Balozi wetu wa kudumu Umoja wa Mataifa,New York,Mh.Ombeni Sefue(shoto mwenye miwani) akiingia ukumbini kujumuika na Watanzania wa New York katika sherehe za Miaka 50 ya UHURU iliyofanyika Jumamosi December 10,2011 kulia ni Mh.Naibu Balozi Mama Munanka.
 Balozi wa kudumu waTanzania umoja wa mataifa New York,Mh. Ombeni Sefue(shoto) akisindikizwa na mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania New York,Bw, Hajji Khamis alipokua akiingia ukumbini hapo.
 Balozi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa,New York,Mh.Ombeni Sefue akipiga picha ya pamoja na Balozi wa Somalia katika sherehe za miaka 50 ya UHURU,Tanzania Bara zilizofanyika New York Jumamosi December 10,2011
kutoka shoto ni Mama wa mitindo Asya Idarous Khamsini,Mh. Balozi Ombeni Sefue,Balozi wa Somalia akiwa pamoja na mkwewe wakipata picha ya kumbukumbu katika sherehe za miaka 50 ya UHURu Tanzania Bara zilizofanywa na Jumuiya ya Watanzania New York.
 Mh.Blalozi Ombeni Sefue(wapili toka shoto) akiwa pamoja na Mkewe(kati mwenye nguo nyeusi) Mh,Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Marekani,Mama Munanka(wapili toka kulia) wakiwa meza kuu na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania wa New York katika kusherehekea miaka 50 ya UHURU Tanzania Bara ilyofanyikia katika Ukumbi wa Malcolm X,Manhattan,New York,Jumamosi December 10,2011
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya wa Tanzania New York,Bw,Hajji Khamis akisema machache kuhusiana na miaka 50 ya UHURU kabla hajamkaribisha Mh.Balozi Ombeni Sefue.
Mh.Balozi Ombeni Sefue ambae ni Balozi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa New York akiongea na Watanzania wa New York katika kusherehekea miaka 50 ya UHURU,Tanzania Bara iliyofanyika Jumamosi December 10,2011,mjini humo.
 
Mh.Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico,Mama Munanka,akiongea machache kwa niaba ya Balozi Mh.Mwanaidi Maajar ambae hakuweza kuhudhulia sherehe hizi za miaka 50 ya UHURU kutokana ya Yeye kuwepo Tanzania.
 Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania New York ukipiga picha ya pamoja na Balozi Sefue,Mkwewe na Naiibu Balozi wa Tanzania Nchini Marekani Mama Munanka.
 Mh.Balozi Ombeni Sefue pamoja na Mkewe katika picha ya pamoja na Uongozi wa Jumuiya ya Watzanzania,New York na wadhamini wa sherehe hiyo ya miaka 50 ya UHURU iliyofanyikia katika ukumbi wa Malcolm X,Manhattan,New York,Jumamosi Decenber 10,2011.
 Juu na chini ni  Mh.Balozi Sefue pamoaja na Mkewe wakipiga picha ya pamoja na Watanzania waliojumuika pamoja katika kusherehekea miaka 50 ya Uhuru New York,NY.
 Mh.Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico,Mama Munanka akiwa anajisaidia mwenyewe kupata maakuli katika sherehe za miaka 50 ya UHURU wa Tanzania Bara zilizofznyika New York kushoto ni Balozi wa Somalia akiwa na mkwewe(kati)
 Balozi wa Somali(kulia) akiwa na mwenyeji wake Mh,Balozi Ombeni Sefue wakijisaidia kupata maakuli katika sherehe za miaka 50 zilizofanyika New York,NY Nchini Marekani.
Mh.Balozi Sefue akiendelea kujipakulia Maakuli

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hongera sana ubalozi USA.Nyie UK mmeona wenzenu hiyo ndio maana ya sherehe sio kuangalia mifuko yenu na mipangilio mibovu hongera sana new york shughuli imetulia.

    ReplyDelete
  2. Mbona picha zilizotoka ni za balozi tu. Vipi picha za watanzania wengine?

    ReplyDelete
  3. I see you Bea!

    ReplyDelete
  4. hebu malizia wewe wa hapo juu, hiyo mipangilio mibovu ya watu wa UK ni ipi ? wenzio wako mbele wanasafirisha magari, naona wewe kwenye ,umelala bado. seaboys

    ReplyDelete
  5. Sasa mbona ubalozi hautangazi hizi sherehe ili wengi wahudhurie?

    ReplyDelete
  6. Huyo Balozi mnaosema wa Somalia sio wa Eritrea? Maana mkewe ni mama Ashura Babu aliekuwa mke wa mmwanamapinduzi Abdulrahman Babu.

    ReplyDelete
  7. hongereni

    ila mkumbuke kwenu miaka hamsini huduma za uhakika hakuna.umeme ,maji n.k.mnapofanya sherehe kubwa hivyo pia mnakumbuka kwenu mlikotoka hapa nazungunzia mlikozaliwa? huko mnawasaidia vipi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...