Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini kwa tiketi ya CCM Mhe. Aeshi Hillal (kulia) akiwa na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima alipotembelea banda la Rukwa kwenye Maonesho ya Miaka 50 ya Uhuru katika viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam. Hapo wakitoa huduma kwa wateja.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa akimsainisha kitabu cha wageni mmoja wa wageni waliofika kupata huduma katika banda la Rukwa. Anayeshuhudia ni Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Mhe. Aeshi Hillal. Banda la Rukwa limekuwa likipata wageni wengi kutoka Mikoa na maeneo mbalimbali wakitaka kujifunza mambo mbalimbali kutoka katika Mkoa huo.

Mhe. Aeshi alitembelea vibanda vyote Sita (6) vya Mkoa wa Rukwa katika Maonesho hayo na kufarijika kwa yote aliyoyaona. Mhe. Aeshi kabla ya kutembelea banda la Rukwa alikuwa ziarani nchini Burundi ambapo ziara yake hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kwani aliapata fursa ya kukutana na baadhi ya Viongozi wa Serikali nchini Burundi akiwepo Meya wa Jiji la Bujumbura pamoja na Wafanyabiashara wakubwa na kuwaeleza juu Fursa zinazopatikana Mkoani Rukwa. Alisema kuwa wote walifarijika na kuonyesha nia ya kutembea na kuwekeza Rukwa. "Nimechukua contact zao na nitakachokifanya ni kuzipeleka kwa Mkuu wa Mkoa ili kuwapa mualiko rasmi wadau hao waweze kuja kutembea Rukwa na kujionea fursa zilizopo" alisema Mhe. Aeshi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...