Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati alipokutana na Watanzania waishio nchini Burundi jana Novemba 30. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dkt. James Mwasi Nzagi (kulia) ni Mwenyekiti wa Kinamama wa Jumuiya ya Kinamama waishio Burundi, Siwajibu Hamis (wa pili kulia) ni Mwenyekiti wa Vijana wa Jumuiya hiyo, Mutalemwa Julian.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwaaga baadhi ya Watanzania waishio Burundi baada ya kumaliza mazungumzo alipokutana nao Bujumbura Burundi jana Novemba 30 na kuzungumzia mambo mbalimbali yanayoendelea katika Taifa la Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Watanzania waishio Bujumbura Burundi, baada ya kumaliza mazungumzo baina yao yaliyofanyika jana Novemba 30 na kujadili mambo mbalimbali yanaoendelea katika Taifa la Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Makamu wa Rais wa Burundi, Therence Sinunguruza, wakati akiwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Burundi tayari kwa kuondoka nchini humo kurejea Tanzania baada ya kumaliza shughuli za Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliomalizika Bunjumbura Burundi juzi Novemba 29. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. mmmaaaahhhh watanzania wa burundi kanga ni mavazi ya kawaida ya warudi wakikutana na kiongozi wa nchi au walikuwa kwenye msiba ambao hatuujui ? mmmm kweli ukila na kipofu na wewe jifanye kipofu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...