Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Lawrence Mafuru (wa pili kulia) akisalimiana na Meneja wa Tawi la NBC Geita, Onael Mpeku katika hafla ya kumaliza mwaka iliyoandaliwa na mkurugenzi huyo jijini Dar es Salaam jana. Wa pili kushoto ni mke wa Mafuru, Noella na kulia ni Meneja wa NBC Kahama, Martin Mkanda.
Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, Maharage Chande (kushoto) akibadilishana na mawazo na Mkuu wa Mauzo Kitengo cha Makampuni,Minnie Adolf Kibuta katika hafla ya kumaliza mwaka iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru (hayupo pichani) jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Lawrence Mafuru (kushoto mstari wa mbele) pamoja na mkewe, Noella Mafuru (nyuma yake) wakiwaongoza baadhi ya wafanyakazi na wenza wao katika hafla ya kumaliza mwaka iliyoandaliwa na mkurugenzi huyo jijini Dar es Salaam jana.
Mshauri wa Habari wa NBC, Redemptus Masanja (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Mama Jane Dogani wakiselebuka pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa NBC na wenza wao, katika hafla ya kumaliza mwaka iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru (hayupo pichani) jijini Dar es Salaam jana.
Meneja Chapa na Matangazo wa NBC, Arden Kitomari (katikati) akifanya vitu vyake pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa NBC, katika hafla ya kumaliza mwaka iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC,Lawrence Mafuru (hayupo pichani) jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC na wenza wao, wakijimwaga ukumbini kusherehekea pati ya kumaliza mwaka iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Lawrence Mafuru (hayupo pichani), jijini Dar es Salaam jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AUDHU BILLAH!!
    HIVI KARIBUNI NILISOMA UTAFITI UNAOONESHA KUWA NUSU YA WAGONJWA WOTE WA MARADHI YA UKIMWI DUNIANI WANATOKA AFRIKA.
    NIKASHTUKA MNO.
    LAKINI LA AJBU NI KUWA HAO WAAFRIKA WENYEWE WALA MSHIPA HAUWAPIGI, HAWAJALI HATA CHEMBE.
    KWA MTAJI HUU, WASICHANA NA MAMA ZETU KUJUMUIKA KADAMNASI WAKIWA NUSU UCHI, HUKU NGUO ZILIZOSITIRI MAUNGO YALIYOBAKI ZIKIWA ZIMEWABANA MNO, NAJIULIZA, NINI HATIMA YA BARA LETU.
    NANI ATABAKI, NANI ATAENDELEZA AFRIKA KWA SABABU TUTAKE TUSITAKE, UKIMWI UNAELEKEA KUTUMALIZA VIBAYA TENA KWA KASI YA AJBU.
    NILIPOONDOKA NYUMBANI MIAKA KUMI NA TATU ILIYOPITA MAMBO YALIKUWA AFADHALI.
    SHETANI NAONA AMEONGEZA KASI, NGONO NA VISHAWISHI VYAKE VIMETAWALA KILA KONA!
    WATU HAWAJALI.
    NDIO USASA.
    HALI ITAKUWAJE MIAKA KUMI IJAYO? NAJIULIZA.
    NI MATUSI NA FEDHEHA KUONA WATZ TUMEENDEKEZA NGONO NA VISHAWISHI VYAKE KWA KIWANGO HIKI. HALI INATISHA, KILICHOBAKI NI KUOMBA REHEMA ZA MUNGU TU.
    PICHA KAMA HII INAONESHA KUVUTIA WENYE UCHU NA TAMAA ZA NGONO, ILA NI MACHUKIZO MAKUBWA MBELE YA MUNGU. NI AIBU, LAKINI ZAIDI NI BOMU AMBALO TAYARI LIMESHAANZA KUFUKA MOSHI, NA KULIPUKA KWAKE SIWEZI KU IMAGINE KIASI CHA MADHARA KITACHOTOKEA.
    NI UCHAFU WA KIWANGO CHA KUTISHA, WENYE IMANI YA MUNGU TUENDELEE KUMWOMBA MUNGU AYAOKOE MATAIFA YETU NA JANGA LINALOTUELEKEA KWA SABABU VISHAWISHI VYA NGONO WENGI TUMESHINDWA KUVIEPUKA ILHALI NAVYO NDIO KWANZA VINAONGEZEKA
    Mndengereko, ukerewe

