Wazanzibari kutoka sehemu mbalimbali za Skandinavia walikutana jana kusherehekea kumbukumbu ya siku ya Uhuru wa Zanzibar wa tarehe 10 Disemba 1963. Sherehe hizo zilifanyika katika mgahawa maarufu mjini Copenhagen ujulikanao kama Ankara Restaurant. Mbali ya wazawa wa Zanzibar, walihudhuria pia wageni mbalimbali kutoka Uingereza, Poland, Uturuki na sehemu nyingine duniani kuunga mkono hafla hiyo.

Katika maadhimisho hayo, mwandishi na mtafiti wa siasa za Tanzania Ludovick Mwijage alipata nafasi ya kuhutubia hadhara hiyo kwa kuwaunga mkono Wazanzibari juu ya uamuzi wao wa kusherehekea siku hii adhimu. Pamoja na mambo mengine, Mwijage amewashajiisha Wazanzibari kuendelea kuikumbuka siku hii kwani ni siku muhimu sana katika historia ya visiwa vya Zanzibar.

Kamati ya maandalizi ya sherehe za kumbukumbu ya siku ya Uhuru wa Zanzibar inapenda kuwashukuru wote waliohudhuria katika hafla hiyo pamoja na wale waliochangia kwa hali na/au mali kufanikisha siku hii.

Kamati maalum,
11 Disemba 2011
Copenhagen

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Mara ya kwanza kusikia Wazanzibari wakisheherekea Uhuru wa Zanzibar. Zaidi ya kusomeshwa skuli kuhusu siku hii haina umuhimu sana kwa Wazanzibari walio wengi. Kuna kundi la Wazanzibari ambao wanaitumia siku hii kwa kutafutia ulaji!!

    ReplyDelete
  2. hakuna siku kama hiyo kwenye kalenda za huku kwetu kuingilia muungano

    ReplyDelete
  3. anony wa kwanza na anony wa pili, hivi kwanini mnapingana na historia? kama nyie mnaona aibu kusherehekea uhuru wa tanganyika, shauri yenu.

    ReplyDelete
  4. It makes no sense honestly, 12th January is the day that the Zanzibar islands became fully independent.However, we can remember December in our history as the day that the Colonial rule handed over Zanzibar islands to the minority and whom the head was the Sultan !!!How can you call Decemeber 10th 1963 when half of the islands did not have equal opportunities..The revolution would remain to be the date where by Zanzibar gained its freedom for its people.However, I completely understand, the nature of the unecessary killing that took place was to the extreme.The only place prior to the revolution that had access to water, health and municipality was only stone town and its vicinity.

    ReplyDelete
  5. teh teh teh sijawahi sikia teh teh

    ReplyDelete
  6. KWANZA HATUWATAKI KABISA MASHOGA WATUPU, JITOWENI BASI KATIKA MUUNGANO KAMA MNAWEZA? NDIO MAANA HAMKUONEKANA KWENYE UHURU DAT ETI MNA UHURU WENU , MIDEBWEDO WATUPU

    ReplyDelete
  7. mdau wa pili, hujakosea sana kwa ufupi siku hii ipo ila haitambuliwi au tuseme haitajwi kwani ilitokea kabla ya mapinduzi ya 1964. Kihistoria zanzibar ilipata uhuru kama tanganyika, lakini muda mfupi tu baada ya uhuru pakatokea mapinduzi yaliongozwa na karume.

    Nadhani nimekusaidia kukupa muangaza kidogo

    ReplyDelete
  8. mdau wa kwanza, skuli zanzibar hatukufundishwa na wala sasa wanafunzi hawafundishwi juu ya uhuru wa zanzibar. Tumefundishwa kuwa zanzibar kulifanyika mapinduzi (hatukupata uhuru) tarehe 12 January 1964.

    ReplyDelete
  9. Historia yetu tunaijua wenyetu Wa Zanzibari 10 December 1963 ndio siku tuliyopewa uhuru kizazi chote cha Zanzibar wamefundishwa historia hiyo na Wazazi wao na tutazidi kukijulisha kizazi chetu kijacho...wacheni choyo na jeoulus hizo za Kitanganyika....mbona Wazanzibari hawajasema kitu wakati mnasherehekea uhuru wenu wa Tanganyika...baada ya uhuru Zanzibar kiongozi Jemshid alizaliwa Zanzibar na waziri mkuu wetu wa mwanzo Mohamed Shamte alikuwa ni mzanzibari na vikosi vya ulinzi vyote walikuwa ni wazanzibari...Habari ndio hiyo!!!
    ndio baadae kukafanyika coup Zanzibar kuuharibu uhuru wetu...Mapinduzi ni njama za uwongo tu na Wazanzibari wote wanajua njama gani zilitumika kuliuwa taifa la Zanzibar.

    ReplyDelete
  10. Mnaposema Uhuru wa Zanzibar sasa huu ni utenganishi!

    Tumesha adhimisha Uhuru wa Tanzania inatosha haya Maadhimisho ya Uhuru wa Zanzibar yanatoka wapi wakati tupo ktk Muungano?...Wazanzibar bwana khaaa wakorofi wakorofi, watenganishi watenganishi balaa!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...