Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polykarp Kardinal Pengo akiwa katika maandamano ya kuingia kanisani tayari kwa ibada ya Sikukuu ya Krismas iliyofanyika leo katika Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Kanisa Katoliki wakiwa katika maandamano ya kuingia kanisani tayari kwa ibada ya Sikukuu ya Krismas iliyofanyika leo katika Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akisalimiana na mmoja wa waumini wa kanisa hilo mara baada ya ibada ya sikukuu ya Krismas iliyofanyika leo katika Kanisa la Azania Front Dar es Salaam .
Kikundi cha Kwaya ya Kanisa la Mtakatifu Petro kikiimba nyimbo za kumsifu Mungu wakati wa ibada ya mkesha wa Krismas usiku wa kuamkia leo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akiwa amembeba mtoto, Daniel Mwandolela mara baada ya ibada ya sikukuu ya Krismas iliyofanyika leo katika Kanisa la Azania Front Dar es Salaam
Baadhi ya Waumini waliohudhuria ibada ya Krismas wakiwa kwenye moja ya misa za ibada hiyo leo.Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. hizi dini ukifatilia kwa makini utaona kama wameshushiwa watu weusi

    maana ukiangalia asilimia kubwa wanaofata hizi dini ki ukweli utaona kuwa ni watu weusi kuanzia amerika mpaka afrika

    huku ughaibuni wanachukulia siku za skukuu kama christmas ni kama siku za kufurahia na kuenjoy holiday na sio kama wanakuwa na imani za kikristo

    asilimia kubwa huku ughaibuni hawana dini na makanisa yao utayaona wameyafanya kama sehemu za makumbusho na sio majumba ya ibada maana hakuna anaetumia kufanyia ibada

    na hata ukiwauliza wanasema kuwa wanasheherekea christmas sio kana kwamba ni wakristo isipokuwa wanapenda kujifurahisha kwa siku hiyo na kutokana ni holiday mapunziko ya kazi

    lakini kwa upande wa watu weusi hiyo siku inakuwa ni siku muhimu sana katika kufanya mengi ya ibada ukiangalia kule amerika makanisa mengi ni ya watu weusi na hata afrika makanisa ni mengi sana

    na wengi wao wana imani za kweli sasa hapo ndipo ninapofahamu kuwa dini hizi ni kwajili ya watu weusi na watu wa mataifa yenye shida kama vile south america.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...