Habari Ankal,

Mimi nina jambo nataka kujuzwa kidogo juu ya ustaarabu wa michango ya Harusi. Mtu akiwa katika harakati za kukusanya michango kabla ya harusi anakua anakutafuta sana na karibia kila week end unapata sms kuhusu kukumbushiwa kupunguza ama kutoa mchango wako wa harusi. 

Wengine wanakuuliza waufuate au wengine wanatoa namba za simu utume kwa M pesa au tigo pesa au hata bank account ukafanye deposit. 

Chaajabu ukishachanga tu, mawasiliano yanakwisha utashangaa siku moja kabla ya harusi unapokea text inayokuomba uwe mvumilivu eti kutokana na usambazaji kadi kuwa mgumu unaombwa uikute kadi yako getini siku ya harusi... wengine ukishawachangia wanauchuna na Harusi ikipita eti wanakutumia ujumbe wa kukushukuru kwa kufanikisha harusi yao..

 Jamani wadau huu ni ustaarabu wa wapi.. ama ndo wanatufundisha kuwa na roho mbaya na kutokuchangia harusi zao? 

Msaada kwenye tuta jamani...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Kwa kweli hii biashara ya kuchangishana harusi mimi inaniudhi sana basi tu. tena pale ambapo inakuwa kama mtu anakuforce umchangie sms na calls za kila mara.its pretty irritating to be honest.

    Kwa nini mtu asifanye kitu kidogo kulingana na uwezo wake badala ya kuchangisha ukoo mzima na marafiki ambao hata huwasiliani nao siku za kawaida?? wajulishe ndugu zako wa karibu kabisa na marafiki wa karibu kabisa kuwa unategemea kufunga ndoa na utashangaa mambo yatakavyoenda kiulaini.

    Pole mdau kama limekukuta hilo lakini its about time this thing should be changed.

    ReplyDelete
  2. Hii michango ya harusi kwakweli inachafua roho sana.Kwasababu kuna watu wanashida dunia hii na hawana msaada.Watoto hawana wazee na wengine wanamaradhi na hawana wadhamini wakuwatibu na wengine wanapoteza maisha.Kuna watoto hawaendi shule kwasababu wazee wao hawana uwezo wa kuwasomesha.Hizo pesa za harusi ni kwa siku moja tu.Acheni kuchanga labda kwa familia tu.

    ReplyDelete
  3. Mtu yuko kwenye mihangaiko ya harusi na wewe umeahidi kumchangia. Ni wajibu wake kufuatilia kwa karibu, na hiyo naona ni vizuri.

    Unataka baada ya kupokea mchango wako aendelee kukupigia simu au kukutumia sms za nini? Neno la shukrani linatosha kisha subiri kuhudhuria harusi. Kwanza kumbuka kuwa mhusika atakuwa amebanwa na maandalizi ya jambo hilo zito,

    Pia kama uko flexible na ulichanga kwa nia ya kumsaidia mhusika akamilishe ndoa yake, hutajali kuikuta kadi yako mlangoni.

    Tukishachanga tusiwe tena kero kwa wanaofanya maandalizi eti kwa sababu tu tumechanga. Muhimu kufanikisha jambo lililolengwa.

    ReplyDelete
  4. Muhimu kwanza ni kupata pesa sio kukupa kadi. Pesa ikishapatikana harusi itakuwepo ikiwa umepata kadi au hukupata.

    ReplyDelete
  5. Hili sidhani kama kweli ni la kuombea msaada kwenye tuta. Sisi wabongo bado tuna'complicate' mambo. Je, mhusika awafuate watu wangapi kuwapelekea kadi??? Kuna utaratibu mzuri wa kugawa kadi siku za vikao. Sasa unakuta wengine wanashindwa kuhudhuria kwa ajili ya uzembe au shughuli nyingine binafsi. Sioni ubaya wa kukuta kadi getini, ilimradi uwe umepewa taarifa kabla. Ujue siku ya harusi inapokaribia, mhusika huwa ana mambo mengi sana. Mimi nakumbuka wakati wa kuandaa harusi yangu, sikuweza kuchukua michango mingi kutoka kwa marafiki waliojifanya 'busy' na kunipigia simu kwenda kufuata mchango mwenyewe siku chache kabla ya harusi, mbali na kwamba nilikuwa nimewapa njia rahisi za kunifikishia mchango.

