Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Francis Miti, (mwenye suti) akikagua gwaride rasmi la Maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru kwenye uwanja wa Jamhuri wa Mjini Morogoro.
Gwaride kupita mbele ya jukwaa kuu kutoa heshima kwa mwendo wa haraka.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Mgeni Baruani, akisoma hotuba ya mafanikio ya miaka 50 kwa Mkoa wa Morogoro, siku ya kilele cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru, Desemba 9, mwaka huu.
Mbwa wa Polisi akikabiliana na mwizi, ikiwa ni sehemu ya maonesho ya Jeshi hilo katika Maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru.
Vijana wa Halaiki wakionesha maumbo ya herufi ya miaka 50 ya Uhuru, kwenye uwanja wa Jamhuri wa Mjini Morogoro.
Nakumbuka wimbo wa mchakamchaka nikiwa shule ya msingi enzi zileee:
ReplyDelete"Mafunzo ya mgambo sio mateso, bali ni mazoezi ya viungo, usibabaikeeeee!"
Wadau mnaikumbuka hii?