Wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya kichina iitwayo China Railway 15Bureuau Group Corporation (CR 15G) Newcentry Company Limited wakijenga daraja katika kijiji cha Matai wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa hivi karibuni katika barabara ya Sumbawanga – Matai – Kasanga inayotengenezwa kwa kiwango cha lami na kampuni hiyo ya ujenzi hata hivyo kazi katika barabara ni za kusua kusua kufuatia Serikali kushindwa kuwa lipa wakandarasi hao malipo yao kwa wakati (Picha na Peti Siyame)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Mkuu sio barabara hiyo tuu ambayo ujenzi wake unasuasua, sisi tuko huku sumbawanga tunaona hata barabara ya kwenda mpanda, kuna wakandarasi wawili nao pia wamesimamisha kazi kwasababu serekali haina hela ya kuwalipa!! karibu miezi miwili sasa hakuna kinachoendelea, nasahangaa kuona waziri mwenye dhamana kuongea upuuzi kwenye media... hebu ndugu zetu waandishi wa habari njooni wenyewe huku mjionee na muueleze uma ukweli!!... tukisema serekali imefilisia wanakuwa wakali!!

    ReplyDelete
  2. Eti hii ni kampuni moja au?

    China Railway 15 Bureau Corporation (CR 15G) Newcentury Company Limited!

    ReplyDelete
  3. dooh! hata mimi hapo nimekoma na jina la kampuni si mchezo

    ReplyDelete
  4. Ha Ha Haaaaaaaaaaaaaaaaa. Yetu macho. Hawana hata kazi kwao hawawezi kupewa ujenzi wa namna gani huo? Waafrika ni wajinga wakiona ngozi nyeupe basi tunawatetemekea na kuwapa kila kitu.Contract za kwenye baa hizo.

    ReplyDelete
  5. hii kali, karne ya leo bado wanajenga daraja magari mawili hayawezi kupishana, kama wami. upuuzi mtupu :(

    ReplyDelete
  6. nadhani hilo daraja lipo muda mrefu (kwa mtazamo tu) -- na hao wachina wanaunganisha tu barabara yao

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...