Mkuu wa wilaya ya Korogwe Bw. Erasto Sima, akifungua mdahalo ulioandaliwa na Mtandao wa Asasi za Kiraia wilayani Korogwe na kufanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kanisa Katoliki katika mji wa Mombo, wilaya Korogwe, lengo la mdahalo huo lilikuwa ni kuwajengea uwezo wananchi wa wilaya hiyo ili waweze kutoa maoni yao wakati wa tume ya kukusanya maoni hayo itakapopita katika maeneo mbalimbali nchini.
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Bw. Stephen Ngonyani 'Almaarufu Profesa Majimarefu', akitoa utangulizi kwa wajumbe waliohudhuria mdahalo kwenye ukumbi wa kanisa katoliki lililopo katika mji mdogo wa Mombo ambapo mbunge huyo alisema wananchi wana umuhimu mkubwa wa kutoa maoni ya katiba hiyo kwa kamati hiyo kwa faida ya maendeleo ya nchi yetu na vizazi vijavyo.
Mtoa mada Bw. Jonathan Ernest Mgongola ambaye ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Handeni mkoani Tanga, akichambua vifungu mbalimbali vya katiba pamoja na kuwaeleza wajumbe wa mdahalo huo umuhimu na faida ya kushiriki kutoa maoni wakati kamati itakayoundwa na Rais kupita na kukusanya maoni yao juu ya marekebisho hayo ya katiba.
Wazee ambao nao walishiriki mdahalo huo uliofanyika kwenye ukumbi wa kanisa Katoliki katika mji mdogo wa Mombo wilayani Korogwe, wakisikiliza kwa makini jinsi watoa mada wakifafanua vipengele mbalimbali vya katiba ya sasa ili waweze kuwa na uelewa mpana wa katiba kabla ya kutoa maoni hayo kwa kamati itakayoundwa na Rais.Picha na Mashaka Mhando wa Globu ya jamii, Tanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Aaaah masikini huyo mama hapo mbele pengine hata chai hajanywa leo munamwambia mjadala wa katiba wa nini?

    ReplyDelete
  2. vijana wakowapi? au wito huu ulikuwa kwa wazee wa Tanga.

    ReplyDelete
  3. wee! sio swala la chai!! huyo mama anasikiliza kwa makini!!! ahh...!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...