa si kwa wamatumbi tu bali hata ubaguzi wa wazawa weusi waliopo nchi zenye wazungu. ushauri wangu kwenu ni kuanzisha kitu kama MISS AFRICA, nchi za kiafrika zinahitaji kubuni mbinu za kujithamini sisi wenyewe, hatuhitaji wazungu ama watu wa asia watuthamini sisi.
ReplyDeletehivi sasa mwafrika akija kushinda hiyo ICA si mtasema mlilazimishia!?
ReplyDeletemimi nadhani ICA waweke process zao more open na sisi tujinoe vilivyo, ila tukianza kulia kwamba ni wabaguzi na hatuko powa itakuwa sio vizuri.
= = =
buffalo,
new york
kwanza hawajaambia, mnadanganya mnapeleka waafika kumbe sio waafrika maana waafrika ni weusi nyie mnapeleka walioweka mkorogo na nywele za bandia. ndio maana mnakosa hawajawaambia tu.
ReplyDeletehuyu mbona anaonekana gambachori.
itachukua mda hawa wazungu kuacha ubaguz wanaweza cheka nawe ukajiona usalama kumbe unaangamia.. kwel jaribun kubun kitu cha kiafrica zaid..
ReplyDeletewewe nshimimana aka dumisane naoina hauko USA. Mimi nipo hapa. Watu kutoka Asia ni wabaguzi sana, afadhali hata mzungu.
ReplyDeleteVITA MAMA LAZIMA UWE VITANI. UKIKIMBIA UMESHINDWA VITA. HUIWEZI HIYO.
ReplyDeleteKAULI YAKO NA USHAWISHI WAKO UNAWEZA KUKUPONZA NA UKAFUNGIWA MAISHA KWENYE MASHINDANO YOTE YA UREMBO KWA KILE KINACHOITWA CALUMNY (VILIFICATION) DHIDI YA ICA.
UNAPOMWITA MTU RACIST LAZIMA UWE NA USHAHIDI KAMILI KUDHIBITISHA MADAI YAKO SIYO KULIPUKA TU NA KUDAI ETI HAKUNA MWAFRIKA HATA MMOJA KWENYE TOP 15! THAT'S NOT RACIST...MAY BE VIWANGO VYENU HAFIKII KINACHOTAKWA NA MAJAJI.
CONTACT YOUR BRAIN, EYES AND MOUTH BEFORE COMING OFF YOU CAGE AND ERUPT WITH YOUR ACCUSATION. THE WORD RACIST MAY TURN SOUR! CIAO
Ukweli mi nilikuwa namuombea huyo dada maana mama yake amejifunika tena real African na yeye ameeanda kuvaa vichu.. hata haibu hana tena anatupigia picha mnawawekea watoto wetu. Si mila zetu Tz, tena mshindwe na kulegea igeni maendeleo ya wazungu si uchafu huo au homosexual.
ReplyDeleteHamjui Mungu anachukia uovo? Ushauri wangu rudini kwenye majumba ya sala mkapate maelekezo upya. Michu usinibanie eee baba
siasa hadi kwenye urembo? eti mnahoji kwanini hakukuwa na mwafrika kwenye top 15. ebu tafuteni visingizio vingine.
ReplyDeleteJamani mulikwisha sikia mtu yeyote mweusi anaitwa mtakatifu? Mtakatifu Michuzi, Mtakatifu Zonga, hakuna. Watakatifu wooote wako ulaya. Lakini hata mweusi akikaa ulaya miaka alfu moja hawezi kuitwa mtakatifu ng'o. Ushauri wangu ni kama wa wadau walionitangulia:
ReplyDelete1. Utamaduni huo sio wetu, acheni mambo ya kuigaiga. Anzisheni miladi bora.
2. Kama kuna king'ang'anizi basi fanyeni ya ki-africa. Lakini msirushiane makonde, jifunzeni kutofautiana bila kugombana.
