Baadhi ya wakazi wa Bonde la Jangwani Jijini Dar wakiwa katika hali ya kuhamisha vitu vyao mara baada ya eneo la makazi yao kujaa maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.Inasemekana kuna watu kadhaa wamepoteza maisha kutokana na kuzidiwa na maji hayo.
Hawa nao mambo hata hayajawaendea vyema maana wao ndio wamezungungukwa na maji kila kona.
Mali zikiondolewa.
Hapa hata kwa kupita hakuna,maji yamejaa kila kona.
Jamaa akiwa amembeba mdogo wake wakati akimvusha kwenye eneo hilo lililokuwa limejaa maji yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo huku pembeni yao kukiwa na Mkokoteni uliokuwa umebeba takataka ambao ulikwama kwenye maji hayo.
Hawa jamaa wa huku kama wakitaka kufika barabarani basi ni lazima watumia mtumbwi ama ngalawa maana upande wao unamaji mengi ambayo ni ya kupiga mbizi.
Hakuna shughuli inayofanyika leo katika eneo hili la Bonde la Jangwani,maana maji ni kila kona.
Baadhi ya wakazi wa Eneo hilo la Bonde la Jangwani wakiwa ni wenye huzuni kutokana na nyumba zao kujaa maji na nyingine kuezuliwa mapaa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Poleni sana wananchi wenzetu. Je mbona maafisa wa serikali hatuwaoni kuhakiki maafa ya wananchi?
ReplyDeletejamani hameni hapo kwenye hilo bonde mbona tanzania ina ardhi kubwa tu .. kila mwaka lazima mtoke kwenye vyombo vya habari au mnangoja siku moja mvua ya kutisha iwabebe wote? jamani kinga ni bora kuliko tiba.. anyway poleni
ReplyDeleteserikali itimize wajibu wake,mbona iliweza kupitisha waya wa umeme kanisa la Kakobe?Imeshindwa nini kuwahamisha wakazi wa Jangwani?na je Kna daya za kutosha za magonjwa ya mlipoko wakati nvua zinkiendela hivi?au wanasubiri wakishakufa kama kumi hivio ndiyo tusikie mara dawa zimeaagizwa na mara MSD hawana dawa na mara hospital hakuna mahali pa kulaza wenye kipindupindu na kuhara damu.
ReplyDeleteYaani,MUNGU ATUSAIDIE NA AWAHURUMIE MASKINI WAKE.
Hakuna wa kulaumu wala siyo seriksli seriksli imejitaidi kuwaelesha lakini wao wanakuwa vigagangani asala ni zakwao wangetaka kuhama serikali ingewapa maeneo wao wanagangania hapo kwa kuwa wapo mjini siyo? shauli alao!!
ReplyDeleteNHC MPO? MNAJUA MAANA YA SLUMS? MNATAKIWA SLUMS ZOTE MSAFISHE NA KUJENGA MAKAZI YA BEI NAFUU KABISA, SIO ZA MAMILIONI! IGENI MIFANO ZA NYUMBA AFFORDABLE ZA HUKO NJE KWA WATU WENGI. HIZO ZA MILIONI ZITANUNULIWA NA MATAJIRI TU.
ReplyDeleteMbona wananchi wa TZ hawajipendi hivi?
ReplyDeleteMasikini mzee Makamba aliwaambia na kujitahidi sana lakini ukimgusa mwananchi kuhama hapo bondeni basi inageuzwa siasa.
Serikali ichukue hatua ya kuwahamisha kwa nguvu kwa usalama wao wenyewe hao wakazi.
Serikali haina maamuzi, na tatizo inawasilikiza sana wachonga mdomo, sijui Ananilea nkya, sijui kibanda, sijui chasdema, basi siasa na wabajidai haki za wanadamu, wakifa na mafuriko watatoka kifua mbele serikali haijali, wakihamishwa watapiga ulimi oh, serikali inawasumbua wananchi walitakiwa iwajengee sehemu stahili kwanza etc
ReplyDeleteHawa watu si waliambiwa wahame miaka mingi na walielezwa hatari za kujenga bondeni?
