MTANGAZAJI wa muda mrefu wa iliyokuwa Redio Tanzania Dar es Salaam RTD na baadae Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC),Halima Mchuka amefariki Dunia. 

Taarifa za kuaminika kabisa kutoka katika vyanzo vya Globu ya Jamii,inaeleza kuwa  Mtangazaji huyo ambaye alikuwa na kipaji kikubwa cha utangazaji amefariki  Dunia mapema leo asubuhi wakati akiwa hospitali kutokana na kuanguka baada ya kupatwa na stroke ya gafla wakati akiwa kwenye kindindi.

Halima Mchuka inaaminika kuwa alijiunga na Radio Tanzania Dar es Salaam mwaka 1994 ambapo alifanya kazi katika idara ya Habari na idara ya mipango.

Wadau wengi wa RTD na baadae TBC-Taifa wanamkumbuka sana mama huyu wa watoto wawili kwa kuwa mwanamke wa awali kuangaza mpira katika ukanda wetu huu wa Afrika Mashariki na kati.

“Unapotaja mpira wa miguu wakati huu huwezi kusahau kipindi cha michezo cha RTD cha saa mbili kasorobo na huyu dada Halima Mchuka.”alibainisha Idd Pazi mmojawapo wa wachezaji nguli wa Tanzania wa wakati huo.

Kwa hakika si wasikilizaji wa RTD na wanamichezo tu bali  hata watu wa Karibu ambao waliwahi kufanya nae kazi tunamtazama kuwa ni mtu mpole mwenye huruma na kusaidia wenzake pale penye tatizo ambalo yeye anaweza kulitatua.

Mungu ailaze Roho ya Marehemu Halima Mchuka mahala pema peponi 

-Amina

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mwenyezi mungu aiweke mahali pema peponi dada yetu mpendwa, tunakukumbuka sana. Sisi wenyeji wa MIONO tumepata pigo kubwa sana.

    ReplyDelete
  2. Soo sad!!
    Inasikitisha sana. Tumepoteza kipaji muhimu sana katika sekta ya Utangazaji.
    Mungu aiweke roho yake pema peponi.
    Amen!

    ReplyDelete
  3. Hakika tumempoteza mtangazaji mahiri...Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi..Amin

    ReplyDelete
  4. inna lillah wa innailaih raaajiun,tutakukumbuka sana kwa uwezo wako wa kutangaza soka kifasaha hadi nilikuwa nashindwa kukusoma,sijui kama itatokea karibuni!

    ReplyDelete
  5. Rest in Peace Halima!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...