kaka michuzi tafadhali weka malalamiko yangu kwa kampuni ya simu ya TIGO, leo ni wiki ya tatu mfululizo hakuna anaepokea simu za customer care nikipiga kueleza shida yangu, namba ninazopiga ni, 100, 150, 0716123103, 0713800800 nimejaribu kwenda mlimani city na Ohio ofisini kwao nillikuta foleni kubwa mno kiasi ambacho ingenibidi nisubiri kuhudumiwa kwa muda usiopungua masaa matatu. Kama huamini piga namba hizo.
Nawashauri TIGO warekebishe huduma ya simu customer care ili wapunguze hata hii kadhia ya kupanga foleni kwa tatizo ambalo pengine lingetatuliwa kwa maelezo ya simu na mtu wa customer care. hebu fikiri, mtu unaishi na kufanya shughuli zako gongo la mboto, kibamba na kwengineko nje ya mji inakubidi uje mjini/mlimani ili utatauliwe kijitatizo ambacho customer care wangeweza kulitatua kwa maelezo ya simu tu. nawaomba tigo warekebishe hilo.
mdau wa tigo
D. ESMAEEL
Unayosema ni kweli, TIGO wamekua na wateja wengi sana lakini utaratibu wao wakuwahudumia ni mbovu sana sana sana. Hawapokei simu kabisa. Na kama ulivyosema ukienda kwenye ofisi zao foleni ni kubwa sana na speed yao ni ndogo kweli kweli. Wakishachoka ndo usiseme. Niliwahi kuambiwa kwamba pia huwa wanatoza kiasi fulani cha hela unapopiga hizo simu zao za huduma kwa wateja. Labda hawapokei ili upige mara nyingi wao waingize kipato.
ReplyDeleteinakera sana ndugu mdau kwa huduma za tigo hasa customer care mimi kuna siku nilipiga simu nikaiacha kwenye loud speaker nakaendelea na shughuli zangu nikisikilizia lakini wapi hawakupokea kamwe mpaka nilipoenda mlimani city napo foleni ndio usiseme
ReplyDeleteinakera sana.
Ni kweli kabisa hata promotion yao ni feki siku moja niliweka voucher ya Shs.10,000/= lakini nilibakiza kama dakika 5 hivi from nowhere ule muda ukaisha kimchezo mchezo. Hiyo siyo biashara ni utapeli tena wa wazi wazi. Ukiwapigia simu Customer Service hawapokei - Sasa hii ni biashara gani? Wasipokuwa makini sisi wote tutahamia kwenye mitandao mingine. TIGO MMEUNGUZA
ReplyDeleteMnalalamika nini hamie basi kubwa TIGO kwishnee sasa hivi.
ReplyDeletemi nimehamia eatel cku nyingi nilichoshwa na mambo ya Tigo
ReplyDeleteTIGO ni mtandao unaoongoza kwa kutoa huduma mbaya Tanzania. Customer care is negative, negative, negative.
ReplyDeleteNi kweji jamaa waramba pesa ile mbaya unapopiga wakati mwengine wanapokea na kukuweka kwenye kusubiri uhudumiwe unashtukia salio lako limeisha, mimi naamini ni ujanja fulani wa kuwaramba wateja
ReplyDeleteWadau
ReplyDeleteWanachofanya tigo, pia kinafanywa na Airtel na hata Vodacom, inakuwaje basi. Huduma hii ya customer care wanaikodishia kampuni nyingine bila wewe kujua ukipiga simu unafikiri unapiga kwa service provider kumbe kwa mtoa huduma wa kati. Hili ndilo tatizo na hata Tigo, au Airtel au Vodacom hawana muda wa kufuatilia jambo hili. Ndiyo maana utaona hata namba muhimu kama za Polisi ziko kama za mmiliki wa kawaida. Namba muhimu kama hizi huwa ni fupi sana tena zinazofuatana na huwa ni nyeti sana, kumbukeni zamani ukipiga 999 unapokelewa Hospitali, Polisi kwa wakati mmoja. Hii ndiyo biashara ilivyo katika enzi hizi, wote hawa watatukamua mpaka wafurahi ukizingatia siku hizi huduma ya utumaji pesa na kupata huduma nyingine kama vile DAWASCO, DSTV, StarTimes zilivyotegwa kiasi kwamba ukitoka basi wewe umeamua kuishi maisha ya miaka kabla ya Uhuru wa Tanganyika!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Jamani poleni sana mimi nilihudumiwa vizuri na tigo internet line ambayo ipo kwenye vipeperushi na matangazo ni 0713800902 hapa ni huduma za internet siyo ulizotaja hapo juu,
ReplyDeleteTigo babukubwa!!!!ahami mtu hapa.
