Hapana shaka  umesheherekea salama miaka 50 ya uhuru.
 
Mwaka jana nilipata nafasi ya kuhudhuria kozi fupi ya uandishi habari nchini Mexico. Mbali na kitabu pia ilikuwa ni nafasi ya kusafisha macho kwenye taifa hilo.
Machi mwakani yatafanyika mafunzo hayo tena. Shule imenipa nafasi tena na la kutia moyo zaidi nitakuwa mmoja wa watakaowasilisha mada. 
Fuata hiyo link hapo chini, ipitie kwa makini. Ukiona unafiti, usisubiri. Omba nafasi chapchap.

Kama una swali lolote tafadhali wasilina nao (email ad yao hapo chini) au niulize haraka iwezekanavyo.

Regards,
 
Nathan Mpangala,
(Political Cartoonist),
Mobile 0713 262 902
Dar es Salaam.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Natamani hii ndio ingekuwa Spirit ya Wabongo wote. ukimpa pande mwenzako na wewe Mwenyezimungu anakupa zaidi. Kijasti Mungu akuongezee.

    Mdau Maganga

    ReplyDelete
  2. Mdau Nathan Mpangala, ahsante kwa salam za kusherehekea Uhuru wetu pia ahsante kwa kuwa na moyo wa wengi wape nafasi na uwezekano kwa faida yetu sote!

    ReplyDelete
  3. Wadau tungepata watu zaidi ,na zaidi na zaidi hadi ktk safu ya uongozi wetu wenye moyo na roho kama Mdau Nathan Mpangala kwa kweli tungefika mbali sana!...NATHAN MPANGALA MUNGU AKUBARIKI!

    ReplyDelete
  4. Ushamba tu ndo tatizo..Eti Mexico kuosha macho!

    ReplyDelete
  5. Wewe Mdau wa nne-4 hapo juu...Ushamba tu ndo tatizo..Eti Mexico kuosha macho! wa Sat Dec 10, 11:38:00 AM 2011

    Watu kama ninyi ndio wazamiaji mnaposafiri nchi za nje kama Marekani na Ulaya, wewe huchukulii kile kinachopatikana baada ya kuhudhuria mpango huo Mexico bali unaangalia ni aina gani ya nchi mtu anayokwenda.

    Ninyi ndio mnasababisha Balozi nyingi sasa zinasumbua na zinanyima sana watu viza kwa kuhofia watu wasio safiri kwa lengo la kweli kama wewe.

    Bado una mawazo ya kizamani ya kwenda kuishi nje ya nchi wakati hali ya kiuchumi Dunia nzima ni ngumu, sio siri jamaa nje wanaficha kuna watu nchi zingine wanafanya kazi za vibarua kwa kubeba maboski madukani, na kuvuna matunda mashambani, baada ya Ulaya na Marekani kufilisika kwa mtikisiko wa Fedha na Uchumi.

    Nathan Mpangala hajatoa tangazo kuwalenga watu kama wewe Wazamiaji wa safari za nje, amelenga watu wanaotafuta Uelewa kufuatia ushiriki na kuhudhuria ktk mipango mbalimbali ya mafunzo!

    ReplyDelete
  6. Hasante Kaka Nathan, nadhani tungepata watu kumi kama wewe nchini, basi mambo yangekuwa mswano, ...ila watanzania hatuna tabia ya kupendana, na ndo maana kamwe hatuji kuendelea, ubinafsi mwingiiiiii

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...