MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF AKIZUNGUMZA NA BALOZI WA INDIA NCHINI TANZANIA BWANA K.V. BHAGIRATH OFISINI KWAKE VUGA MJINI ZANZIBAR.BALOZI BHAGIRATH ALIFIKA KWA BALOZI SEIF KUAGA BAADA YA KUMALIZA MUDA WAKE WA UTUMISHI NCHINI TANZANIA.
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AKIMKABIDHI BALOZI WA INDIA NCHINI TANZANIA BWANA BHAGIRATH ZAWADI YA KASHA PAMOJA NA VIUNGO KAMA ISHARA YA KUMBU KUMBU YA KUWEPO KWAKE NCHINI.
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AKIBADILISHANA MAWAZO NA BALOZI WA INDIA NCHINI TANZANIA BWANA BHAGIRATH BAADA YA KUMALIZA MAZUNGUMZO YAO.

India inakusudia kuongeza nafasi za masomo ya elimu ya juu kwa Wanafunzi wa Tanzania katika kipindi kijacho cha mwaka 2012 katika fani ya kilimo na Ufundi.

Balozi wa India Nchini Tanzania anayemaliza muda wake Bw. Bhagirath ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi hapo Afisini kwake Vuga Mjini Zanzibar .

Bw. Bhagirath alisema ongezeko hilo la fursa za masomo litakwenda sambamba na mpango wa utoaji wa mafunzo ya amali ambao uko katika hatua za matayarisho.

Alisema ushirikiano mwema uliopo kati ya India na Tanzania ikiwemo Zanzibar kwa ujumla umewezesha kunyanyua kiwango cha Taaluma kwa Vijawa waliowengi Nchini Tanzania.

Balozi Bhagirath alifahamisha kwamba katika uendelezaji wa uhusiano huo India imeamua kugharamia mafunzo ya Teknolojia ya Habari

{Teknohama } yatakayofanyika hapa Tanzania.

“ Walimu wa Mafunzo hayo yatakayochukuwa takriban wanafunzi 100 wa Tanzania Bara na Zanzibar wanatoka India wakati mfuko wa gharama tayari umeshatengwa ”. Alisisitiza Balozi Bhagirath.

Balozi wa India Nchini Tanzania amepongeza kutokana na ushirikiano wa karibu aliyoupata wakati alipokuwa akitekeleza majukumu yake aliyopangiwa hapa Nchini.

Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameelezea kuridhika na Utumishi wa Balozi Bhagirath uliopelekea kusaidia vyema Maendeleo ya Tanzania.

Balozi Seif alisema Mpango wa India wa kufikiria kuanzisha Mafunzo ya Amali unaweza kuwa mkombozi kwa Vijana wengi wanaomaliza masomo yao hasa ya Darasa la 12 { Form 1V }.

“ Tumekuwa na kundi kubwa la Vijana wanaomaliza masomo yao ya Form 1V likiwa halina muelekeo. Sasa Mafunzo hayo yatapunguza wimbi la Vijana hao kuzurura mitaani bure ”. Alisisitiza Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alimshauri Balozi Bhagirath kuangalia Nchi yake uwezekano wa kutoa mafunzo kwa wakulima kuhusu matumizi ya mazuri ya maji ambayo Zanzibar imebarikiwa kuwa na rasilmali hiyo muhimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...