Ukumbi mpya wenye hadhi ya kimataifa wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam unatarajiwa kuzinduliwa rasmi Januari Mosi, 2012 na kusindikizwa na burudani ya nguvu kutoka kwa wasanii kibao wakiongozwa na Juma Kassim Kiroboto "‘Sir Nature" sambamba na Kundi la Muziki wa Kizazi Kipya la Gangwe Mob.


Nature, Haroun Kahena ‘"Inspekta" na mwenzake Karama Bakari ‘"Luteni Kalama" wameahidi kuonesha ukongwe wao katika gemu na kuandika historia ya kipekee kwa kuangusha bonge la shoo ya uzinduzi, ambapo watakamua steji moja na Mzee Yusuph atakayekuwa na kundi zima la Jahazi Modern Taarab bila kuwasahau Extra Bongo chini ya Ali Choki ‘"Mzee wa Farasi".



“Kama bado ulikuwa unaamini kuwa Mbagala ipo nyuma kwa burudani za kimataifa, basi umechelewa kujua kwani Mwaka Mpya ndiyo siku ambayo Wabongo watajionea wenyewe maujanja yanayopatikana ndani ya Dar Live!
Haya ni mapinduzi katika tasnia ya burudani,” alisema Nature, juu ya kuzaliwa kwa Disneyland ya Bongo!



Hii ni patgazeti tu. Kwa picha kamili
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Haufikii uwanja wa Kariakoo, Zanzibar!!

    ReplyDelete
  2. so what?! wabongo bwana...

    ReplyDelete
  3. tuacheni compare kila kitu jamani, hivi tunajua Disney iko vipi. hiyo ni Disney au ni kama public park ambayo watoto wanaenda cheza bure?

    ReplyDelete
  4. sasa hivi hapo tutaona hayo magari yametapakaa mavi, na mengine yanaendeshwa mitaani huko uswahilini. bongo bwana yaani watu hawajaelimika hata kidogo.

    ReplyDelete
  5. Tunaweza iita Disney land ya Bongo kimasifa tu, lakini naona bado hata Zero haijafikia. kwani pembeya hizi ughaibuni ni kawaida tu katika mitaa. Hata hivyo siombaya angalu wenetu wataosha macho.

    Hongera mjariamali

    ReplyDelete
  6. Mbona hii michezo ya kuchezea inaonekana kama si imara vile na haitadumu sana. Natumaini watakuwa wamezingatia ubora na viwango

    ReplyDelete
  7. wewe mtoa maoni hapo juu heti haufikii uwanja wa Kariakoo huko Zenji,Sasa wewe unataka watoto wa Dar wapelekwe huko Zenji?watoto awajui hilo..wao hata mavumbi,michanga kwao ni sawa tuuu..ONGERENI SANA MLIOJENGA SEHEMU HII::SAFI SANA MUNGU AWABARIKI ZAIDI:

    ReplyDelete
  8. HAHAHA ATI DISNEYLAND LOL
    HIZO NI PARK ZA MITAANI TU HUKU MTONI KILA KWENYE COUNCIL HOUSE COMPLEX WAKO NAZO HIZO MBELE YA BLOCK NA ZIKO OPEN ALL DAY FREE KWA WATOTO WAO.

    ReplyDelete
  9. Naam bongo mambo safi sana,utafikiri ulaya. Ila wajitahidi bei isiwe kali kama ya Ulaya ili walalahoi nao wajinome.

    ReplyDelete
  10. Nyie mnao lalamika si mjenge yenu? Mwanzo wa hesabu ni sifuri, moja ...... Wabongo mnapenda kubonda sana. Hakuna mtu alielazimishwa kwenda?
    Afadhali mngeuliza hizo mashine zinataumia umeme wa Tanesco au umeme wa nguvu za jua!

    ReplyDelete
  11. Mimi watu wanaoponda vitu vya nyumbani kwa kushobokea vya ughaibuni wamenichosha humu kwenye blog ya jamii. Huko ulaya kwenyewe hata mtoto wako ukimpeleka park wazungu wanamuangalia kama kinyesi mmeng'ang'ania tu huku mnakufa na tai shingoni, frustration mnazitolea kwenye mablog. Nendeni mkawasifie wazungu kwenye mablog yao, hapa kama kitu mnaona kihuko ulaya kwenu hakifai kaeni na mawazo yenu matumboni. Kibongobongo kila mtaa hata lami hatuna ukitujengea sehemu ya kuwapeleka watoto wetu walau Krismas au Iddi tunashukuru Mungu. Hongereni kwa hii michezo ya watoto, ni mwanzo mzuri.

    ReplyDelete
  12. KIINI CHA DHARAU YA WABONGO;

    Hao wanao ponda hawana lolote kwa kutokana na hulka mbaya ya wa Tanzania ni kudharauliana kwa misingi wa maeneo!

    Kitu ambacho hakina msingi kabisa, kwa vile mambo yanabadilika kulingana na muda, mfano timu ya Mpira inaweza kuwa na kiwango cha juu wakati fulani lakini baadae ikashuka, au ilioyo chini ikatokea ikapanda!

    Hali hiyo vile vile ipo kwa viwango vya wachezaji ktk timu mmoja hadi mwingine,

    Vile vile hali halisi ya maisha mtu hadi mtu (kubali au kataa)inabadilika kwa misingi ya kushuka na kupanda!


    Na hata maeneo tunayoishi kama hapa Dar Es Salaam vile viwango hushuka na kupanda!

    HAPO KTK HII DAR LIVE HAKUNA KINGINE WANACHO PONDA KWA HULKA MBAYA YA WA TANZANIA NI VILE HIYO IPO MBAGALA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...