Pole sana dada yangu Nelly, naona umesononeka sana. Ninapenda kukuhakikishia kuwa wewe bado ni mzuri tu, machoni pa Mwenyezi Mungu. Na zaidi katika macho yetu watanzania na weusi popote tulipo. Hata hao waliokuangusha, kama walikuangusha wanajuwa uzuri wako. Kwa hiyo basi usiinamishe kichwa wala macho yako, kiinue na ufungue macho yako ili tuendelee kuuona uzuri wako na tumtukuze aliyekujalia (Muumba)
ReplyDeleteMizuka tunaijua, yenyewe inaamini kuwa iko bora katika mambo yote: demokrasia wao, akili wao, dini wao, mali wao, uungwana wao, upendo wao, mapenzi wao, majina mazuri wao, utamaduni safi wao, meno meupe wao, NA UREMBO WAO.
Jifunzeni. Hivyo ndivyo walivyo huko kwao. Wanaweza kukupa nusu upendo kama wanakutumia. Vinginevyo sahau
hehehe, dada kakatishwa viuno mbele ya kadamnasi ndio kaona atashinda kumbe mijitu ilikuwa inakula gudtaimu u. niynyi waafrika wenzenu wamejitoa mapemaa nyie mkaona kwakuwa waafrika wachache you stood a better chance, poleni sana ila mmewasaliti wenzenu!!
ReplyDeletenyie wenyewe wabaguzi mbona alivoshinda muhindi mliwaka?
ReplyDeleteKama unamuona ana vigezo mbn hakushinda hiyo miss universe?au utasema wanabagua taifa la tanzania?Acha kulalama tatua tatizo
ReplyDeletedenanesh!? ane dennah, chigirr ielemu!
ReplyDeletesas jamani kwani hamuoni pia nchi yingine zimewahi kucomplain ndo maana na yeye amecomplain, si kwamba amekurupuka. ila mimi namuunga mkono aliyesema wajaribu kuanzisha kitu chenye asili ya Africa. Halafu tunasema eti wazungu ndo homosexual ina maana hakuna mwafrika homesexual? acheni kunyoosha watu vidole mkijidai wasafi eti kisa mmejifunika mwili mzima usafi wa moyo hauletwi na mavazi bali matendo.
ReplyDeleteKwa maneno ya Maria ni kuwa walienda kushiriki mwaka huu baada ya kuahidiwa "mabadiliko". Ni kwamba mwaka huu angechaguliwa mwakilishi wa Afrika hata kama hatakidhi vigezo ili kuwapooza waafrika? Mashindano gani hayo? Nachelea kukubaliana na hoja ya ubaguzi kwani kuna uwezekano kabisa kuwa waafrika hatujapeleka msichana aliyestahili kushinda tangu mashindano yaanze. Sijui miaka mingine, ila Nelly is not winning material - she's just not fresh anymore! Angeshinda ningeshangaa. Jamani tubadilike, tuache kutegemea favours kuwa eti sisi weusi, hatuna uwezo, wanawake etc etc.
ReplyDeletehi tanzania poleni sana. pole sana nelly i know how you feel.. wasia ni wabaguzi sana mimi naishi australia yani huwezi amini wote tu wageni hapa ila utashangaa mgeni anambagua mgeni mwenzake.
ReplyDeletewaasia ni wabaguzi sana yani wazungu ni bora sana kuliko hata hao wasia ambao wengine nchi zao ni masikini kuliko za africa.
poe sana maria.
Watakatifu waafrika wako yupo mtakatifu Bhakita na Nyerere yuko njiani. Mi nashangaa tunashangaa nini wakati ubaguzi upo hapahapa Tanzania. hulka za binadamu ni ya ajabu sana yote haya ni watu wengine kuona rangi yao ni bora kuliko ya wengine, color is skin deep. Kama nchi tuanze cc tuache kubaguana kwa rangi, dini na hata makabila hakuna anayetambika hapa!!!
ReplyDelete