Vijana wengi hapa jijini Dar ambao wanacheza mchezo huu wa kutembea na viatu vya matairi hupenda sana kufanya michezo hiyo kwa kushika magari kwa nyuma namna hii na kusafiri umbali mrefu na kurudi huku akiwa hana tahadhari ya namna yeyote,jambo ambalo linaweza kusababisha hari ya hatari kwa maisha yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Hawa madogo vichwa ngumu saaana...kujiliwaza gani huku?, hivi kweli hakuna mazingira mengine ya kufanyia michezo ya namna hii hadi ktk mabara bara yetu na hali yake kama ilivyo na madereva wetu hawa mbili kasorobo?

    Wengine watoto wanafanya mchezo huu kwao majumbani wazazi wao na ndugu hawajui kabisa kinachoendelea!

    Tena utakuta mtoto anafanya hivi hali ya familia yake ni mwenzangu na mimi!,,,pooo kavunjika matibabu mgogoro!,,,au puuu kafa unakuta yeye ni mtoto pekee anategemewa!

    Ya nini presha yote hii?

    ReplyDelete
  2. mwache amwage maini kajitolea huyo kwani ukiangalia umri wake anaweza kujuwa baya na zuri

    ReplyDelete
  3. Waache wacheze, "asiyefunzwa na mamaye, ............."

    ReplyDelete
  4. kwani wakifa tatizo ni nini? wanatujazia tu hewa chafu, acha wafe.

    ReplyDelete
  5. Tusiwaache hawa vijana kwani, ni ''teenegers''. Matatizo ya huo umri kila mtu mzima anayajua. Wakatazwe wasijiletee hatari

    ReplyDelete
  6. hao hawajui kuwa wenzao wanocheza huu mchezo wanalipwa na masponsor na pia kuna hospitali za kueleweka sio MUHIMBILI

    ReplyDelete
  7. Ni mchezo wa kifo, halafu ni wabishi ka nini inabidi we mwenye gari ndo umuangali kama yuko mbele yako. Ni vyema wakamatwe na kutozwa faini kwa matumizi mabaya ya barabara La sivyo tutaishia kulaumiana na kuvunjiana vioo vya gari bure.Maana wabongo wahisi kila ajali mwenye kosa ni mwenye gari bila kuangalia mtu huyo amegongwa katika mazingira gani.

    ReplyDelete
  8. Tuwanunulie magari traffic polisi wetu ile watembee barabarani na kuwatokomeza watu kama hawa ambao wanahatarisha maisha ya kila mtu.

    ReplyDelete
  9. Mkuu si ungeandika Kiswahili inachokijua tu, hiyo broken English imeniacha hoi bin taabaan!

    ReplyDelete
  10. Mkuu si ungeandika Kiswahili inachokijua tu, hiyo broken English imeniacha hoi bin taabaan!

    ReplyDelete
  11. Polisi traffic wapo kibao na wamepewa pikipiki,inashangaza wanashindwa kuzuia kitu kama hiki.Mimi nafikiri polisi wapewe somo.

    ReplyDelete
  12. nNYINYI HAMJUI KUA HUYU HAPA ANAKUA KISHASAVE NAULI YAKE HAPO ANAKWENDA ANAKOTAKA BILA YA KULIPA

    ReplyDelete
  13. sorry hii post ya mda lakin nimesoma comments na mi nimeona nchangie! jaman msisahau huu cio mchezo tuu ni usafiri pia! afu kama hamwatak barabarani si mu wajengee maeneo yao special!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...