Jamaa akiwa kauchapa usingizi kwa pozi la namna yake huku kichwa akiwa amekiweka kwenye baiskeli yake ili wajanja wasije ondoka nayo,kama alivyonaswa na kamera man wa Globu ya Jamii katika mitaa ya Moshi,mkoani Kilimanjaro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Sijalala! Utauwawa bure!

    ReplyDelete
  2. Kwa wazungu, amini usiamini, jamaa ingebidi aweke kichwa chake au miguu/mikono yake kwenye kiti. Jamaa wanaiba viti vya baiskeli balaa. Ndio maana hata kwenye migahawa unakuta mtu kakaa hapa na pembeni kuna kiti cha baiskeli. Akipaki baiskeli nje anakichomoa.

    ReplyDelete
  3. Wazungu gani hao? Nimewahi kusikia Waholanzi kwa kawaida huwa hawaibi baiskeli wanaazima tu

    ReplyDelete
  4. Hahahha..mdau wapili umenichekesha sana..Basi hapa Ubatani(Uturuki) huwa wanaiba ringi yani frame hawana kazi nazo wallah nikweli na tushaibiwa sana ringi mpaka tukawa twacheka wenyewe kwamba Bongo wanaiba frame ndo dili huku jamaa wanaiba ringi ndo dili..na ww unasema wazungu kwao dili kiti..hahahaha..tabu sana humu duniani.

    ReplyDelete
  5. We anonym 25 nov, 07.37;00 wazungu wa wapi hao unatudanganya? Wazungu wa huku niliko hata baiskeli inalala nje na hakuna noma. Ukiwa unashop na ulikuwa na baiskeli unaiegesha eneo maalum la baiskeli ukishaifunga basi hakuna wa kuichukua. Tena kwa wazungu camera kila kona. Don't lie again to the people who doesn't know

    ReplyDelete
  6. Kama mdau wa pili alimaanisha wazungu wa Canada basi ni kweli kabisa, huku jamaa wanakwiba viti vya baiskeli balaa.

    ReplyDelete
  7. Hahahaha...jamaa ameweka ''lock'' kufuli ya kimtindo...alimradi asiangukiwe na nyoka au akiingizwa puani ulimi na kenge!

    ReplyDelete
  8. Usingizi ni ajizi nyumba ya njaa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...