Asante sana mdau umeniwahi kwasababu nami nilikuwa nataka kulalamikia swala hili hili halafu lingine swala la kulipia Customer care ya Tigo, mimi kwa upande wangu naona si vyema kulipia kwasababu sisi tunatoa malalamiko yetu ambayo ni njia moja wapo ya wao kuboresha huduma zao sasa iweje maoni yalipiwe!? ni hayo tu.
ReplyDeleteHAO NDIO TIGO BWANAAAA WANATUZINGUAAAA HALAFU HATUHAMI, SIJUI WAMETUROGA NA NINI!!!??
ReplyDeleteMIMI SIWAPENDI ILE MBAYAAAA! YAANI MGAO WA MAJI, UMEME NA SASA HADI MAWASILIANO?!!!!! TIGO NI KAMPUNI YA SIMU ISIYOJUA KABISAAA HUDUMA KWA WATEJA, INAYODHARAU WATEJA NA KWA KIFUPI NI KAMPUNI AMBAYO INAJITAHIDI SAAAAAANA KUPUNGUZA WATEJA BADALA YA KUONGEZA!! HONGERA SAANA TIGO!!!!
HAO NDIO TIGO BWANAAAA WANATUZINGUAAAA HALAFU HATUHAMI, SIJUI WAMETUROGA NA NINI!!!??
ReplyDeleteMIMI SIWAPENDI ILE MBAYAAAA! YAANI MGAO WA MAJI, UMEME NA SASA HADI MAWASILIANO?!!!!! TIGO NI KAMPUNI YA SIMU ISIYOJUA KABISAAA HUDUMA KWA WATEJA, INAYODHARAU WATEJA NA KWA KIFUPI NI KAMPUNI AMBAYO INAJITAHIDI SAAAAAANA KUPUNGUZA WATEJA BADALA YA KUONGEZA!! HONGERA SAANA TIGO!!!!
TCRA mko wapi? wateja wa TIGO tunaumwizwa!
ReplyDeletetigo wanaboa siku hizi halafu makato yao hayaeleweki, nikisema wanadhulumu fedha za wateja wao nitakuwa sijakosea..
ReplyDeleteBiashara ushindani, kwani ukliambiwa ukihama ndo mwisho wa kuwasiliana,Maisha yakupe stress,folen stress sasa hata simu ambayo una option ya kubadili line inakupa stress,a wapi mi nilishama zamani
ReplyDeleteAirtel naona wanajitahidi sana hawana longo long ,Mi nilichoka pale ambapo nilikuwa nampigia ndugu yangu mara 4 naambia namba haipo,sio hiyo hiyo nilihamia Airtel na huwezi amini naenjoy maisha sana.
Ushauri wa bure, We hamia tu ukiona hapakuafai hamia kwingine,wateja tuna uhuru sana
Si afadhali ya hilo kukatwa hela siku hizi wanatabia kama unampigia mtu simu haipatikan wanaanza kukupigia manyimbo then wanakwambia kama unataka huo wimbo sijui fanya hivi na kibaya zaidi wanakwambia simu unayopiga haipatikani
ReplyDeleteBURE SIKU ZOTE NI AGHALI.... ACHANI KULALAMIKA NJOONI VODACOM MTASAHAU MATATIZO YOTE HAYO. MSIOGOPE GHARAMA
ReplyDeletetigo sasa wamekaa kisanii zaidi, tuliwaamini but now mmh very stupid kwakweli, kama wanasoma humu leo hii waelewe, watakufa kifo kizuri km ttcl,au ndo wanataka kujustfy kuiuza tena? mara unashangaa jina limechange inaitwa VUZE ( au malizia na ZI badala ya ZE) Tanzania!
