Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kusini Jackson Kiswaga akiongea na wazazi na wanafunzi wa kata ya Kalenga Mkoani Iringa wakati wa hafla ya kuwakabidhi msaada wa madarasa mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 29 kwa shule ya sekondari ya Lipuri ya mkoani humo ,yaliyojengwa na Vodacom Tanzania kupitia mfuko wa kusaidia jamii”Vodacom Foundation”Kulia ni Afisa Elimu wa Sekondari za Wilaya ya Iringa William Mkangwa na Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule.
Afisa Elimu wa Sekondari za Wilaya ya Iringa William Mkangwa akikata utepe kuashiria kupokea msaada wa madarasa mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 29 yaliyojengwa na Vodacom Tanzania kwa kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii”Vodacom Foundation”kwa ajili ya shule ya sekondari ya Lipuri, iliyopo kata ya Kalenga mkoani Iringa, wakishuhudia kutoka kushoto ni Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule,Mkurugenzi wa Vodacom Kanda ya kusini Jackson Kiswaga,Diwani wa kata ya Kalenga Ameria Galinoma na diwani viti maalum Shakila Kiwanga.
Mkuu wa mfuko wa kusaidia Jamii wa Vodacom Tanzania Yessaya Mwakifulefule akiteta jambo na mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lipuri iliyopo kata ya Kalenga mkoani Iringa Agness John,mara baada ya kukabidhi msaada wa madarasa mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 29 yaliyojengwa na Vodacom Tanzania kupitia mfuko huo.Akishuhudia watatu kutoka kulia ni Mkuu wa shule hiyo Alex Mwakiyanga akiwa na walimu wa shule hiyo.
Haya ndiyo madarasa mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 29 yaliyojengwa na Vodacom Tanzania kwa kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii”Vodacom Foundation” kwa ajili ya shule ya sekondari ya Lipuri ya mkoani Iringa.
Wazee wa kabila la Kihehe, kata ya Kalenga mkoani Iringa wakimpa heshima ya kichifu Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kusini Jackson Kiswaga kwa kumkabidhi mkuki baada ya kumvisha vazi la mgorole ikiwa ni heshima kubwa kwa mkoa huo wakati walipofika kukabidhi madarasa mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 29 katika shule ya sekondari ya Lipuri mkoani humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. hayo madarasa hayana thamani ya hiyo hela come on vodacom!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Yaani hivyo vibanda wiwili ndio zaidi ya milioni 29 sio mchezo
    mdau
    kisiju pwani

    ReplyDelete
  3. hakuna darasa la milion hizo hapo, jamani tusidanganyanye. cheki vimilaango viduchuuuu. wizi mtupu

    ReplyDelete
  4. VODACOM VODACOM KAZI NI KWAKO!

    ReplyDelete
  5. Je kwa wanaume kufunga kilemba kichwani na kujirushia vikoi namna hii ni mila ya kabla gani? hope si wamasai

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...