Robo fainali ya michuano ya 35 ya Kombe la CECAFA Tusker Challenge inaanza kesho (Desemba 5 mwaka huu) kwa mechi mbili zitakazochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mechi ya kwanza itakayochezwa saa 8.00 mchana itazikutanisha Burundi na Sudan wakati ya pili itakayoanza saa 10.00 jioni itakuwa kati ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) dhidi ya Rwanda.
Keshokutwa (Desemba 6 mwaka huu) mechi ya kwanza ya robo fainali itakuwa kati ya Uganda na Zimbabwe wakati ya pili itakayoanza saa 10.00 jioni itawakutanisha mabingwa watetezi Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) na Malawi (The Flames). Mechi zote zitaoneshwa moja kwa moja kupitia SuperSport 9.
Viingilio kwa mechi zote za robo fainali ni sh. 2,000 kwa viti vya kijani na bluu, sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B na sh. 15,000 kwa VIP A.
Boniface Wambura
Media Officer
Tanzania Football Federation (TFF)
Member, CECAFA Media Commitee
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...