ReplyDeletetena washenzi kabisa, kwanza promosheni zao ni wizi mtupu, hata ile promosheni ya milioni 100, hakuna aliyeshinda, kuna mtu alipandikizwa tu, ukitaka ankal michuzi ushahidi ninao, na mtu ninamjua aliyechongeshewa dili, tigo wezi sana na nadhani ndo mchezo wa watu mitandao, natamani niishi bila simu, kwa ajali ya huu upumbavu wao, mimi natumia HTC phone,eti nilienda pale mlimani city ili niconnect internet, muhudumu anasema kwa kweli hii simu ni mpya siwezi kuitumia,nilibaki mdomo wazi, nikamwambia ina maana hawapewi training kabla ya kuanza kazi? huyo kaka akajikanyaga hata hajui aongee nini, kweli tigo, hawana akili hata kidogo, na sasa hivi wameanza kamtindo, ukipiga simu unasikia ule wimbo wa marlow wa mbayumbayu, hapo ujue simu haipatikani, kah mnakera sana tigo, jirekebisheni tafadhali, na promosheni zenu ziwe za ukweli sio kuibia watu, mtu unakuta ana kahela kake mia 500, anajitahidi kucheza halafu nyie mnamwibia sio poa hata kidogo
ReplyDeleteTigo ni mtandao wa wanafunzi na watu walio na muda wa kuchezea. Hamia huku..
ReplyDeletesijui wanafanyaga nini huko. jana nlipiga simu tigo for about 38 minutes inaita tuuuu ndo wakapokea then huyo kaka akasema simu ni nyingi ila mimi sidhani kama hiyo ni sababu tosha.... wameshashuka viwango na vocha zao wanatoa kumbe hawaja zi activate. wanakeraa jamani.......
ReplyDeleteHii kampuni itakufa kifo cha mende, nyie subirini tuu muda si mrefu
ReplyDeletewadau kuna kitu kinaitwa voice mail. Baba hawajamaa noma.Ukimpigia mtu ukamkosa jamaa wanakutumbukiza kwenye Voicemail kwa lazima halafu unaendelea kuliwa uongee au usiongee shauri yako. Hii unaingia through kubonyeza key yoyote ile. Yaani sasa hivi TIGO kipenzi chetu wanafunzi kwisha habari yake. Ni hatari kama ukoma. BEWARE my Tigo friends kumpoteza mteja ni easy ila kumrudisha ni kazi mara mia.
ReplyDeleteKATIKA HILI NAMI SIWEZI KUKAA KIMYA. NILINUNUA LUKU HELA YANGU IKAPOTELEA HUKO, ILIKUWA USIKU NIKALALA GIZA, KESHO YAKE NIAENDA KWENYE SHUGHULU NIKARUDI LATE KUFIKA NYUMBANI NDO NASHITUKA SINA UMEME, HIYO SIKU YA PILI BILA UMEME HADI NILIPOAMUA KWENDA KUINGIA GHARAMA NYINGINE NILIPIGA SIMU CUSTOMER CARE UNASUBIRI MPAKA DK TANO SIMU INAITA NA HAKUNA WA KUPOKEA NA NIMESHAPIGA SANA KUJUA PESA YANGU VIPI NA HAKUNA MAJIBU. PESA YANGU JAPO NDOGO ILINIUMA SANA KULALA GIZA.
ReplyDeleteHamia Airtel, kwani hamsikii matangazo kila siku??? sio utani huduma ya uhakika na kweli. Tigo ukienda kibamba tu network mgogoro. Mie nililalamika weee sasa nishaipiga chini niko airtel, kama ofa wanazo nao kibaoo sasa kwanini ning'ang'anie maumivu??? Hamia Airtel
ReplyDeletekwani si muache kuwa kumiliki simu mbona zamani maisha yalikuwa yanakwenda tu. Kuna watu maarufu duniani hawamiliki simu na wanamahela yao kibao. Tatizo Tanzania tunajiendekeza, na tunaongoza kwa matumizi ya simu Afrika na kumiliki simu za bei mbaya wakati uchumi wetu wenyewe mdororo. Mithupu tuanzishe kampeni ya kutotumia simu kwa mwezi mmoja tuone kama hatutishi. Najua utaibania hii kwa kuwa Vodacom wanakufadhili ila ujue nao ni wale wale wanakula hela zetu tu. Wanajenga minara hadi vijijini badala ya kujenga zahanati ama vituo vya afya.
