Hii ni Studio inayotembea ambayo ipo pale Nyerere Square mjini Dodoma,ambapo utawakuta wapiga picha wengi wakiwa katika shughuli mbali mbali za upigaji picha,na hapa jamaa alimpiga picha ya passport size mteja wake huku kitambaa kikiwa kimeshikiliwa na mtu mwingine kwa nyuma,kama walivyonaswa na kamera man wa Glogu ya Jamii.
 "Usicheke sana,halafu weka kichwa kwa hivi"
 "Sogea kwa hivi tena."
"Daaahh.....!! wee Dada mgumu kuelewa,hebu sikaka namna hii na kichwa weka hivi." ndivyo alivyokuwa akiongea mpiga picha huyo wakati akimuelekea mteja wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kama ni ya visa watamkatalia. Hawataki picha za kucheka (no smile!)

    ReplyDelete
  2. Mdau wa MaguNovember 21, 2011

    Aaaaaa
    Ndo mpaka amsogelle hadi vifua vikutane. Mashavu na kugusa dimple ndo mpaka aguse?
    Hizi zama za memory card sio Konica na kodak Gold film. piga picha huku ukielekeza then choose the best photo ndo uprint.

    ReplyDelete
  3. Hutakiwi kumshika unaharibu hair dressing yake, we vipi.

    ReplyDelete
  4. MDAU WA MAGU AFADHALI HUYO MPIGAJI PICHA,JE HUYO ALIYESHIKA KITAMBAA NYUMA,MTAZAME ALIVYOJIBANA,ANAJIPONEA TARATIIIBU.FISADI MKUBWA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...