Na Global Publishers

Mahakama Kuu Dar es Salaam, imeamuru Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila (pichani), kuendelea na wadhifa wake wa ubunge hadi hapo kesi yake ya msingi itakaposikilizwa.
Hivi karibuni, Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi, ilimfukuza Kafulila uanachama, uamuzi ambao unamuondolea sifa ya kuwa mbunge.
Hata hivyo, kutokana na uamuzi wa Mahakama Kuu leo, Kafulila ataendelea kushikilia nafasi yake ya ubunge mpaka hapo kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa hukumu.
Uamuzi huo wa mahakama, umefuatia kesi iliyofunguliwa na Kafulila, kupinga uamuzi wa Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi wa kumvua uanachama na kumuondolea sifa ya kuendelea kuwa mbunge.
Kafulila alipozungumza na mwandishi wetu alisema kuwa Mahakama Kuu itakaa Februari mwakani na kupanga kuanza kusikiliza kesi hiyo.
“Namshukuru Mungu, siku zote Mungu yupo pamoja na wanyonge. Bado nasimamia ukweli kwamba kikao cha Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi kilichoamua, kilikiuka sheria na taratibu. Hata hivyo, suala hili lipo mahakamani, tuache mahakama itaamua,” alisema Kafulila.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, amepongeza uamuzi wa mahakama na kuueleza kwamba ni mpango wa Mungu kumtetea mnyonge.
Zitto, aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Kijamii, Facebook leo saa 9:40 alasiri: “Kafulila kuendelea na ubunge. Mahakama Kuu imetoa amri muda mfupi uliopita. Ataendelea kuwa mbunge mpaka hapo kesi ya msingi itakapokwisha. Mungu yupo pamoja na wanyonge siku zote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Huyu Bwana atakuwa ameshauriwa na Chama chake afungue kesi mahakamani. Naona mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea kati yake na wazee wa chama chake walikuwa tayari kumsamehe na kumrudisha lakini ili chama kisionekane hakina msimamo wamemshauri hivyo wakijua kuwa atashinda kesi na hivyo kuwafunga watu midomo. Kumbuka Mbatia alikuwa tayari kumuombea msamaha kwa wajumbe wa ule mkutano wakagoma. Naona walitafakari athari za kumpoteza huyu bwana ndio wakaja na hii strategy. Huo ndio mchezo wa siasa.

    ReplyDelete
  2. Hongera Mheshimiwa! Swali kubwa nalojiuliza ni kwa nini katiba yetu inaruhusu Mbunge aliechaguliwa na wananchi kupoteza kiti chake baada ya kufukuzwa uanachama.

    Huu ni wakati muafaka wa kubadili kipengele hiki kwenye katiba. Na imefikia muda wa wabunge kuruhusiwa ku switch vyama bila kupoteza viti vyao. Pia imefikia wakati wa kuruhusu wagombea binafsi.

    Glisio

    ReplyDelete
  3. Mwacheni DAVID KAFULILA (JEMBE) na yeye ale zake!

    Haya mambo gani jamani?,,,

    Hamuoni mchango wake kisiasa?
    Hivi ndio tunajenga au tunabomoa?

    Mnaacha kuwaajibisha Watu wasiokuwa na faida mnamwajibisha Dogo Davi kama mnavyoona kijana mdogo anvyongára pichani na ndio kwanza tu amemaliza Chuo Kikuu!

    Khaaa, acheni kumuharibia hatma yake ya maisha dogo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...