MBUNGE wa Wawi, Hamad Rashid Mohammed (CUF) ameigomea Kamati ya Nidhamu na Maadili ya chama hicho kumhoji na kumjadili kuhusu tuhuma zinazomkabili za kukiuka Katiba, akidai hana imani na wajumbe wake.
Pia ameigomea kwa kudai kuwa tayari alishafahamu kwamba Kamati hiyo ilikuwa na maamuzi
ya kumfukuza uanachama, kupitia barua pepe aliyoinasa ikitoka kwa Katibu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kwenda kwa Mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mh Hamad ambaye pia ni Mjumbe wa
Baraza Kuu la CUF alisema alipokea barua ya kuitwa kuhojiwa kwa tuhuma za kwenda kinyume cha Katiba ya CUF, Desemba 23, mwaka huu na kikao hicho kilifanyika rasmi jana.
Alisema baada ya kuhudhuria kikao hicho, alilazimika kukigomea kuendelea kumjadili kutokana na kutokuwakubali wajumbe watano kati ya wanane akiwemo Mwenyekiti wa Kamati
hiyo ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CUF, Machano Khamis Ali na Katibu wake Hamis Hassan.
Alisema viongozi hao wawili amewakataa kutokana na ushiriki wao katika kumtuhumu.
Alisema hana imani na Machano baada ya kiongozi huyo kuahidi kumshughulikia katika
kikao kilichofanyika hivi karibuni bila ya kumpa nafasi ya kusikiliza upande wake.
Aidha, kwa upande wa Hassan, Hamad alisema Katibu huyo alimtuhumu kwa kumuandikia
Lipumba barua na kumtuhumu kuwa (yeye) ni chachu ya kuchafuka kwa hali ya kisiasa ndani
ya chama na kwamba pamoja na washirika wake, wamekuwa wakifanya mbinu za chini
kwa chini kumuondoa Lipumba kwenye nafasi yake.
Alisema pia katika Katiba ya CUF hakuna kipengele chochote kinachozungumzia Kamati
ya Nidhamu na maadili hivyo alikuwa na sababu ya kuikataa Kamati hiyo.
Pamoja na hayo, pia alisema sababu iliyomfanya aigomee Kamati hiyo ni baada ya kufahamu
kuwa tayari wajumbe wake walikuwa na uamuzi wa kumfukuza uanachama kupitia barua pepe ya Maalim Seif kwenda kwa Lipumba.
Aliinukuu barua pepe hiyo ambayo ilisema “Nimeshauriana na Makamu tumeona kuna ahadi ya jamaa yako (Hamad) na genge lake kuitwa kwenye Kamati ya Nidhamu kuhojiwa, ushahidi wa kutosha umekusanywa dhidi yake…Kamati hiyo italeta taarifa kwa Kamati Kuu ya Taifa.
“Kamati Kuu ya Taifa ifanye uamuzi mgumu wa kuwasimamisha uongozi vinara wao na
wengine kupewa karipio, Kamati hiyo ifikishe taarifa yake katika kikao kitakachofanyika Februari mwakani... muono wetu tumfukuze kwenye chama na akienda mahakamani, ikitoa
uamuzi wa kumpendelea, mwache awe Mbunge wa Mahakama kama akina Asha Ngede na Naila
Majid,” Hamad alinukuu barua pepe hiyo.
Aidha, alisema katika barua pepe hiyo, Maalim Seif alimshauri Lipumba kuwa ikiwezekana
na Hamad Rashid aachwe hata akienda Chadema, CCM au aendelee na urafiki wake na
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa.
“Jamani hii ni dhambi kubwa anayoifanya Maalim Seif, mimi namheshimu sana na ndio maana nataka ajipime mwenyewe kwani haya ndio yaliyomfanya Jumbe ajiuzulu,” alidai mwanasiasa huyo mkongwe.
Alisema hana ukaribu wowote na Lowassa zaidi ya kusalimiana kawaida kama watu wengine.
Alisema amezushiwa mambo mengi, ameitwa muasi na anataka kukibomoa chama, wakati
amekuwa kiungo muhimu baina ya Wazanzibari na Wabara ndani ya CUF.
Aidha, alisema amesaidia kampeni hadi ya Lipumba wakati wa uchaguzi na kufadhili baadhi ya wabunge tofauti na Maalim Seif, aliyedai hajawahi hata kufungua mkutano mmoja wa chama Bara.
“Namuomba Maalim Seif kwa hali iliyofikia kama anataka kujisafisha na kuheshimika, basi
afuate nyendo za aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela na Baba wa Taifa hayati
Mwalimu Julius Nyerere,” alisema.
Alisema hali ya chama hicho ni tete kwa kuwa hakiendeshwi kwa haki na mambo mengi ya kusingiziana na kuzushiana huku fedha nyingi zikitumika bila maelezo na iwapo watu
wakihoji wanaitwa waasi.
