MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein,akikabidhiwa  mashine ya INCUBATORS, na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania,Sander Gurbuz,(katikati) katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika jana kwenye Hospitali kuu ya Mnazi mmoja,Zanzibar.kushoto ni Mke wa Balozi hiyo,Mama Durhan Gurbuz.Picha na Othman Maulid 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hivi ni maelezo ya mwandishi ndiyo yamekwenda kombo au vipi? Inaonesha mheshimiwa balozi ametoa msaada wa kitu chenye madhara kuliko faida. Yani kama hiyo incubator inamfanya mtoto awe taahira baada ya kuzaliwa, sidhani kama ina faida!

    Bin Mashi,
    Uturuki

    ReplyDelete
  2. Huenda maoni yangu hamtayaweka hewani, lakini kama Mhariri wa Kujitegemea, huwa napenda kufikisha ujumbe tu, kwa manufaa ya toleo lijalo: Tafadhalini muwe mna-hariri habari vizuri. Ukisoma hii habari, hakika utashangaa ni kwa nini mke wa rais anapokea mashine yenye madhara!!! Nanukuu kama mlivyoandika,"mashine hiyo hupunguza Bilirubini katika mwili wa mtoto, na inaathiri ubongo, hivyo mtoto anakuwa taahira baada ya kuzaliwa". Mwisho wa kunukuu. Ukisoma tena kwa umakini hiyo habari utaona kuwa mashine inaathiri ubongo na kusababisha mtoto kuzaliwa akiwa taahira. Lakini naamini mwandishi alitaka kumanisha kuwa Bilirubini ndiyo yenye madhara hayo.

    ReplyDelete
  3. hiyo mashine inaathiri ubongo au inasaidia ubongo usiathirike?

    ReplyDelete
  4. WADAU WAWILI HAPO JUU VIPI TENA?KAMA HAMUNA KNOWLEDGE SI MUONDOE UVIVU MO GOOGLE TU.
    INCUBATOR NI SUPPORTING MACHINES KWA PREMATURE INFANTS ILI VIUNGO VYA NDANI MBALIMBALI VIKAMILISHE UKUAJI WAKE,SPECIFIC LUNGS(MAPAFU).
    ANAWEZA KUKUA BILA HIYO MACHINE ILA KUPATA ULEMAVU NI ASILIMIA YA JUU.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa tatu, habari ilipotoka kwa mara ya kwanza palikuwa na maelezo kuwa incubators zinawafanya watoto wawe taahira baada ya kuzaliwa na ndiyo maana wadau wawili wa mwanzo wakatoa maoni hayo. Na si kwa kuwa hawana ufahamu wa hivyo vifaa. Bila shaka umetoa maoni yako baada ya sentensi husika kuondolewa.

    Mdau mwingine!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...