Wachezaji wa Timu ya Hazina wakiwa kwenye maandamano ya kupita mbele ya mgeni rasmi wakati wa sherehe za ufungaji wa mashindano ya SHIMIWI yaliyofanyika mkoani Tanga jana.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa (aliesimama) akitoa hotuba ya ufungaji wa mashindano ya SHIMIWI kwa mwaka 2011 yalimalizika jana jijini Tanga.
Timu ya Mpira wa Miguu ya Hazina wakishangalia ushindi wao jana jijini Tanga mara baada ya eapinzani wao Timu ya Uchukuzi kugomea kugipa penati mara baada ya dakika 90 kumalizika wakiwa wamefungana bao 1-1.
Nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Hazina ,Respecious Mugisha akipokea Kombe la Ushindi wa Kwanza wa mashindano ya SHIMIWI kwa 20011 kutoka kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa (kushoto) mara baada ya kuibuka mabigwa wa SHIMIWI kwa mwaka 2011 kwa mpira wa miguu kufuatia timu ya uchukuzi kugoma kupiga penati ya kuamua mshindi wa fainali baada ya mchezo kumalizika wakiwa wamefungana bao 1-1
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa (wa pili kushoto) akiwavisha medali wachezaji wa timu ya mpira ya Hazina jana jijini Tanga mara baada ya kuibuka mabigwa wa SHIMIWI kwa mwaka 2011 kufuatia timu ya uchukuzi kugoma kupiga penati ya kuamua msindi wa fainali baada ya mchezo kumalizika wakiwa wamefungana bao 1-1.
Wachezaji wa timu ya mpira wa Miguu ya Hazina wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wao mara baada ya kuibuka mabigwa wa SHIMIWI kwa mwaka 2011 kwa mpira wa miguu kufuatia timu ya uchukuzi kugoma kupiga penati ya kuamua mshindi wa fainali baada ya mchezo kumalizika wakiwa wamefungana bao 1-1
Sasa kama dk 90 zimeisha sheria inasema ziongezwe dk 30 kwanini hawajaongeza huo ndio ubabaishaji wa viongozi wetu wa soka
ReplyDelete