Hivi ni hatua gani za lazima zinazopaswa kuchukuliwa ili kuwafanya hawa madereva wa daladala kufuata sheria za barabarani bila kushurutishwa??maana hebu ona hapa anachokifanya,kasimama barabarani anapakia abiria huku magari mengine yamepanga msururu nyuma kusubiri amalize.halafu hana hata wasiwasi kwamba kuna magari yanasubiri nyuma yake.
Home
Unlabelled
daladala ..... daladala..... daladala........!!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
sababu ni kwamba anahofia kukosa abiria mbele iwapo ataruhusu mabasi mengine kupita.hapa kinachotakiwa ni kumpiga faini dereve.
ReplyDeleteKwa nini madereva tu? hao raia wanaopanda na kuteremka pasipo vituo je? Akizikuta fedha lazima azichukue, si ndizo anazo tafuta?
ReplyDeleteHiyo ni public transport.Nchi nyingine public transport inapewa first priolity lakini kwa sababu bongo hamjui mnalalamika tu.Sehemu nyingi zinazotumia left hand side,left side inakua ni kwa ajili ya buses,taxis na gari nyingene zenye abiria zaidi ya mmoja lakini kwa sababu bongo utaratibu huo hakuna wenye magari yao wanadharau public transport.
ReplyDeletemdau Sugu.
Hiyo ni public transport.Nchi nyingine public transport inapewa first priolity lakini kwa sababu bongo hamjui mnalalamika tu.Sehemu nyingi zinazotumia left hand side,left side inakua ni kwa ajili ya buses,taxis na gari nyingene zenye abiria zaidi ya mmoja lakini kwa sababu bongo utaratibu huo hakuna wenye magari yao wanadharau public transport.
ReplyDeletemdau Sugu.
Usafiri wa umma ndio namba moja1 halafu mtu mmojammoja ndio anafuata jamani.Sasa nyie wenye magari binafsi mnapenda haraka kuwahi kwa hiyo msiwashumbue watu wengi wanao tumia bus.
ReplyDeleteMUHIMU KILA MTU AMSUBIRI ALIYETANGULIA KAMA KUNA NAFASI YA KUOVER TAKE NDIO APITE.
Msitufanye kama sisi hatujatembelea nchi nyingine! Hakuna nchi inayoruhusu gari eti kwa sababu ni public transport basi isimame barabarani badala ya kituoni. By the way mleta mada hajasema kuwanyima kipaumbele bali kasema "kuwafanya wafuate sheria". Sasa kama hao huko ulikotembelea wanapewa priority kusimama popote basi wanafuata sheria za huko kwao kwa na sisi kwa sababu hatuna sheria za kupaki magari holela basi inabidi wafanye kama sheria inavyotaka!
ReplyDeleteTatizo mdau wa Sat Dec 31, 08:41:00 PM 2011, barabara zetu sehemu zingine vituo hata havieleweki, hakuna vibao vya kuonesha vituo, barabara nyembamba, na kama pana basi hata hizo priority lane za public transport hazijachorwa,,,kwa kweli tunahitaji mabadiliko! Tunajitahdi lakini bado tunahitaji kuongeza kasi! Sasa hivi watanzania wanaokwenda nje kimasomo na kikazi ni wengi, Tujifunze kutoka kwa wenzetu na kuleta mabadiliko kwetu hatua kwa hatua,,,inawezekana! Mdau-Canada
ReplyDeleteNdio maana wengi wanafeli mitihani, kwasababu wanakurupuka kujibu kabla hajaelewa swali, swali ni nini kifanyike sheria zifuatwe katika mazingira ya barabara hizihizi na sheria zetu hizihizi? maoni yangu, askari wa usalama barabarani wawajibike na adhabu aadhibiwe muhusika halisi, mfano askari akimkamata dereva huyo amtoze faini kwa namba ya leseni yake, si kwa namba ya gari, au amuweke dereva mahabusu kwa ajili ya hatua nyingine na mwenye gari (bosi wa dereva) aitwe aje achukue gari yake akatafute dereva mwingine. halafu tuziangalie sheria za wenzetu kama zitatufaa na kama zitaendana na mazingira yetu.
ReplyDeleteFIRST OF ALL HAKUNA KITU KINACHOITWA KUFUATA SHERIA BILA KUSHURUTISHWA. HAPA HATA MBINGUNI.NDIO MAANA HATA KATIKA VITABU VYA DINI VINASEMA USIPOFUATA SHERIA UTAHOMWA MILELE. SULUHISHO DOGO SANA. KUWAPA WANANCHI UWEZO WA KUMKAMATA NA KUPIGWA FAINI BILA LONGO LONGO. NENDA MBEYA UKAONE INAVYOFANYA KAZI.
ReplyDeleteNyie pigeni kelele kisha najua mtalala tu. Acheni tufanye kazi sisi majungu hayana madhara kwetu.
ReplyDeletekweli kabisa wanaohusika daladala zimezidi haswa kituo cha ilala kwa mlangoni kwa ofisi ya mkuu wa mkoa dar na pale kigogo round about kwenda magomeni wanasimama barabarani kabisa hawajali kuingia kwenye vituo kupaki vizuri tafadhali muhusika fanyeni kazi bwana tumechoka!!!
ReplyDelete