    ReplyDelete
  2. wewe inaonekana hujaelewa kwanini ukimwi unawafuata zaidi weusi, kama ni kutembea nusu uchi basi nikuambie wazungu ndo wanatembea uchi sasa na wanafanya mapenzi kichafu sana ungetegemea ndo wafe zaidi na ukimwi kinyume chake tunakufa zaidi sisi weusi, hujui kwanini na sijui kwanini lakini usiseme kuvaa nguo za kubana wala kuvaa nusu uchi hiyo siyo sababu , tafuta sababu utapata, inaonekana hata hujatembea wewe, usingesema hivyo, nadhani unazunguka tu hapo hapo Tanzania ndo maana unasemahivyo, usiniudhi, mwulize hata Michuzi atakuambia.

    ReplyDelete
  3. Lawrence Mafuru siijui sana historia yake ya utendaji, lakin nadhani anaonekana kuwa mtendaji makini mwenye imani kubwa kwa watendaji wake...ambao wengi wao ni vijana...sina uhakika ni speculations tu.....

    tuombe mungu hii executive and vibrant nature yake ireflect maendeleo ya benki hii..

    ReplyDelete
  4. MDAU WA SUN DEC 18, 01:50:00 UNAJUA UNACHOSEMA?
    MIMI NAISHI ULAYA MWAKA WA 13 HUU, NIMETEMBEA NA NAJUA NASEMA NINI.
    HAPA UKEREWE UKIMWI UMEJAA TELE, I WISH UNGELIJUA HILO. HUO NI UKWELI SIKATAI, WIFE WANGU KILA ANAPOKUWA MJAMZITO HUPIMWA NA HUPEWA TAKWIMU.
    LAKINI KILA ANAELIA HULIA MAMAANGU, KIWANGO KINACHOATHIRIKA HUKU ULAYA HAKIFANANI NA HICHO CHA AFRIKA, SO WE HAVE TO BE MORE CAREFUL, MORE SERIOUS!!
    UNANIELEWA?.
    JE TUKIIGA KWENDA UCHI, TUNAJUA KUSEMA HAPANA?
    JE TUNA SHERIA ZINAZOMLINDA MWANAMKE NA KUMPA UHURU WA KUSEMA: YOU CAN WATCH BUT YOU CAN DARE TOUCH!!
    UNAYAJUA HAYO, AU TAMAA TU ZIMEKUTAWALA?
    WEWE UNADHANI KUTEMBEA UCHI SI TATIZO, INAWEZEKANA MWENZETU UNAJIRAMBA MIDOMO UNAPOYAONA HAYO, NDIO MAANA UNASEMA NAKUUDHI. SHETANI PIA ANAUDHIKA KUONA KUNA WATU TUNAOCHUKIZWA NA KATABIA KA KUTANGAZA BIASHARA YA MIILI. WEWE MDAU TUELEZE KWA NINI ULAYA NA MAREKANI KIWANGO CHA UKIMWI SI KAMA CHA AFRIKA. NADHANI LABDA NI MENTALITY YAO KUWA KUTEMBEA UCHI NI DESTURI WALA SI KUSHAWISHI. KWA BAHATI MBAYA MAMBO SI HAYO HUKO NYUMBANI, NDIO UKAONA NGONO ZEMBE HUKO NI KITU CHA KAWAIDA, BIASHARA INAYOLIPA NI KUFUNGUA GUEST HOUSE. MDAU USIUDHIKE KWA SABABU NIMETOA MAONI. KAMA NAWE UNA MITAZAMO YAKO TUNAIKARIBISHA, SIKUKUSUDIA KUKUUDHI, ILA MIMI MWENYEWE NAUDHIWA NA UKWELI KUWA UKIMWI UNATUMALIZA.
    KAMA KWENDA UCHI SI KICHOCHEO CHA UKIMWI HUKO AFRIKA, TWAMBIE FAIDA ZA KWENDA UCHI, NA SABABU ZA KWENDA UCHI KATIKA MATAIFA YA AFRIKA.
    MIMI NAKWAMBIA TABIA HIYO KWA MTAZAMO WANGU NI MOJA YA VYANZO VIKUU VYA KUENEA KWA MARADHI HAYO HUKO NYUMBANI.
    Mdau Leicester ukerewe

