Meneja Masoko wa TBL, Fimbo Buttalah akimkabidhi mshindi wa kwanza wa Ubunifu toka chuo kikuu cha SAUT Bwana Simon Joseph Kiasi cha 700,000 alipoibuka mshindi kwenye Redds Uni Fashion Bash mkoa wa Mwanza.
Mwakilishi wa TBL Mkoani Mwanza akimkabidhi zawadi ya Tsh 500,000 mshindi wa kwanza wa upande wa mitindo,Oliver Kikare baada ya kuibuka mshindi kwenye fainali za Redds Uni Fashion Bash Mkoa wa Mwanza, Anasoma Chuo kikuu cha SAUT
Washiriki upande wa mitindo kwenye Redds Uni Fashion Bash wakipita kwa pamoja jukwaani kabla ya kutangazwa kwa washindi,hapa walikuwa wakionyesha mavazi maalum kwaajili ya muda tofauti tofauti wa mchana na usiku.
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva,Mwana Fa akifanya vitu vyake kwenye Tamasha hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa M10 kwenye chuo kikuu cha Saint Augustino jijini Mwanza usiku wa jana.
Majaji wa tamasha hilo,Costantine Magavile na Mr Tanzania walishiriki kwa pamoja kumtafuta mwana mitindo na mbunifu wa Redds Uni Fashion Bash jijini Mwanza wakitazama kwa umakini washiriki wakati walipokuwa wakipita jukwaani, nyuma yao ni wanavyuo wakishangilia katika moja ya matukio ya washiriki.
Meneja masoko wa TBL,Fimbo Buttalah (pili kushoto) akiwa na viongozi wengine wa TBL wakifuatilia kwa ukaribu mashindano hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...