Mambo vipi Ankal,

Natumai ni mzima wa afya na unaendelea vyema na libeneke.

Mie ni Mkazi wa eneo la Mwanagati, Kitunda, Dar es salaam ambapo barabara yetu huku imeharibika vibaya sana baada ya mvua kubwa iliyonyesha hivi majuzi na kuweza kutafuna njia zote na kubakia vipande,hali inayopelekea magari kupita moja moja huku upande mwingine ikisubiria lipite jingine na kufanya msongamano mkubwa. 

hivyo kupitia Libeneke la Globu ya Jamii tunaomba tufikishie ujumbe wetu wa kuhitaji msaada sie wananchi wa huku Mwanagati,Kitunda ili mambo yawe mswano kama ilivyokuwa awali.

ahsante sana na lidumu Libeneke la Globu ya Jamii.

Mdau wa Mwanagati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Ma Profesa wa kibongo wako wapi au kazi yao ni unafiki tu?

    ReplyDelete
  2. Hongera Mdau kwa kuweka hiyo kero kwa sisi wakazi wa Mwanagati nashindwa kuelewa diwani na hao viongozi wengine wa serikali ya mtaa kama wapo kweli!!!

    ReplyDelete
  3. Kwa hiyo maprofessor wafanye nn!?...peleka mawazo mafupi kule kama huna cha kucomment!

    ReplyDelete
  4. Hivi kweli hiyo waweza kuiita barabara? Mbona imejengwa kwa kiwango kibovu kabisa, you can't even dare to call it a tamarack road

    ReplyDelete
  5. Pigeni mchango faster mtengeneze wenyewe. Mtasubiri serikali hadi lini? Mbona harusi mnachangia sana, mnashindwa kuchangia barabara kwa maendeleo yenu? Nitawashangaa sana kama mtashindwa kuchangia swala la maendeleo kama ukarabati wa barabara. Halafu kutwa mnachangia sherehe! Mtakuwa wajinga sana!

    ReplyDelete
  6. Watanzania wazembe kweli,hivi mnataka Serikali ije hata kuwapanga jinsi ya kuzuia huo mmonyoko? Mlishindwa hata kupata viroba vya mchanga mkaweka na kuweka mifereji ili maji yasiendelee kuleta uharibifu? Endeleeni na malalamiko na deko zenu shida ikiwazidia mtapata akili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...