Wazanzibari kutoka sehemu mbalimbali za Skandinavia walikutana jana kusherehekea kumbukumbu ya siku ya Uhuru wa Zanzibar wa tarehe 10 Disemba 1963. Sherehe hizo zilifanyika katika mgahawa maarufu mjini Copenhagen ujulikanao kama Ankara Restaurant. Mbali ya wazawa wa Zanzibar, walihudhuria pia wageni mbalimbali kutoka Uingereza, Poland, Uturuki na sehemu nyingine duniani kuunga mkono hafla hiyo.
Katika maadhimisho hayo, mwandishi na mtafiti wa siasa za Tanzania Ludovick Mwijage alipata nafasi ya kuhutubia hadhara hiyo kwa kuwaunga mkono Wazanzibari juu ya uamuzi wao wa kusherehekea siku hii adhimu. Pamoja na mambo mengine, Mwijage amewashajiisha Wazanzibari kuendelea kuikumbuka siku hii kwani ni siku muhimu sana katika historia ya visiwa vya Zanzibar.
Kamati ya maandalizi ya sherehe za kumbukumbu ya siku ya Uhuru wa Zanzibar inapenda kuwashukuru wote waliohudhuria katika hafla hiyo pamoja na wale waliochangia kwa hali na/au mali kufanikisha siku hii.
Kamati maalum,
11 Disemba 2011
Copenhagen
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...