    Sasa ikiwa kweli unashindwa hata kufuata mchango siku za mwishoni, utapata muda wa kumpelekea kila mtu kadi yake, iwe nyumbani au ofisini?

    ReplyDelete
  6. Mochango ya harusi ni desturi mbaya tu kwa mwangalio wangu kwanini uchangiwe na wewe ndio unaowa haileti picha nzuri nikama yule mke au mume munamuowa watu mnaochangia desturi mbovu na mila mibovu!wazungu wanaowana wawili wakitoka hapo kila mtu anatumia mshahara wake kwa Hanimuni kama yuko na uwezo huna unaachana nayo pia!

    ReplyDelete
  7. Yaani we acha tu,maharusi naona siku hizi imekuwa deal,,kwani lazima mtu ufanye harusi ya kifahari,,kuchangisha watu mapesa na ukapa wa siku hizi jamani noma!.kwa nini mtu usione familia flan wanadhiki ukawachagishia pesa?au wewe ukasema naowa naomba mnichangie pesa ya kuanzia maisha na mke wangu!Huku ulaya hiyo ya kuchangia maharusi wanaishangaa sana,,,Ahlam UK

    ReplyDelete
  8. Tafadhari naomba mwenye akili timamu aache kuchangia harusi. kama unataka kuoa au kuoza, jiandae sawasawa. Nakumbuka nilipokuwa mdogo, watu wakitaka kuomba msaada wa harusi, walikuwa wakituma kikaratasi na kusema kwa adabunyingi kwa kihaya eti,"Ninshaba ontwele" tena huyo ni baba wa mtoto lakini mtoto mwenyewe ilikuwa mwiko kuomba mchango. mchango wenyewe ilikuwa mkungu wa ndizi, pombe, kuni hata mbuzi kama unayo. Je leo tunapewa sharti la mchango kuwa ni kiasi gani tena siyo pungufu ya kiasi fulani.

    Mimi nitachangia mgonjwa anayehitaji matibabu, mtoto aliyekosa ada au mama anayehitaji vifaa vya kupeleka clinic kama hana mme. NIMEMALIZA NAOMBA MICHANGO IKOME. JIKUNE UNAPOFIKIA ACHANA NA ULIMBUKENI.

    ReplyDelete
  9. Siasa za Ujamaa ndizo zinazotupa Umasikini.
    Nchi za kibepari hakuna kitu kinitwa Mchango wa Harusi..
    Utaandaa sherehe yako mwenyewe then waalikwa watatoa zawadi.

    Tubadilike Africa.. Usipokuwa na pesa za kufanya sherehe yako mwenyewe, unavumilia tu bila ya Kusumbua watu.

    ReplyDelete
  10. Ulichoombwa wewe n kuchanga siyo kutafutwa tena baada ya mchango wako elewa kuwa inawezekana ikawa siku ya sherehe ukawa ukumbi unachukuwa watu mia 200 na wachangaji ni mia 400 sasa yaya afanyaje? ni lazima panga lipite hapo na pengine waliopigwa panga mmoja wapo ndiyo wewe kwa hali hiyo hata wewe ungefanya hivyo kakaacha kulalamika angalia mbali.

    ReplyDelete
  11. MICHANGO YA HARUSI:::

    Ahsante mdau kwa kuanzisha mada muhimu sana ambayo inamgusa kila mmoja.

    Naomba nianze na dhana ya sherehe,
    Ni muhimu tufikirie sana kuwa unapo azimia suala lenye gharama kama sherehe halafu ukalikabidhi kwa walio karibu ni kuwa umewapa watu jukumu.

    Suala la muhimu kwa harusi ni ''NDOA TU'' na kilichobaki vitu kama sherehe ya harusi,send off,pati,kicheni pati, na zawadi ni ziada na sio muhimu.

    Itafaa muhusika mkuu kama anataka sherehe aanze yeye binafsi kuwajibika na pia asilazimishe watu kwa kuwa kila mmoja na nafasi yake!

