Siku ya Jumapili, tarehe 4 Disemba, 2011 katika hafla ya uzinduzi wa Royal Billy's Lodge ambayo ipo nyuma ya Kanisa KKKT Tangi-Bovu palifanyika pia harambee kwa ajili ya kuchangia shughuli ya kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Mwananyamala pamoja na kutoa misaada ya hali na mali kwa wagonjwa katika wodi ya wazazi na wodi ya watoto hospitalini hapo. Kabla ya kuanza kwa hafla ya uzinduzi wa lodge hiyo na harambee, wakimbiaji wa mbio za pole pole (jogging) kutoka vilabu vya Biafra, Namanga, Kunduchi, Mbezi Beach, Temeke na wenyeji Tangi Bovu walikimbia mbio hizo kutoka Tangi Bovu kupitia Kawe na kurudi Tangi Bovu.
Baada ya mbio za pole pole kumalizika wakimbiaji waliendelea kufanya mazoezi kwa mtindo wa aerobics na kama kawaida ili aerobics inoge basi unapigwa muziki na kaka Michael J almaarufu Mopao anaongoza mazoezi hayo. Kwa mapicha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...