ReplyDeleteTatizo la Tigo hata network yao saivi hapa DSM ni shida tupu sembuse kupiga customer care??kuna usanii mwingi wanafanya ila kuna mtandao mmoja uko kimya kimya jamaa wanafanyakazi vizuri
ReplyDeleteHiyo habari ya kupandikizwa mshindi wa milioni 100 nani asoijua?hata ankal analijua hilo pengine kashikishwa ndio maana hajaitoa!
ReplyDeleteTigo wana mambo ya ajabu sana kudadadeki zao
Kwa mtazamo wangu, kampuni zote za simu zinamtindo unaofanana wa huduma kwa wateja na uongo mwingiii kwenye matangazo mara unlimited mara sijui nini uaongo mtupu! Cha msingi ni kuangalia sheria itakayotuwezesha wateja kuyashikisha adabu haya makampuni ya simu pindi tukipata huduma chini ya kiwango kinachotangazwa.
ReplyDeleteYote tisa, wana promosheni yao unapigiwa simu kwa namba zenye sifuri na tisa tisa kibao, ukipokea eti unaambiwa ujiunge ili upate marafiki wapya, come on... mie marafiki nilionao wananitia kizunguzungu sasa nyie tena mnataka kuniongezea vimeo, alaah! Kama haitoshi wanatuma sms kibao za promotion za ajabu ajabu kwenye simu, mtu unadhania imeingia sms ya maana kutoka kwa watu wako, kumbe wao wanakulazimisha usome utumbo wao, sio watu wote tuko after promotion... inakera kiukweli.
ReplyDeleteWabongo bwana sasa mnacholalamika ni nini? Kwani mmelazimishwa??? Yaani mnaona jahazi linazama na bado mnasubiri awajibu, poleni!!
ReplyDeleteNdugu Mteja wa Tigo,
ReplyDeleteSamahani kwa usumbufu uliokutokea. Tunatoza kiwango kimoja tu cha Tsh 50 unapopiga huduma kwa wateja Tigo. Hivyo, haijalishi simu imechukua muda gani, utatozwa kiwango kimoja tu cha Tsh 50.
Unaweza kuwasilisha tatizo lako kwenye ukurasa wa Tigo katika mitandao jamii ya Facebook na Twitter. Ukurasa wa Tigo kwenye Facebook sehemu ya huduma kwa wateja ni: http://www.facebook.com/TigoTanzania?sk=app_282053001833414
Ukiwa unavinjari mtandao kwenye simu, tembelea tovuti ya Tigo huduma kwa wateja: http://m.tigo.co.tz/customercare
Kama msaada zaidi utahitajika, unaweza kupiga 0713 800 902 kuhusu Tigo Internet; piga 150 kuhusu Tigo Pesa; na kuhusu huduma zingine za Tigo, tafadhali piga namba 0713 800 800.
Tafadhali zingatia kwamba kuna vituo vya kuhudumia wateja wa Tigo kote Tanzania, unaweza kuona pahali zilipo kwenye tovuti ifuatayo: http://www.tigo.co.tz/customercare.php
Tafadhali tupatie namba yako ya simu ili tuwasiliane na wewe moja kwa moja.
Tigo inadhamiria kukupa huduma bora kwa bei nafuu kote Tanzania.
Asante kwa kuwa mteja wa Tigo.
Tigo
Binafsi Tigo wamenikwaza leo baada ya kuweka vocha ya dharura kama mida ya saa 4 na dakika chache usiku wa leo(27/2/2014
ReplyDelete.baada ya mda mfupi nikaanza kuinunulia bundle,nakuta wamekata salio.nikawapigia wakanieleza kuwa ati nilipiga simu.namba waliyonitajia nilipiga saa 3.44 usiku,na wakasema nikatuma msg,ambayo sijatuma.nilipoomba wacheki mda niliyoipiga hiyo namba,wakaomba nisubiri,na wakakata simu.juhudi kuwapigia ikaishia wanakata kila inapoita,hatimae akapokea dada mida ya saa 5.28 usiku.akasema(akadanganya) kuwa nilituma sms,namba aliyonitajia sina silka ya kutuma msg kitambo,kibaya zaidi,sikutuma hiyo msg.tigo wamekuwa washenzi na waizi kipumbavu mno.nimeshindwa kupiga simu ya muhimu na ni ya dharura,wamejaza customer care kutukera na kuhalalisha uizi wao bila haya.