Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum CCM kutoka Mkoa wa Ruvuma alipata fursa ya kutembelea banda la Mkoa huo wa nyumbani na kujionea shughuli mbalimbali katika Banda hilo. Pichani akikabidhi zawadi ya Samaki aina ya Mikebuka kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kupitia kwa Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo Ndugu Revocatus Kassimba.
Alitembelea pia banda la Kagera na kujionea hatua kubwa iliyopigwa na Mkoa huo katika kutengeneza kahawa kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi.
Mhe. Eng. Stella Manyanya (MB) Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akijaribisha Kata ya kunywea Maji iliyokuwa ikitumika katika kipindi cha nyuma.Wakati huu tunapoadhimisha Mika 50 ya Uhuru vifaa hivyo vimekuwa havitumiki tena kutokana na Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.
Miongoni mwa bidhaa zinazopatikana katika Banda la Rukwa ni Samaki wazuri kwa Lishe aina ya Mikebuka kutoka Ziwa Tanganyika. Hapo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akitoa zawadi ya samaki hao kwa watoto waliotembelea banda hilo la Rukwa na wazazi wao.
Aliingia kazini na kutoa maagizo kwa Wataalamu wa Mipango Miji katika banda hilo la Rukwa kwa kuwaagiza kutenga maeneo maalum yasiyopungua hekari tatu kwa kila Wilaya kwa ajili ya Ujenzi wa Vituo vya kuhifadhia mambo ya Utamaduni (Makumbusho) katika kipindi cha mwezi huu wa Desemba kabla ya tamko rasmi la Mhe. Rais la kuanzisha Mkoa mpya wa Katavi.
Mtaalamu wa Mifugo Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa Bw. Respitch Maengo akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kitabu cha Mkoa huo cha Mafanikio ya Miaka 50 ya Uhuru. Kitabu hicho kinaelezea Mafanikio yaliyopatakana katika Mkoa wa Rukwa kwa kipindi cha Miaka 50 ya Uhuru kwa kila sekta. Kitabu hicho kinapatikana bure katika banda hilo na katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...