Wakati wa kuazimisha Miaka 50 ya uhuru wa Tanzania hapa Jijini London Ubalozi wetu katika siku ya Ijumaa Tarehe 9 Desemba 2011 ulipata fursa pekee ya kukutana na kumpongeza afisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ndg. Semu Mwakyanjala ambaye pia ni mwanafunzi wa shahada ya Pili( Masters Degree in Communication, culture & Media) katika chuo kikuu cha Coventry alieshinda tuzo ya kuandika insha kuelezea jinsi gani nchi ya Ujerumani itakavyokua mwaka 2051.

Aidha Mh. Balozi Kallaghe alimpongeza sana Afisa Semu kwa juhudi zake kwa kufanikiwa kushinda tuzo hii na kuiletea heshima Tanzania Ughaibuni na kuwahamisisha watanzania wote  kusoma na kufanya kazi kwa bidii zaidi. Wakati akiongea na waandishi wa Habari afisa Semu alianza kwa kutoa shukrani kwa familia yake, wafanyakazi wenzake kutoka TCRA na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa kumwezesha kufikia hatua aliyopiga leo.
Kutoka Kushoto Naibu Balozi Chabaka, Semu Mwakyanjala na Tim 
Afisa Semu Mwakyanjala akisema machache baada ya kupokea tuzo hiyo
Baraka Baraka  wa Urban Pulse akifanya Mahojiano na afisa Semu Mwakyanjala baada ya kupokea tuzo yake jijini London. Bw Mwakyanjala, ambaye kabla ya kuhamia TCRA alifanya kazi kama mwandishi na mpiga picha kwa miaka kadhaa katika gazeti la kila siku la serikali la Daily News ambapo akijulikana kwa jina la utani la 'CNN' kwa umahiri wake wa kupata habari na picha motomoto kila mara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Jamaa wa tbl alishinda tuzo kwa kufanikiwa kuivisha pombe.

    ReplyDelete
  2. HONGERA SANA TENA SANA, UMETUPA UMARADUFU SANA WABONGO TUNAJIVUNIA, KAKA, DUH, HATUKUJUA UNA AKILI KIBOKO HIVI, HONGERA SANA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...