Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba wakati wa halfa ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislam iliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiqaama Tanzania Tawi la Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika leo katika Ukumbi wa Karimjee jijini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Msaafu kutoka kwa, Sheikh Ahmed Mohamed Lbadry, baada ya kumaliza hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislam iliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiqaama Tawi la dare s Salaam na kufanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakati akiondoka kwenye Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam, leo  baada ya kumaliza shughuli ya hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislam iliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiqaama Tawi la Dar es Salaam.
Waumini wakiomba dua baada ya kumalizika hafla hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia gari alilopata nalo ajali Bw. Arif Yusuph, eneo la Mji wa Fiche Kilometa 100 kabla ya kufika Adis Ababa , wakati akitoka Kuhij Makha baada ya kugongana uso kwa uso na gari aina ya Hiace iliyokuwa imebebea Jeneza ikisafirisha msiba, katika ajali hiyo watu wote walisalimika na kurejea nyumbani. Makamu wa Rais alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislam iliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiqaama na kufanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo Desemba 12.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waumini na viongozi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Istiqaama, baada ya kumalizilika kwa hafla hiyo leo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal amewataka Waislam kote nchini kuhakikisha wanajiendeleza na kuacha kujilaumu hasa katika kuwekeza katika mambo ya maendeleo.

Dk. Bilal ametoa rai hiyo leo katika maadhimisho ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislamu (1433 Hijriyya) ulioadhimishwa na Jumuiya ya Istiqama (Istikama) ya Tanzania tawi la Dar es salaam katika ukumbi wa Karimjee.

“Wakati tukiadhimisha mwaka huu mpya tunapaswa kujikumbusha pia kwamba tunao wajibu wa kuhakikisha tunajiendeleza na kuacha kujilaumu hasa katika kuwekeza katika mambo ya maendeleo,” alidokeza.

Makamu wa Rais alisema katika kufanikisha hilo Waislam wanapaswa kuhamasisha na ikiwezekana kushirikiana na Serikali kuwekeza katika ujenzi wa nchi ukiwamo wa shule na katika utoaji wa huduma mbalimbali.

Alisema pamoja na kuwa anafahamu vyema kwamba mambo hayo yanafanyika lakini aliwataka kuongeza nguvu zaidi na kusisitiza uwekezaji ufanywe kwa malengo maalum ya kutoa huduma na elimu iliyo bora ili wananchi na vijana wafaidike na uwekezaji huo.

“Watoto wetu wamesoma kasida hapa, wameonesha wana hamu ya kutaka kujua zaidi. Tunahitaji watoto wetu wasome, tunahitaji familia zetu ziwe na afya bora. Kwa kutambua hili tunapaswa kushikamana pamoja katika kukuza huduma za maendeleo huku tukibakia kuwa wacha Mungu, alisema Dk Bilal na kuongeza

“Tufanye hivyo kwa lengo maalumu. Kama ni kuwekeza kwa kujenga zahanati, tuhakikishe tunajenga zahanati zinazotoa huduma bora na nzuri kuwasaidia wananchi, wanawake wajawazito na watoto. Kama ni ujenzi wa shule, ziwe shule za mfano zinazotoa elimu iliyo bora.”

Dk. Bilal alitumia fursa hiyo pia kuwataka Waislam wahamasishe jamii kumcha Mungu ili kupunguza mabadiliko ya tabia na mambo yanayokuja kwa kasi hasa katika kipindi hiki cha utandawazi .

Katika risala yao Jumuiya hiyo ya Istiqama tawi la Dar es salaam waliipongeza Serikali ya Muungano na ile ya Mapinduzi Zanzibar kwa uamuzi wao wa kupinga ndoa za jinsia moja kwa kuwa zinaenda kinyume na mila na desturi za Watanzania.

Naye Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhaji Mussa Salum aliiomba Serikali isibadili msimamo wake wa kupinga ndoa za jinsia moja baada ya Marekani kuungana na Uingereza katika hilo kwa hofu ama woga wa kukosa misaada.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...