Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama akitoa hotuba yake kwa wanahabari wakati wa mkutano wa waandishi wa habari na wadau wa habari uliofanyika Umoja Hostel.
Mweka hazina wa klabu ya waandishi wa habari Mkoani Kilimanjaro, Jane Mhalila akitoa na shukurani kwa mgeni rasmi .
Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro Bi Hilda Kileo akitoa maneno machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika mkutano huo.
Makamu mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro (MECKI) Rodrick Makundi akizungumza wakati wa mkutano wa wanahabari na wadau wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Umoja Hostel.
Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima na Globu ya Jamii,Dixon Busagaga akitunukiwa cheti na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kutokana na kuandika habari za Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro.
Wanachama wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro (MECKI) wakifuatilia majadiliano katika mkutano wao na wadau wa habari mkoa wa Kilimanjaro.
Wadau wa wanahabari.
Viongozi wa klabu ya waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama.Picha na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...