    ReplyDelete
  5. Ndugu wa 18,01:50pm Alioyasema mndengereko wa ukerewe ni sahihi na ametembea, wewe ndio hujatembea inaonekana uko africa kusini hao wazungu unaowaona wako uchi je wanafanya ngono kama ilivo kwa waafrica? Usione mikanda ya xxx kwene neti au hayo maisha hapo ulipo south ndio uchukulie maisha ya wazungu yako hivo,wengi wao ni waaminifu wanapokuwa kwene uhusiano.. Hii inamaana hata akivaa nusu uchi sio ati ndio utampata akiwa na mweza.

    ReplyDelete
  6. Ni kweli hamjui sababu ya wazungu kutokupata ukimwi while wanatembea uchi. Ikiwa Afrika wanakwisha. Let me say something"Mzungu akitenda dhambi anatenda kweli kila mtu anajua na akimwaamini Mungu anamwaamini kweli.Wenzetu wanajua kumaanisha na kukutafakari wanachokifanya kwa muda. Na wanaheshimu maamuzi yao. Du tukija kwetu kina sisi tunamuabudu Mungu na kujifananisha na watu wa Mungu ila chuki, zinaa, unafika zimejaa kwenye majumba ya ibada. Hata wachungaji, mashehe wanazini mbaya kwa kutumia jina la Mungu. Tutapona? Angalie baba anazini na mtoto wake wa kumzaa na hata kuzaa na binti yake. Wanaume wanatembea na wasichana wa kazi, je hamjui kuwa Mungu hadhihakiwi? Apandacho mtu ndicho atakachovuna na mavuno cku zote ni mengi kuliko mbegu. Hatuwezi kuwa pande mbili the same time. Kuna vitu viwili ambavyo havijawahi kupatana giza na nuru lazima kimoja kishinde ndo maana kuna ucku na mchana

    ReplyDelete
  7. Jamani mimi sitaki malumbano, nakubali kwamba wazungu wakiwa katika mahusiano ni waaminifu hata kama anaenda uchi, lakini mimi nipo hapo Los Angelos Marekani na takwimu zinasema ratio ya wanawake kwa wanaume ni 5:1 sema mwenyewwe wangapi wameolewa hapo? ni mmoja tu, wanne wanatafuta ni hela yako au pengine yeye ndo anakupa hela ukamfanyie kazi yake,si tu wanaenda uchi bali pia iko kitu inaitwa social network, kuna face book, jeho, wayn na nk,mingine mitandao hiyo ikiwemo ile ya wanaita cupid.com, sijui christin mingle, nk. hiyo yote ni namna ambayo wanawake wa kizungu na wanao fanana nao taja rangi zao mwenyewe wanatafuta mapenzi, je Mtanzania anajua hayo? na wala katika hizo picha hapo simwoni anaye enda nusu uchi ni mabinti tu wa NBC wamependeza kwa mavazi yao basi.
    mimi nadhani, ukimwi umekuwa "directed genetically", sina hakika, lakini kusema sisi tuna wanashinda wazungu kwa ngono hiyo siyo kweli, na unaambiwa ngono yao ni yakichafu siyo hiyo ya mtanzani.

    ReplyDelete
  8. NBC hasara tupu, party si hoja!!

    ReplyDelete
  9. Mdau, basi rudi nyumbani Bongo utusaidie jinsi ya kuepukana na ukimwi, maana wewe unayajua sana kwa kuwa unaishi huko ughaibuni!

    ReplyDelete
  10. Igeni CRDB mtakufa kifo chamende!

    ReplyDelete
  11. Mmm, kweli huyo Dada (mwenye nguo rangi nyekundu) anastahili kuwa wa mauzo, mpaka mwili anauza!!!

    ReplyDelete
  12. huyo madau anayejisifia kukaa ulaya MIAKA 13 kwanza ajiiulize yeye kaleta MAENDELEO gani africa???
    na lazima aelewe MAVAZI ni FASHION na fashion inabadilika kutokana na muda....so sidhani hivo vivazi vinachangia kwa nafasi kubwa kama yeye anavovikilia...i personally think he's just being ARROGANT if not IGNORANT.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...