Mtandao wa Wanataaluma Tanzania umemtunuku nishani maalum Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere katika kongamano la wanataaluma hao leo kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam. Pichani, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, akikabidhi tuzo hiyo kwa mtoto wa Malimu, Makongoro Nyerere wakati wa kongamano hilo. Kulia ni Rais wa Mtandao huo, Phares Magesa.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara, Makongoro Nyerere ambaye ni mtoto wa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Nyerere akimuonyesha tuzo hiyo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Nape Nnauye. Kulia ni Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) John Mnyika.
"Ukosefu wa ajira kwa wasomi husababisha baadhi yao kushawishiwa kwa urahisi kushiriki maandamano" Waziri wa Maliasili na Utalii Ezekiel Maige (kushoto) akisema maneno hayo wakazi akizungumza na Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) John Mnyika (kulia), Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara Makongoro Nyerere na Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Katibu wa NEC ya CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) John Mnyika katika kongamano la Mtandao wa Wanataaluma Tanzania lililofanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam. Katika kongamano hilo Nape na Mnyika wametoa mada 'Uzalendo na Utaifa'.
Makamu kuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Profesa Tolly Mbwete akijadili jambo na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa na Rais wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania, Phares Magesa, wakati wa kongamano la wana taaluma hao kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam. (Picha zote na Bashir Nkoromo)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. KAKA MAKO, OYEEEEEE, hakuna kama Mwalimu Tanzania nzima, Mungu azidi kumlaza mahali pema peponi amina.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...