Kikosi cha Timu ya Yanga
 Kikosi cha Timu ya Azam
Nurdin Bakari (katikati) akimiliki mpira huku akizongwa na mshambuliaji wa Azam, Humud Mohamed katika mchezo wa kirafiki wa kuchangia walemavu uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini dar es Salaam leo. Azam imeshinda 2-0.
Mshambuliaji wa Yanga, Keneth Asamoah akiruka daluga la beki wa Azam, Agrey Morris.
Mshambuliaji wa Yanga, Pius Kisambale wa Yanga akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Azam, Said Morad.
Mshambuliaji wa Azam, Mrisho Ngasa akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Yanga, Salum Telela katika mchezo wa kirafiki wa kuchangia walemavu uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa leo. Azam imeshinda 2-0.
Wachezaji wa timu ya Azam FC wakishangili ushindi wa timu yao.Picha na Francis Dande.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. wachezaji wetu bwana kwa kusema kweli wamechoka , yani wakifua hizo jersey uwezi wataambua kama hata ni wana michezo. jamani wakubwa mazoezi ya mpira si kukimbizana tu na kutoka jasho , kuna kula pia. lol
    mdau paris

    ReplyDelete
  2. klabu zetu hovyo,hao wachezaji ukiwaita timu ya taifa hamna kitu hawana msaada wowote kwenye soka letu siwakubali kabisa ni mizigo tu,kwanza hata miili ya kimichezo hawana uozo mtupu

    ReplyDelete
  3. Hahahaha Mdau wa Paris umesasambua!!!

    Mipango ya lishe inahitajika saana kwa Wachezaji wetu hasa angalau timu ya Taifa wangekuwa hata wanapewa Kupon za madishi ktk Hoteli kubwa kubwa badala ya Mashabiki kuwakirimu kwa Pombe ktk Mabaa na kuwaunganisha na shawishi za Ngono zembe!

    ReplyDelete
  4. tazama soksi za wachezaji wa Yanga,
    aibu tupu na hapo mechi ndo inaanza

    ReplyDelete
  5. Mbona hakuna mashabiki??? Au kwa sababu hizi ( yanga and azam ) zimejaa wachovu watupu

    ReplyDelete
  6. azam endeleeni vivyo hivyo, hata simba wakija jitahidini kuwafunga, tuondoe mawazo mgando ya usimba na uyanga yanaharibu maendeleo ya soka tz.
    SHABIKI WA AZAM
    THE BRAIN

    ReplyDelete
  7. Safari ya Ngasa Marekani imeota mbawa? Anaenda au haendi?

    ReplyDelete
  8. HUYU WALIMWAMBIA KUWA HAWAMCHUKUI,SASA YEYE NA WAKALA WAKE ILI WASIAIBIKE WAKASEMA KUWA ATAENDA DESEMBA WAKIDHANI KUWA DESEMBA NI MIAKA 50 IJAYO,SASA DESEMBA IMEFIKA MBONA KIMYA KINGI.
    KIJANA ALISHAPATA SIFA ZA KIJINGA NA KUINGIA KTK MAMBO YA NGONO,MARA LEO HUYU KESHO YULE,MPIRA HAUTAJI HIVYO UNAHITAJI DISCPLINE YA HALI YA JUU,MAMBO YA KUNGONOA HOVYO HANAWAMALIZA NGUVU NA HIVI VICHIPSI VYENU MNAVYOSHINDIA BAADA YA KUTOKA ZOEZI BADALA YA KULA DONA.MTU KAMA NGASA ALIHITAJI MSIMAMIZI WA KUANGALIA MUENENDO WAKE WA MAZOEZI PAMOJA NA LISHE KAMA KWELI ALIAHIDIWA NAFASI KULE NA INGEWEZEKANA PIA AKAISHI KAMBINI NA SI NYUMBANI KWAKE,MAANA WALE JAMAA FIKIRIA MUDA WOTE TANGU UFANYE ZOEZI MPAKA LEO AMEONGEZEKA MWILI?AU AMEONGEZEKA MSULI?NGASA WA LEO SIYO YULE ALIYEKUWA KAGERA SUGAR,WA LEO AMECHUJA SANA KWA HIYO HAWEZI PATA NAFASI ULAYA LABDA KUBEBA BOKSI/KUCHUMA MATUNDA KAMA MWAMEJA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...