Wana CCM UK na Watanzania nchini Uingereza tumepokea kwa huzuni kubwa habari za mafuriko makubwa yaliyosababishwa na mvua zilizoanza kunyesha Jumanne ya Desemba 20, 2011 na kusababisha athari za kijamii jijini Dar es salaam.
Kwa majonzi mazito tunaungana na Watanzania wote kuwapa faraja wale wote waliopoteza wapendwa wao, kuwaombea huduma na nafuu ya haraka majeruhi na kuwatia moyo wa ujasiri wote waliopoteza mali zao katika janga hili la mafuriko.
Aidha tunawashukuru na kuwapongeza Rais na mamlaka za serikali, asasi binafsi na wananchi kwa kujituma kwa haraka kusaidia kuokoa maisha ya watu na kupunguza athari zaidi kwa wahanga wa mafuriko haya.
WanaCCM UK tunaamini kuwa hakuna kifo cha Mtanzania yeyote ambacho ni kidogo au cha idadi ndogo. Vifo vilivyotokea katika mafuriko haya ni maafa ya kitaifa na kimeuguza mioyo yetu.
Tunatarajia mamlaka zote zinazohusika na mipango miji, makazi na usalama wa wananchi zitapokea salaam za faraja za Rais Jakaya Kikwete kwa wahanga wa mafuriko kuwa ni AGIZO KAMILI na kwamba watahakikisha makazi yote ya bondeni na athari ambatano zinakoma kwa kupatiwa suluhisho la kudumu.
WanaCCM UK tunawaomba Watanzania wanaoishi kwenye maeneo/mabonde yenye tahadhari watumie haki yao ya msingi kushirikiana na Serikali ili wapatiwe Makazi Bora yenye hifadhi ya Kudumu.
Nasi Watanzania wote nje ya Nchi, kama ilivyo ada kwetu, tuendelee kushikamana na tuwachangie Misaada ya Kibinadamu ndugu zetu wahanga wa mafuriko nyumbani Tanzania.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Imeandaliwa na CHAMA CHA MAPINDUZI.
TAWI LA UNITED KINGDOM.
22 DESEMBA, 2011.



Wataalamu wa BAKITA wametwambia tusitumie neno "Wahanga" badala yake tutumie "WAATHIRIKA".
ReplyDeleteNatumai sote tutajirekebisha.
WANA CCM-UK KWA PAMOJA NA SISI HUKU NYUMBANI TANZANIA, tuseme ''KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI''
ReplyDeleteNatuwaenzi ndugu zetu waliopata maafa na Waathirika wa janga!
Janga la mafuriko ni pigo kwa taifa na tunatowa rambi rambi kwa wale wote walio athirika. Pia ni somo kwa Taifa iwapo lina jali maisha ya raia wake, kuweza kuweka mipango mizuri ya makaazi kwa kuangalia kipato halisi cha Mtanzania. Shirika la nyumba two bedroom flat 60m Tsh. Sasa muda umefika kwa walala hoi kuvaa gamba watalovuwa wakubwa.
ReplyDeleteAhsante kwa angalizo la wataalam wa BAKITA. Tuelewe mjengo na ufinyanzi wa lugha huihushwa toka vyanzo shirikishi au tegemezi kutokana na asili ya matendo. Kazi ya BAKITA ni kuyakinisha ili yakidhi mahitaji ya wakati.
ReplyDeleteNeno "U/M/WAHANGA" linaweza kufafanuliwa toka unyambulisho tegemezi na kuleta maana zinazokaribiana au tofauti kulingana na chanzo cha tukio.
Sasa WAHANGA wanaweza kuwa:
1. "wale" waliojitolea maisha yao kwa kutambua na kufa ili kukidhi haja ya kukataa au kuunga mkono shauri la wakati.
See: Wahanga means Martyrs. Au
2. "wale" ambao maisha yao yameathiriwa/kupotea kutokana tukio ambalo halikutegewa.
See: Wahanga wa Mafuriko means Victims of floods. Hizi tafsiri sio lazima ziwe rasmi.
La msingi hapa ni nani mwathirika moja kwa moja wa TUKIO la kwanza na pia nani ni mwathirika baada ya tukio la shauri la kwanza.....
Tafadhali pokea pendekezo langu pia na tuendelee kuwa wanafunzi wa lugha mama kiswahili.Tuna imani na BAKITA
OWINO.