Na Mery Ayo,Arusha

ZAIDI ya watu milioni moja hapa nchini wanaishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa takwimu za mwaka 2007-2008 ambapo takwimu hizo zimepungua tofauti na mwaka 2003.

Takwimu hizo zimepungua baada ya tume ya kuthibiti ukimwi tanzania (TACAIDS) kuweka sera na mikakati mipya ya kuhakikisha kuwa jamii inapata elimu ya kutosha kuhusu namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi .

Hayo yalisemwa na afisa uhusiano wa tume ya kuthibiti ukimwi Tanzania (TACAIDS) bi Glory Mzirai alipokuwa akitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa redio za jamii wa mikoa ya arusha,kilimanjaro,manyara na tanga katika semina iliyofanyika mjini hapa.

Bi Glori alisema kuwa tafiti hizo zinaonyesha kuwa wanawake wengi ndio wanaoongoza kuwa na maambukizi zaidi ya wanaume .

"Tafiti zinaonyesha kuwa asilimia moja ya wanaume wana maambukizi ya virusi vya ikimwi lakini asilimia kubwa wanawake ndio wanaoongoza kuwa na maambukizi kwa kuwa wengi wao bado walikuwa hawajapata elimu ya kutosha juu ya kujikinga na virusi"alisema Glory.

Aidha aliongeza kuwa tafiti hizo zinaonyesha kuwa wanawake wenye umri kati ya miaka 30-34 ndio ambao wanaishi na maambukizi ya virusi wakati wanaume wenye virusi ni kuanzia umri wa kati ya mika 40-44 .

Alieleza kuwa tafiti hizo zinaonyesha kuwa watu waishio mijini ndio ambao wana maambukizi ya virusi zaidi ya wale waishio vijijini ambapo pia takwimu zinaonyesha kuwa wanawake wa mijini ndio wanaoongoza kuwa na maambukizi zaidi ya wale wa vijijini.

"Maambukizi yanazidi kwa wanawake kwa kuwa hawakuwa na elimu ya kutosha juu ya namna ya maambukizi ya kuthibiti ukimwi hivyo ni jukumu lenu waandishi wa redio za jamii kuwaelimisha namna ya kuthibiti ukimwi wakati mkiwa mkiendesha vipindi vyenu"alisema

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tujitahidi kubadilika ili kupunguza maambukizi ya VVU...acheni utamaduni wa ngono zembe wanawake msiwe wabishi, taarifa hii ipo wazi!.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...