Mama wa Mitindo nchini,Asia Idarous akipita jukwaa ni na mmoja wa mamodol wake katika ufunguzi Swahili Fashion Week uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Makumbusho ya taifa jijini Dar.
Mwanamkitindo Kiki's (katikati) akipita jukwaani na mmoja wa mamodol wake katika ufunguzi Swahili Fashion Week uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Makumbusho ya taifa jijini Dar.
Baadhi ya Mamodol waliovalia mavazi mbali toka kwa wabunifu tofauti tofauti wakipita jukwaani kuonyesha mavazi hayo katika ufunguzi Swahili Fashion Week uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Makumbusho ya taifa jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Wandugu wapenzi. ingawa nimezaliwa darisalama, lakini katika hili swala la umodo kwa wanaume, mimi bado ni mkambunga tuu katika mambo haya. Hivi nguo kama alizovaa huyo brazamen hapo zinavaliwa wapi? na hivyo viatu vyake navyo? Mbona humu mitaani sijawahi kumuona mtu hata mmoja akivaa nguo kama hizi au viatu kama hivyo? Jee vinauzwa maduka gani na anauziwa nani? wajuzi wa mambo haya naomba mnitoe tongotongo tafadhali.

    ReplyDelete
  2. Mdau wa kwanza kutoa maoni hapo juu hujakosea hata kidogo kwani na mimi masuala yako wewe ni sawa ninayojiuliza mimi kwahio umenisaidia kuuliza tusubiri jibu pengine tutapewa

    ReplyDelete
  3. Matangalu nakuondoa tongo tongo zano: Hawa huwa wanaonesha UBUNIFU si lazima nguo watu wanazovaa sana. Ndio kazi yao ilivyo kwenye anga za kimataifa. Ukiishia kuonesha kanga na misulu tu basi wewe utakuwa ni mbunifu local - hutafanikiwa kimataifa. Mambo mengi uliyosoma na paper ulizoandika kwenye mitihani unatumia kwenye maisha yako ya kila siku? Hapana - ila zimekusaidia kuwa mdadisi zaidi! Vile vile the whole thing ni ENTERTAINMENT.

    ReplyDelete
  4. Mimi nadhani haya mambo ya umodo ni ya kuiga hawa wa magharibi.Ni juzi tu hapa nimeona ma modo wetu wamerudi kushiriki mashindano ya kimataifa na wamekuja na malalamiko ya kuwa wanabaguliwa.Sioni ajabu kwa wenzetu walivo na dharau kwa sababu nimeishi nao miaka 11 na kujiona ni wa bora kwa kila kitu.Kwa ushauri wangu tu ningeomba mtafute ubunifu tofauti hata kama mtaibia kidogo lakini yaendane na tamaduni zenu.Onyesheni mitindo ya kuvalika na jamii kwa wakati wote.Kama alivosema mdau kuhusu viatu,ni kweli na sidhani kama unaweza kuvaa hasa miji ya joto kwa hapa kwetu.

    ReplyDelete
  5. Nadhani aliyetoa ufafanuzi hapo juu amelenga vizuri. Ni kwamba wanaangalia fani inavyoendeshwa kimataifa sababu na wao wanakwenda kushiriki huko. Na wa Ulaya huwa wanaonesha vipaji kwa mitindo mingi tu ya ajabu ajabu ambayo watu hawavai. Tuendane na wakati la kwenda na viwango vwa kimataifa la sivyo tutabaki socially isolated na criticism zetu KAMA WAKATI WA NYERERE...Google tu fashion shows utaona mavati mengi tu ambayo watu hawavai. Kuna mawavi hata wa maboksi lakini theme inakuwa ni "environment" - - wewe unaweza vaa maboksi?

    ReplyDelete
  6. EBO! sasa kuna maana gani ya kubuni kitu ambacho hakitatumika?

    ReplyDelete
  7. Wewe Anony wa Frid. Nov. 11, 02: 37:00pm 2011

    Bra bra bra. Bra bra. Bra bra bra bra, brab braaa, bra paper bra. INTERTAINMENT.

    Umejipinga mwenyewe! Umesema paper ulizoandika shuleni hazikusaidii kwenye maisha yako ya kila siku. Harafu umesema paper ulizoandika zinakusaidia kuwa kudadisi zaidi.

    Ninaamini kuwa ukiwa dakitari au muuguzi elimu uliyonayo itakusaidia wewe binafsi, familia yako na ndugu kuepuka
    maradhi au kuyatibu. Ukiwa mwalimu utatoa elimu. Ukiwa mwanasheria utatenda haki na kuitetea haki. Ukiwa askari hutapokea rushwa, nk. Kwa maana nyingine ni kuwa elimu uliyonayo ni vema ikusaidie katika kuishi vema. Kama elimu yako haikusaidii katika maisha ya kila siku, basi kuelimika kwako ni bure. Paper ulizoandika zinakusaidi kukamilisha maisha hasa juu ya utafiti ulioufanyo juu jambo furani ulipokuwa chuoni!! Bwana wee asipotoshe, wala usitoe maoni ukiwa na steam kichwani.

    Unapovumbua kitu ni lazima uanze kukitumia wewe mwenyewe ili ukitangaze kwa watu wengine wakifahamu , wakipende na hadi wakinunue. Kwa hiyo basi ni muhimu wabunifu wa mavazi kama watabuni mitindo inayokubalika na wazalenda wa tz ambao watakuwa wa kwanza kuivaa. Huwezi kuonyesha mavazi yako harafu siku ya party, au kanisani au msikitini au ufukweni ukavaa mavazi ya watu wengine. Kwanza watakushangaa. Mambo haya sio rahisi, inahitaji kujikomboa ki-fikra kwanza. je, mko tayari?
    Bra, bra, braaa, bra.

    ReplyDelete
  8. NYIE MNAOPINGA ANZISHENI FASHION INDUSTRY YENU ISIYOKWENDA NA TREND ZA KIMATAIFA MUONE MTAISHA WAPI. WAO WANAOFANYA HIVI NDIO WANAISHI KWA FANI KAMA ILIVYO SASA. NYIE ANZISHENI KWA CRITICISM ZENU MUONE KAMA MTA SURVIVE. MNACHOJUA NI CIRICISM TU - HII NI KAZI YA WATU. SARAKASI TUNACHEZA ZA KICHINA, KUNG-FU ZA KICHINA NA JAPANI NA FASHIO SHOW NI WESTERN. THATS THE WAY IT IS - BLAH BLAH BLAH!!!!! (NOT BRA!!! - KURYA)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...