Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mmoja kati ya wananchi waliohifadhiwa katika Kambi ya Shule ya Sekondari ya Azania, waliookolewa katika maeneo yaliyojaa maji kutokana na mvua zilizonyesha jijini Dar es Salaam kuanzia majuzi, wakati Makamu alipofika katika Kambi hiyo leo Desemba 23, kwa ajili ya kuwapa pole waathirika hao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Bi. Monica Luis, Mkazi wa Jangwani aliyeathirika na mafuriko ya Mvua kubwa iliyonyesha jijini kuanzia majuzi, wakati makamu alipotembelea katika Kambi ya Shule ya Sekondari Azania jijini Dar es Salaam leo Desemba 23, kwa ajili ya kuwapa pole waathirika wa mafuriko hayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya wananchi waliohifadhiwa katika Klabu ya timu ya Yanga ya Jijini Dar es Salaam, wakati alipowatembelea kuwapa pole wananchi hao walioathirika na mafuriko ya Mvua kubwa zilizonyesha jijini kuanzia majuzi. Makamu alifanya ziara hiyo ya kutembelea baadhi ya kambi za waathirika leo Desemba 23.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo ya jinsi maji yalivyokuwa yamejaa wakati wa mvua kubwa iliyosababisha mafuriko, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick (kulia), wakati alipotembelea kuwapa pole wananchi waliokuwa wamehifhadhiwa katika Klabu ya Yanga, iliyopo Jangwani leo Desemba 23. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.






Enhee, mmeona jinsi YANGA ilivyokuwa na jukumu la Chama na Serikali?
ReplyDeleteNajua mtabisha mtasema ohhh, kwa vile mafuriko yametokea huko huko miferejini kwao Jangwani ndio maana wamebeba jukumu la kuwapa hifadhi waathirika, lakini yangetokea Msimbazi na sisi tungebeba jukumu!
Yanga oyeee,
Lakini Habari ndio hiyo!
Hahh Mdau wa mwanzo Yanga ndio Chama na Serikali!.
ReplyDeleteYanga ndio mzazi, mtoto yeyote yakimfika ya kumfika (KAMA MAFURIKO) hata kama atakuwa mkubwa lazima atakimbia na kuangukia miguuni mwa mzazi!
Yanga kamili......mwanzo mwisho!
Wajameni shida haina adabu!,
ReplyDeleteMfano mtu ni shabiki wa Simba wa kufa na kupona, halafu ikatokea hali kama hii maafa ya mafuriko na uharibikaji wa makazi yetu, na ikabidi baada ya Kambi ya Shule ya Mchikichini kujaa, Serikali za Mitaa eneo la Jangwani wakupangie makazi ya muda ndani ya kituo cha klabu ya Yanga kwa makazi ya muda je utakaa?
Hahaha Mdau wa tatu acha masihara !
ReplyDeleteMimi ni SIMBA DAMU hata kwa viboko siwezi lala ndani ya jengo la Yanga ingawa ni kweli nyumba yangu imejaa maji!.
Nitakachofanya kwa vile mimi ni Muislamu nitaomba hifadhi ktk Msikiti wa OMAR IBN KHATTAB ulio jirani na unatazamana na Klabu ya Yanga!
Lohh jengo la Yanga sikai ngó mimi ni Simba na Mlokole.
ReplyDeleteNitaenda kuomba hifadhi Kanisa la Mito ya Baraka kwa Mchungaji Mwingira Jangwani nitapata Mapumziko ya amani!
Mimi jamani ushabiki wangu mbaya Yanga inanichefua sana!
ReplyDeleteMaana hata nikipita Yanga au hata nikiona rangi ya njano na kijani damu inanicheza!
Sasa sijui nitakaa au kulala vipi humo wakinipangia?