Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Bw. Absalom Kibanda akiongea na wanahabari wakati wa msiba wa Mwanahabari Danny Mwakiteleko siku zilizopita |
Mahakamani Kisutu
Waandishi wa habari wa vyombo tofauti tofauti leo walijaa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu muda mfupi uliopita kusikiliza kesi inayomkabili mwandishi mwenzao ambaye ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Bw. Absalom Kibanda (45).
Kibanda aliunganishwa leo katika kesi inayomkabili Samson Mwigamba (36) ya kuchapisha habari katika gazeti hilo habari inayodaiwa kuhamasisha askari kutotii amri ya wakuu wao wa kazi ambao ni mamlaka halali.
Mwigamba ilidaiwa kuwa hakuwepo mahakamani alikuwa Arusha ambako anakabiliwa na kesi nyingine namba 5/2011 kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wakili wake Mhozya John.
Akisomewa mashitaka Mhariri Kibanda alidaiwa na wakili wa serikali Beatrice Kagonda mbele ya hakimu Stuwart Sanga, kuwa Novemba 30 mwaka huu alitoa habari katika gazeti lhilo yenye kichwa cha habari kisemacho “Waraka Maalum kwa Askari wote” habari ambayo inahamasisha askari kutotii mamlaka halali.
Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Kibanda alikana mashitaka na jopo la mawakili linalomtetea, wakili Deo Ringia, Isaya Matambo, Juvenalis Ngowi na Nyaronyo Kicheere waliomba dhamana kwa mteja wao.
Hakimu Sanga alisema masharti katika kesi hiyo ni yale yaliyowekwa Desemba 8 mwaka huu kesi hiyo ilipokuja kwa mara ya kwanza kwa mshitakiwa wa kwanza (Mwigamba.)
kuwasilisha hati ya mali isiyoamishika yenye thamani ya shilingi milioni tano na kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini hati ya dhamana ya Sh milioni tano kila mmoja, mashalti mengine ni kusalimisha hati ya kusafiria na kuripoti Polisi kati kila mwezi.
Mwigamba anadaiwa Novemba 30 mwaka huu, toleo Na.2553 lilichapisha safu hiyo iliyokuwa na kichwa cha habari “Waraka Maalum kwa Askari wote”
Mwigamba alifikishwa mahakamani Desemba 8 mwaka huu na kusomewa mashitaka hayo alidaiwa kuandika makala inayotoa ushawishi kwa jeshi nchini kutotii wakuu wao halali kinyume cha sheria. ya Kanuni ya Adhabu. Mwigambaanaandika Safu ya Kalamu ya Mwigamba, safu inayotoka kila Jumatano katika gazeti la Tanzania Daima,
, Kesi hiyo imepangwa itajwe Januari 19 mwaka huu kwa kuwa upelelezi katika kesi hiyo haujakamilika.
Kama Libya na Egypy wandundu walipohasi.. Balaa hii!
ReplyDeleteHeee sasa mbona hiyo makala yenyewe ni ya kutoa elimu kwa askari wetu na si jinai..je ni kosa kuwakumbusha kwamba askari nao ni binadamu kama cc..kwani wao wanalipwa bei gani kwa mwezi mpaka wasielewe kuwa hali mbaya?ukombozi wa kweli unakuja na mnaotuibia ni lazima mtaenda jela na tutarudisha mali za nchi yetu mnazoendelea kuiba..aluta kontinua...
ReplyDeleteZITTO KABWE KAZI KWAKO KUPAMBANA NA WAKUBWA WANAO PAMBANA NA WAANDISHI WA HABARI PALE WANAPOANDIKA HABARI ZINAZOHUSU UKWELI.TUNAOMBA UPAMBANE NA HILI JAMBO TUNAONA TAIFA LINAVYOTEKETEA BILA KUWA NA TRANSPARENCY JOUNALISM
ReplyDeleteHapana elimu hapo ni uchokozi tu huo kwa serikali,Kama elimu hiyo ilikua inawafaa askari basi makala hiyo angewatumia ktk vyombo vyao vya mawasiliano eg.Email,posta,.....na sio public kwa sababu kuanika mambo ya wanausalama wa nchi na mwajiri wao serikali ni kuwachonganisha na badala yake askari wenyewe wangefaa ndio wayaibue madai yao hayo.vyombo vya habari vinamchango mkubwa kwenye kuivuruga au kuiboresha amani. Tuache jazba za kushabikia mambo bila kuona matokeo yake baadae,wao waandishi wanachokifanya wanajua na miongoni mwao ni kutaka kuungwa mkono na jamii kwa kuidanganya kupitia mambo kadhaa na wakati mwengine kwa kutumiwa na mafisadi kama njia za kupambana na mahasimu zao ktk serikali.
ReplyDeleteMadudu yaliyomtokea Jerry Muro mpaka kesi inaisha kwa aibu kubwa,,,Jamani Mamlaka hazijifunzi tu???...ni yaleyale yanamtokea tena Mhariri wa Tanzania Daima Absalom Kibanda na mwenzie Samson Mwigamba!
ReplyDeleteSerikali mara nyingi inajitia kitanzi yenyewe. Waraka huo (uliochapishwa na gazeti la Tanzania Daima), ulikuwa umesomwa na watanzania 1% tu, lakini kutokana na kesi hii kila mtanzania anataka kusoma waraka wenyewe, na hata askari (ambao si wasomaji wa magazeti) nao pia wanatafuta waraka huo wausome.
ReplyDeleteNa pale watakapogundua waraka huo unasema kweli kuhusu haki zao, basi tutarajie askari kupigania haki zao (kama raia mwingine yeyote wa Tanzania).
Polisi nao imewachoma kwani hali halisi wanaiona 3quarter maisha taabu,ni mabosi wao ndiyo wanapata mayai&humberg kwa kulinda maslahi ya mabosi,hongereni wahariri ujumbe na elimu vimefika.Siku si nyingi ukombozi wa kweli utapatikana.
ReplyDeleteKatika sakata la Jerry Muro Bosi wa Polisi ambaye ni Alhaji ,Sheikh alikuwa mpikaji wa sumu,,,je hili ni nani Mpishi?
ReplyDelete