Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Afisa wa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nchi za nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Mindi Kasiga wakati wa mahojiano maalum yaliyofanyika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Kazi kubwa inayoikabili Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Tanzania ni kuhakikisha ile sera ya Mambo ya nje ya kuelekea kwenye uchumi inaimarishwa zaidi na kutekelezwa ipasavyo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameeleza hayo katika Kipindi Maalum cha Mahojiano wakati akizungumza na Afisa wa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nchi za nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Mindi Kasiga hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Balozi Seif alisema utekelezaji wa sera za Diplomasia ya uchumi hivi sasa umekuja kufuatia kumalizika kwa ukombozi wa Baadhi ya Nchi za Afrika mwishoni mwa miaka ya 80.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambaye ni mwanadiplomasia mkongwe amesema Tanzania ililazimika kupunguza baadhi ya Ofisi zake za Kibalozi Nje ya nchi kwenye miaka ya 80 kutokana na kuwa na uchumi Duni.

“ Ulikuwa ni uamuzi mgumu wa kufunga Baadhi ya Ofisi zetu Nje ya Nchi lakini tulilazimika kufanya hivyo kwa vile ilikuwa kuendesha Ofisi hizo ni gharama na inahitajika uwezo zaidi ”. Alisisitiza Balozi Seif.

Alisisitiza haja ya watedaji wa Ofisi za Kibalozi za Tanzania kujikita zaidi katika Taaluma ya kufanya kazi zaidi ya moja kwa lengo la kubana matumizi yasiyo ya lazima.

Akijibu suala la Mchakato wa Katiba mpya ya Tanzania Balozi Seif alitahadharisha kwamba ni vyema jambo hili wakaachiliwa wananchi wenyewe kuamua bila ya kuingiliwa na Vyama vya Siasa au wimbi la Taasisi na Mataifa ya nje ya Nchi.

“ Wapo baadhi ya watu wana wasi wasi kwamba upo mkono wa nje unaotumiwa kuwachanganya wananchi katika suala hili ya Katiba ingawa mimi sina ushahidi wa hilo ”. Alisema Balozi Seif.Hata hivyo aliwaomba wana Diplomasia wa Kigeni kuendelea kuheshimu Sheria za Nchi kwa vile taratibu za kuwepo kwao haziruhusu kuingilia mambo ya ndani ya Nchi.

Balozi Seif alikumbusha kwamba kazi ya Balozi ni kuimarisha uhusiano mwema kati ya nchi yake na mahali anapopawakilisha.

Hadi sasa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ina Ofisi za Kibalozi Nje ya Nchi zipatazo 32 kutoka 25.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Maalim Seif yeye je? Mbona tunamuona tuu huyu jamaa kila siku?

    ReplyDelete
  2. Mindi must be a really fast typist to be able to take notes on her netbook while conducting the interview! Congrats to her!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...