ReplyDeleteI cann't believe my own eyes, hizi nyumba nikweli ziko Tz-Dar au kijijini kibosho? Na bado wakubwa mnadai posho. Embu leteni maendeleo acheni utani. Mnaweza mkaweka ujenzi imara hapo
ReplyDeleteHapo hakuna hata nyumba moja iliyojengwa kwenye kiwanja halali na chenye hati ya kumiliki kiwanja hicho. Lakini bado kuna watu wanalaumu serikali. Hawa watu hujenga vibanda vyao wakati wa kiangazi na kusahau kwamba kuna siku msimu wa mvua utawadia.
ReplyDeleteMimi ningekuwa ndo mkuu wa nchi, eneo la Jangwani hili ningeamuru pajengwa shopping center (mall) kubwa sana pande zote mbili za eneo, ili kuzuia eneo lisiwe wazi na watu kama hawa wasio na masikio kujenga katika eneo hilo, kwasababu hilo ninalosema linawezekana kabisa badala ya kuacha eneo wazi namna hii na watu kushawishika kulitumia na tunaanza kuwalaumu wanapoathilika namna hii.
ReplyDeleteTHESE PEOPLE ARE IGNORANT IF NOT STUPID I REMEMBER DURING MAKAMBA'S TERM THEY WERE MOVED AND GIVEN LAND BUT THEY REFUSED DUE TO STUPID UNRELATED REASONS. I REALLY DON'T FEEL SORRY FOR THEM I JUST FEEL SAD.
ReplyDeletekama kawa, watu wengine wanaona hili ni kosa la serikali.
ReplyDeleteMwishowe hata `ukijichafua' utailaumu serikali kwa kutokuwekea choo karibu .
Serikali iwe na maamuzi mazito,haiwezekani watu wajenge maeneo yasiyotakiwa kujengwa kama haya inawaacha lakini wakipata shida serikali hiyohiyo inatumia kodi zetu kuweka mambo sawa ni lini watu watafunguka nakufanya mambo endelevu?
ReplyDeleteUkaidi wa kutohama Mabondeni unatokana na kutojiamini na kufikiri kuwa kukaa Mjini au karibu na Mjini ndio kupata uhakika wa maisha,,,duhhh hizo ni fikra dhaifu ,,,kumbe ,maisha ni popote!
ReplyDeleteWandugu muwe mnajiaminia kimaisha kukaa Mjini sio msahafu wa kufanikisha maisha!, nendeni Chanika Kijijini, Mbagala, Vikindu, na Kongowe mtaishi pia badala ya kushirikiana maisha na vyura huku mkijiita mpo mjini!, ebo!
ReplyDeletejaman hata tukiwalaumu wataenda kukaa wapi?????? msijiropokee midomo mipana kama mabawa ya ndege,hizo posho wanazodai hawa wabunge zingejenga nyumba za bei nafuu ili wananchi waweze kuishi,tz ni nchi nayo??? hakuna cha maana wakubwa ndio hao wanajinyakulia chao mapema sie tunatoa mimacho, kwa ivyo tusiwalaumu jaman plzzzzzzzz
ReplyDeleteHayo ndo matunda ya miaka 50 ya uhuru Tanzania.
ReplyDeleteYa nini maisha ya Kenge nusu nchi kavu nusu ndani ya maji,,,maisha sio kujitweza kwa kukaa mitaroni Jangwani kwa vile ni ndani ya jiji la DariSalama,,,hamieni nchi kavu kama Vikumburu,Mbande,Mwanadilatu,Kibugumo,Gezaulole,Vijibweni,Kisemvule,Mwanambaya,Mwarusembe,Kimanzichana,Buyuni Bagamoyo, Kibaha Picha ya Ndege na Chalinze kwenye makao mapya!
ReplyDeletehao waliojenga hapo wengi wao wanazo nyumba zingine pembeni hapo wanajifanya ndo wanaishi, wengine kipindi cha mvua ndo wanahamia hapo ili waonekane na kulipwa , SERIKALI IUNDE TUME YA UCHUNGUZI .. kama kawaida yake tume za uchunguzi kibao.... serikali haina meno , ipo ipo tu
ReplyDeletealokuambieni hao hawana pa kuishi ni nani ? wananyumba hao kuna moja hapo ni baba mwenyenyumba moja ipo tabata tena nzuri kweli nyumba ya kama laki 3 kwa mwezi... hao wanaitania serikali.. angekuwa baba wa taifa yu hai upumbavu kama huu usingekuwepo
ReplyDeleteAhhh unajua wengine hawaamini kama wapo mjini Dare salaamu hadi waone Klabu ya Yanga, pale Jangwani ipo ngámbo ile inaonekana kule upande wa pili wa bonde!
