Bendi ya muziki wa dansi Ngoma Africa band aka FFU yenye makao yake Ujerumani, Inaungana na watanzania wote kwa kutoa pole na salam za rambi rambi kwa wahangwawaliopatwa na maafa ya mafuriko ya maji mkoa wa Dar-es-salaam.Maafa hayo yalisababishwa na mvua kubwa,yamepoteza maisha ya watu na kusababisha uharibifu mkubwa wa makazi ya jamii na mali zao,pamoja na barabara mkoani Dar-es-salaam. Tunaotoa pole kwa wahangwa wote,Mwenyezi Mungu atupe uvumilivu na mshikamano katika kipindi hiki kigumu.

Umoja ni Nguvu
www.ngoma-africa.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. HAWA FFU BADO TOURIST VISA YAO IPO VALID?..WAZALENDO KAMA NYINYI SITOFURAHI KUJA KUWASIKIA MUKIJITAMBULISHA KAMA WAKONGO AU WABURUNDI...TEHE TEHE.
    HAPPY NEW YEAR

    ReplyDelete
  2. NGOMA AFRIKA BAND WAKIWA HUKO UJERUMANI, WANAJITAMBUA KULINGANA NA AINA YA SANAA WANAYOWAKILISHA,,,NA INGEFAA WAENDELEE KUJIHESHIMU KAMA WAAFRIKA WATANZANIA,,,CHA MSINGI WAFUATE TARATIBU ZA VIBALI VYA SHUGHULI ZAO HUKO.

    Kwa vile Dunia ya sasa kama una msimamo hakuna sababu ya kujikabidhi UKIMBIZI wakati hiyo biashara ni ngumu sana kwa sasa kulingana na hao Wafadhili nchi za Ulya na Marekani kifedha na kiuchumi zilivyo filisika!

    ReplyDelete
  3. Ngoma Afrika Band, la muhimu ni kufuata taratibu tu za ufanyaji kazi wao wakiwa huko Ujerumani.

    Kama watataka kuendelea na shughuli zao ni kufuata taratibu za vibali za huko Ujerumani na sio sisi kuwakadiria wao kurudi Tanzania wakati matashi yao yanawapelekea kuendelea na kazi huko.

    Mbona pana wageni wengi nchini wakiwemo hao hao Wajerumani wanakuja na viza za Utalii lakini wanakuwa na matashi ya kuendela kukaa nchini na kufanya shughuli zao, wanafuata taratibu na wanakaa, sembuse ije kuwa Ngoma Afrika Band huko Ujerumani?

    ReplyDelete
  4. Jambo lingine uwepo wao Ngoma Afrika Band huko Ujerumani ndio unaleta tija zaidi kwa kuwa mwenendo wa sanaa yao ni Utamaduni wetu kwa hivyo ndio nafasi zaidi ya kuutangaza Utamaduni wetu wa Tanzania Waafrika huko Ujerumani na Ulaya nzima!

    ReplyDelete
  5. NGOMA AFRICA BAND AKA FFU,kutokana na na utafiti nilionao mbona wakuu wa kazi hao wana vibali vyote halali vya kuishi nchini Ujerumani,vibali ambavyo ni vya kudumu, Parmanent resident Permit,(Unbefrisetet) vibali ambavyo vinawaruhusu kuishi katika nchi yoyote ya jumuhia ya ulaya,kwa hili nawapa hongera sana,ila kazi ipo kwa wanamziki wafrika wanaotaka kuvamia soko la ulaya,upatikanaji wa Visa na vibali umekua mgumu,FFU endeleeni kutuwakilisha

    ReplyDelete
  6. Kamanda na kikosi chako,tukukubali kuwa ni mpiganaji wa kweli unayejitoa muhanga kwa kuitangaza miziki ya kiafrika,wato maoni wengi wa juu ni watu wa kijicho na wanafiki wasiotakia nchi mema

    ReplyDelete
  7. kamanda mkuu ras makunja na kikosi chake ffu,naona ni wanamuziki waliostukia soko la nje tangu mwishoni mwa miaka ya 80s,kwa hili jamaa wanastaili pongezi,kwa wakati huu mgumu jumuiya ya ulaya inafirisika na wageni wanachukiwa ulaya,Ngoma Africa band aka ffu au watoto wa mbwa,ngome yao imekuwa kubwa.kamanda zidisha mwendo wa kasi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...