    ReplyDelete
  12. Mie nimeudhuria harusi chache saana bongo. Ya mwisho ni ya Bro mdogo tarehe 14 November. Michango yote ilitokana na "PLEDGES" zilizotolewa na watu wenyewe (wengi wao walikaribishwa ktk kikao cha kwanza cha taarifa au sie wa ughaibuni tulishiriki kwa skype). Kwenye kikao hicho cha kwanza, iliundwa kamati na hapo hapo waliamua kuwa michango yote chini ya kiwango kadhaa basi hawatakuwa na right za automatic kupewa kadi (ila wanaweza kualikwa na wenyeji na kupewa kadi za ziada).
    Muhimu: Wengi waliotoa pledges ni ndugu, marafiki au tuseme watu wa karibu. Hakuwepo mtu wa mtaani pale.
    Hivyo wanakamati walipoanza kufuatilia michango, walikuwa wanafuatilia zile ahadi ulizotoa wewe mwenyewe bila kulazimwishwa.
    Na kwa kesi yetu, wote waliotoa michango walikaribishwa ktk harusi (wengine mara mbili-kwenye send off Golden Tulip na ya kwetu Movenpick).
    Maoni yangu kuwa tunapochukua jukumu basi tulitimilishe kama ipasavyo. Vitu hivi vinaendana: bila pesa kadi hazipatikani. Yaani pledges tuziwakilishe mapema na kadi tuzigawe on time.
    Ni swala lingine kuwa mamilioni yanatumika kama show offs, lakini hilo sio swala la Mdau kwa Uncle....
    Naomba kuwakilisha. Blackmpingo

    ReplyDelete
  13. Wadau, tatizo Waoaji wa sasa Makachala na Waoleaji Micharuko!!!.

    Unakuta mtu anakurupuka hajajiandaa kimaisha anataka kuoa au kuolewa tena kwa sherehe ya kifahari ya gharama kubwa kulipiwa na wengine!!!.

    Upande wa pili watu wengine walio na chochote na wenye uchu wa starehe wanashinikiza michango kwa nia ya kupata pesa nyingi na kuwa na tafrija kubwa ya kulewa na ufahari!!!

    Kama hawana akili vile, huku wanandoa hawana maandalizi yeyote kimaisha!.

    Michango imefanywa kwa ufanisi na kiasi kizuri cha pesa kimekusanywa sawa, si bora wangefanya tafrija ya kawaida na kuacha kiasi kidogo cha makusanyo kiwape Msingi au Mtaji wa Maisha wanandoa kuanzia maisha?

    ReplyDelete
  14. Hahaha pana mziki mpya wa Kizazi kipya jamaa ameitisha michango ya harusi amekusanya pesa kibao, mwishowe harusi ikafanyika chini ya mwembe bila kuwapeleka ukumbini kwa pati na vinywaji jamaa wankuja juu warudishiwe pesa zao!!!!

    ReplyDelete
  15. Shirika la maendeleo la Marekani USAID waliwahi kufanya utafiti jinsi wananchi Duniani wanavyo changia ktk masuala mbalimbali ya jamii,,,
    TAARIFA YA UTAFITI KWA NCHI 3 ZA AFRIKA MASHARIKI ZA WAKATI HUO:
    Ilionekana matokeo haya kwa nchi nini wanajali na kipi hawajali,


    1.TANZANIA-(WANAJALI sherehe,harusi,ngoma,jando,unyago-HAWAJALI elimu,matibabu,maendeleo ya jamii kila kitu wanasubiri serikali)

    2.KENYA-(WANAJALI wanafanya Harambee kwa,elimu,misiba,maendeleo,mifuko ya akiba na uwekezaji-HAWAJALI harusi,ngoma,sherehe na matumizi mabovu)

    3.UGANDA-(WANAJALI tambiko, utamaduni,mizimu, elimu na akiba ya uwekezaji-HAWAJALI harusi, na sherehe zisizo na tija)

    Kwa ujumla ktk Afrika ya Mashariki ya nchi 3 za mwanzo sisi Tanzania ndio tunajali zaidi michango kwa minajili ya matumizi yasiyo endelevu kama harusi zisizo na malengo!

    ReplyDelete
  16. Unakuta unashinikizwa kuchangia Harusi ukikataa au ukiwatolea nje ,unanyooshewa kidole,unalaumiwa,unasemwa vibaya au unatishiwa kutengwa!