ReplyDeleteMdau Mtoa maoni wa 18 hapo juu unaesema,,, ''Hayo ndo matunda ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania''
ReplyDeleteHuwezi kusema ahhh jamani Mwenyezi Mungu amenijaalia mimi kuwa mtu wa dhiki maishani, atakaesema hivyo sio bure atakuwa ni taahira!
Wala sio hivyo huu ni ujinga binafsi wala hakuna uhusiano wowote wa ujinga huu na miaka 50 uhuru wa nchi ya Tanzania!
Wajameni wakazi wa Jangwani Mdau wa 19 hapo juu amewatajia maeneo mengine salama kwa makazi yenu ambayo nayo yamo ndani ya nchi yetu ya neema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati JK akiwa ndio Raisi wenu na sio nchi nyingine,,,Nani aliwadanganya kuwa Jangwani pekee ndio Tanzania?, nani aliwaambia kuwa Vikumburu sio Tanzania?, nani aliwaambia kwamba Kibugumo sio Tanzania?, nani aliwaambia kuwa Gezaulole sio Tanzania?, nani aliwaambia Mbande sio Tanzania?,,,nendeni huko mkaishi mkale vyakula na kunywa vinywaji kama mko Paradiso!
ReplyDeletehata mie nakumbuka DC BALAMA aliwaambia wahame mdogo mdogo pale hii serikali nayo tuitue kuitupia lawama always wabongo wabishi sasa apo mbaka balaa hilo ndo tunaona tatizo pole yao lakini
ReplyDeleteoh ndugu zangu, hii hali ni ngumu kidogo niionavyo mimi. kama mtu anachagua kuishi ndani ya bahari wewe inakuhusu nini kama sio uchokozi wa kiswahili mtupu?? mtu anaamua kuishi kariakoo wewe unakaa kijichi? safi!! waacheni kama walivyo, marufuku mtu kwenda kuwabughudi hasa kipindi hiki cha mafunzo muhimu kwao, la sivyo hawatajifunza hawa,
ReplyDeletemnavyowabugudhi ndio manawaharibu zaidi, leave them alone and mind your own business only. mtu asiwaguse iko siku watapata akili kama ulivyo kuwa nazo wewe. mimi niliishi hapo kwa mika kumi; siku moja nikasema hapa basi!! na leo mimi naishi OYSTER-BAY. Dont Disturb Them .
Waachweni Kabisa Mkafanye Kazi Zenu; kama huna kazia pumzika na mwenzio.
Please help those who need your help! Tanzanians are very generous and kind people! God bless u all!
ReplyDeleteKinachowaweka na kuwaponza WANA JANGWANI hao jamaa KWA GHARAMA KUBWA NA HATARI YA MAAFA KUELEKEA KIFO, ni ile BURE GHALI (UCHUMI RAHISI NA UJANJA UJANJA, UMJINI MJINI) unakuta mtu kiwanja anauziwa TSHS. 30,000/=bila vipimo na dalali fiksi, anajenga nyumba kwa TSHS, 450,000/= tu ili kukwepa KODI YA NYUMBA ya TSHS. 250,000/= KWA MWAKA HUKO SINZA NA TABATA na huku akikwepa nauli ya basi ya kuja mjini(shs.300) na kurudi(shs.300) ya kila siku ya TSHS. 600/= tu!
ReplyDeletePana watu ambao sio majasiri wa maisha!,,,hawaamini kuwa bila kukaa Magomeni ,Jangwani, Kariakoo au Karibu na Soko la Kariakoo,Feri /Kivukoni,Buguruni,Ilala au Mburahati MAISHA HAKUNA AU HAYAWEZEKANI KABISA!
ReplyDeleteMi Naomba Rais awakabidhi TANAPA ilo eneo la Jangwani wapande miti ya kutosha , Majambazi wakienda kuijificha itafanyika msako watadakwa then arthi itaendelea kuwa na mti kuliko hao wanaosumbua watu sasa.Jamani kwani Dar pekee ndio mji mbona wengine tunaishi mikoani tuna maisha mazuri tuu.Rudini ma kwenu nyie mliovamia huko.
ReplyDeletePoleni ambao hamkua mabondeni na maji yaliwakuta.
Hata wakati wa NUHU aliwaambia watu lakini hawakusikia mpaka walipoona maji yamefika shingoni ndio walimkumbuka.