Na Lydia Churi- MAELEZO,Bagamoyo –PWANI.

WATANZANIA wametakiwa kutowapa nafasi watu wanaopotosha mchakato wa kupata Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bali washiriki mchakato huo kwa amani na utulivu.

Akizungumza na Vijana wa Chama cha Mapinduzi wa wilaya ya Bagamoyo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi amesem kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ana nia njema ya kuhakikisha kuwa watanzania wanapata katiba mpya baada ya kutimiza miaka 50 ya uhuru wa nchi yao.

Amesema taarifa zinazotolewa na serikali juu ya kuanza kwa mchakato wa katiba mpya ni za dhati na serikali ina nia njema katika hili hivyo wananchi hawana budi kuwapuuza wale wanaopotosha taarifa hizo.

Waziri Nchimbi amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Mnara wa kumbukumbu ya mkutano wa kwanza wa TANU kitaifa uliofanywa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika mwaka 1954.

Amewaasa vijana kuwa Mnara huo usibaki kuwa kumbukumbu tu bali wayafanyie kazi yote yaliyofanywa na waliowatangulia.

Amewataka vijana kudumisha amani na utulivu uliopo nchini kwa faida ya vizazi vijavyo na kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara kwa kutathmini kazi zilizofanywa na waanzilishi ili waweze kuwarithisha watoto wao baadaye.

Naye Katibu mkuu wa UVCCM Taifa, Martin Shigella akizungumza wakati wa uzinduzi huo amewataka vijana wa CCM kuwa na moyo wa kujitolea ili waweze kuliletea taifa maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...