Alihoji inakuwaje chama hicho kimekaa zaidi ya miaka mitatu na CCM kujadili muafaka wa
Zanzibar na kushindwa kukaa hata kikao kimoja kujadili na kufikia muafaka kuhusu mgogoro
unaoendelea.
Naye mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Doyo Hassan Doyo, alisema wanachokitaka kwa sasa ni kukirejesha chama hicho katika hali inayokubalika kwa pande zote Bara na Visiwani ikiwemo kuhakikisha fedha za ruzuku za chama zinafikia maeneo yote.
“Sisi tunapata kwa mwezi Sh milioni 124 na michango ya fedha za wabunge takribani Sh
milioni 60, jumla ni Sh milioni 190 hadi 200 lakini fedha hizi zinaishia makao makuu, huko
wilayani watu wanazisikia tu, tukihoji tunaitwa waasi,” alidai Doyo.
Kwa sasa sakata hilo, baada ya Hamad Rashid kuigomea Kamati ya Nidhamu na Maadili linasubiri kuwasilishwa wakati wowote mbele ya Baraza Kuu la CUF kwa majadiliano zaidi.
Chanzo: HABARI LEO


Na yeye amechoka kama alivyochoka huyo Sefu anayemsema.
ReplyDeleteHivi yeye anajiona ni kijana mpaka kushikilia kutaka kugombea ukatibu mkuu?
Awawachie vijana wanaoweza kukimbizana na harakati za kuimarisha chama.
Makomredi vipi tena au ndio choyo na husda vimeanza?
ReplyDeleteSawa Sheikh Hamad Rashid,,,Ni kweli kabisa pana maswali mengi ya kuuliza ambayo majibu ni kidogo sana hela zote hizo Shs.200 Millioni hapo Makao Makuu Buguruni zinaenda wapi wakati muda huu hakuna hata Uchaguzi mdogo?
ReplyDeleteMamad Rashid ametoa wapi ridhaa ya kuimarisha CUF huku Tanzania Bara? CUF inaeleweka kwamba wanachama wake hawataki muungano na sisi makafiri, machogo, watu wa mrima, au Watanzania Bara.
ReplyDeleteKama wazanzibari wengi tulikuwa tunasema na walokuwa hawakukubaliana nasi wakati huo wanaona ukweli, wanasiasa wote wa CUF zanzibar wako chamani kwa manufu yao tu, na wakati wowote wakipewa madaraka makubwa zaidi kwenye ccm au serikali watatoka CUF. Kila mtu anajua sababu kubwa iliyomfanya sharif akubali kushindwa uchaguzi ni madaraka aliyoahidiwa na sio kwa manufaa ya chama chake, wanachama wa CUF au Zanzibar.
ReplyDeleteHawa jamaa kujifanya hawataki MUUNGANO ni geresha tu!
ReplyDeleteWanajua sana kuwa wao ndio wananufaika sana!
Sasa hebu angalia kelele zote za Maalim kabla ya kupata Uongozi Serikalini zilikuwaje?
Na sasa mbona yupo kimya?...ina maana anajua napata maslahi!
Hawa Wazanzibari bwana, kazi kula chukuchuku la samaki na ndimu ,hadi vitunguu na nyanya wana import kutoka Bara!
Unakuta Bosi wa Kizanzibari anamaliza safari za kikazi Bara anajiandaa kurudi Kisiwani kabla ya kupanda Boti, breki ya kwanza ni Sokoni Kariakoo ,ndani ya BRIEF CASE LA DOCUMENTS zake anachanganya anajaza na Vitunguu,Nyanya,Tangawizi,Pilipili hoho na Nyama ya mbuzi!!!
Hii ndivyo ilivyo kwa Mzanzibari awe Mwana CUF au asiwe atapiga kelele akiwa hajapata madaraka akipata ananyamaza KIMYA KWA VILE ANAJUA WAO ZANZIBAR WAPO VINYWA WAZI SANA WANAOSHA SANA VINYWA NA WANATOKA SANA KUPITIA HUO HUO MUUNGANO WANAOUKEJELI!!!
Hamadi, chonde chonde usiende chadema, utabebeshwa msalaba ndugu yangu. Bora hata uunde chama chako.
ReplyDeleteUcheni udini! waengine munaabudi mashetani, bila kutisha kwa uchawi hupati cheo au uongozi kwenye nanihiii.............
ReplyDeleteWewe Anonymous Thu Dec 29, 12:17:00 PM 2011
ReplyDeleteUcheni udini!,,,, uongozi kwenye nanihiii..........
Sasa hujui kuwa KUBEBESHWA MSALABA NDIO KUABUDIA SHETANI KWENYEWE HUKO?