    Sasa basi kwa nini wasijiulize wao wahusika muoaji na muolewaji wamejiandaa vipi??? sio wanakurupuka tu kutaka kuoana tena kwa harusi ya hadhi ya juu wakati wanajua pana gharama!

    ReplyDelete
  17. Tutabaki masikini hivihivi tu tukiendelea kuchangia harusi na misiba na kuacha kuchangia elimu na afya. Ukiomba mchango umepungikiwa dad hakuna hata mmoja atakusaidia lakin lakini ukiomba kuchangiwa harusi basi watu watachanga kwa sababu wanajua watakuja kula na kunywa siku ya harusi. Vile vile ukiwa taabani hospitali ukaomba kusaidiwa hata baadhi ya ndugu zako hawakusaidii ila ikishakufa ndo watu wanatoa michango kibaaaaao! Lazima tubadilike na haya mambo ya harusi yabaki kuchangishana kifamilia zaidi. Nafikiri hata ndoa nyingi hazidumu zikichangiwa na kwamba mtu hajui machungu ya kugharimia ndoa kwani kutokana na michango kuwa mingi alibaki na chenji kama faida. Lakini mtu aliyegharamia harusi lazima aiheshimu. Kuna ndoa nyingi sana zinakufa kabla hata anivesary ya kwanza haijafika.

    ReplyDelete
  18. Kama ulitoa ahadi ni lazima uitimize na kama uliona hutaweza kumchangia ungemweleza kwamba hutachanga.Maana siku hizi walio wengi kabla ya kukupa card ya mchango huwa wanakuuliza kwamba nina harusi na je nikuletee card utanichangia?Sasa kama ulisema utamchangia kwanini uone kero wakati anakukumbusha ahadi yako uliyompa?Kitu kingine harusi nyingi siku hizi kunakuwa na kiwango cha chini cha kuchanga na sio wote wanaliweka hilo wazi,sasa inawezekana wewe hukupewa card ya mwaliko kwa kuwa hukufikia kile kiwango cha chini cha mchango ndo maana baada ya harusi unaletewa text msg ya shukrani kwa kufanikisha harusi yao!Jambo lingine ni kwamba mchango wenyewe unatoa kiduchu na last minutes kiasi kwamba watu wankuwa bizzy kumalizia mandalizi na ndo maana unakosa hata mtu wa kukupa maelezo kwamba kiasi ulichotoa ni cha kupewa asante kwa kutuchangia!

    ReplyDelete
  19. Hii tabia ya kuchangishana ililetwa na ndugu zetu wachaga. Ona sasa ilivyookuwa kero!

    ReplyDelete
  20. Sioni sababu ya kuikuza shughuli wakati uwezo hakuna,,,fanya kitu kulingana na uwezo wako binafsi ila jamii yetu ni sikivu ukipungukiwa omba utasikilizwa na sio kulazimisha watu mchango!

    Tatizo la kukuza kitu ni kuwa ,muolewaji akiona shughuli ni ya kifahari ataona amepata mume tajiri na mwenye uwezo akifika ktk nyumba atataka maisha kilingana na ilivyokuwa harusi ya kifahari,,,kumbe lahaula!!! jamaa kazi yake ni MFYATUA MATOFALI au DEREVA WA BODA BODA, ndio maana ndoa zinavunjika haraka!

    ReplyDelete
  21. Nilishawahi kusikia maongezi ya Shemeji wa jamaa mmoja yaani mke wa kaka yake jamaa ambae ameoa karibuni sio zaidi ya wiki mbili,,,mume anapitisha bakuli kwa kaka yake akiomba msaada wa maisha akale na mkewe mpya,,,hii ni taswira ya kukurupukia ndoa na harusi ya kifahari bila maandalizi ya kukabiliana na maisha!

    ReplyDelete
  22. Ni busara wanandoa wakajipanga kwanza kabla ya kugeukia kwa wachangiaji, kwa kuwa ni utamaduni wetu kupeana hisani kwa michango ktk mashughuli yetu, atakaye taka akaribishwe kutoa kama sehemu ya kushiriki na sio kulazimishwa michango!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...