Nahodha wa Timu ya Pool ya Taifa,Charles Venance (wa tatu kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada kwa Mtoto mwenye ulemavu wa akili,Mlashani Rwuza wa kituo cha Miyuji,Mjini Dodoma wakati Timu hiyo ilipotembelea kituo hicho.Kulia ni Kocha wa Timu hiyo ya Taifa,Dennis Lungu na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Pool Tanzania,Freddy Mushi ambaye ndie kiongozi wa Msafara wa timu hiyo.Timu ya Pool ya Taifa imeshatembelea mikoa ya Morogoro,Iringa,Mbeya na Dodoma ambapo kila mkoa iliotembelea ilicheza mchezo wa kirafiki na timu ya mkoa husika,imesinda michezo katika mikoa mitatu ambayo ni Morogoro,Iringa na Dodoma na kufungwa mchezo mmoja na timu ya mkoa wa Mbeya.Timu hiyo imeondoka mjini Dodoma leo asubuhi kuelekea Mkoani Manyara ambapo itacheza mchezo mmoja na timu ya mkoa huo.
Wachezaji wa Timu ya Pool ya Taifa wakiwa wamebeba sehemu ya msaada waliokwenda kuutoa kwenye kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa akili cha Miyuji,Mjini Dodoma.
Baadhi ya Wachezaji wa Timu ya Pool ya Taifa wakia wamevalia t-shirt zao safi kabisa za Safari Lager ambao ndio wadhamini wakuu wa Timu hiyo ya Taifa.
Kwa miaka yote tumekua tukiona hiyo inayoitwa misaada ya watoto hao wanapewa vitu vile vile.Kwa mfano utaona gunia la unga, mafuta, vijuice juice, biscut nk. Nafikiri hivyo vitu sio misaada. Ikiwa kama upo camp (chuo/shule) na washkaji wakakuletea vitu ambavyo timu ya pool wamewapelekea hao watoto nadhani hutasema ni msaada. Nafiriki ungesema ni ZAWADI. Kwani baada ya siku chache tu utahitaji tena.
ReplyDeleteNaona msaada ungekuwa kama hivi: Tusema thamani ya hivyo vi lambalamba vyoooote hao jamaa wa pool walopeleka kwa hao watoto ni kama sh 500,000. Naona kama wangepeleka angalau ka kompyuta ka1, ya thamani ya 300,000, ingekuwa msaada sana kwani hao watoto, kwani wangepata UJUZI ambao ungewasaidia katika maisha yao ya baadae. Au vitabu vyenye thamani sawa na vizawadi hivyo, naona ingeleta tofauti kidogo jamani. Ingawa kutoa ni moyo na mtu hachaguliwi kitu cha kumpa mtu, jamani hebu tubadilike kidogo na tukijipanga pia mabadiliko yatatokea ikiwa kama kweli kweli tuna nia ya kutoa MISAADA.