Ndugu zetu Watanzania,
Jumuiya ya watanzania waishio hapa nchini Malaysia imepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa sana habari za janga la mafuriko yaliotokea maeneo mbalimbali nchini kwetu Dar es Salaam na kwingineko. Tunapenda kuungana na watanzania wengine katika kutoa salamu zetu za pole kwa ndugu jamaa na marafiki wote walioathirika katika majanga haya. Tunawapa pole wale wote ambao wamepoteza ndugu zao, jamaa na marafiki katika janga hili, Tunamwomba mweneyezi MUNGU azipokee roho za marehemu wote mahali pema peponi na wapumzike kwa amani - AMINA
Tunawapa pole wale wote waliopoteza makazi yao pamoja na thamanai mbalimbali zilizokuwapo katika makazi yao tunamwomba mweneyezi MUNGU awape faraja na uvumulivu mkubwa katika kukabiliana na kipindi hichi kigumu. Aidhatunapenda kuwapongeza wale wote ambao kwa namna moja au nyingine wamejitolea kwa hali na mali katika kuokoa maisha ya ndugu zetu na kuwapa hifadhi ya makazi wale waliopoteza makazi yao. Tuendeleeni kudumisha moyo wa upendo amani na mshikamano wa dhati kusaidiana katika kipindi hiki kigumu.
Tunapenda kutoa wito kwa serikali yetu hususani ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa kuchukua hatua za dharura na haraka katika kukabiliana na magonwa ya milipuko yanayoweza kutokea kutokana na mafuriko haya. Tunamwomba mwenezi MUNGU atufariji sote na tuwe na mshikamano katika kipindi hiki kigumu.
Tunapenda kuchukua fursa hii kutoa ushauri wa dhati kwa serikali kutumia vyombo vyake ikiwemo idara ya utabiri wa hali ya hewa katika kutambua na kutoa tahadhari mapema kuhusiana na majanga ili kuepuka maafa kama haya yasijirudie wakati mwingine katika nchi yetu, wizara ya ardhi ikishirikiana na halmashauri na manispaa mbalimbali kote nchini ziwezeshwe kutimiza majukumu yao kwa kusimamia vema ujenzi wa makazi ya watu katika maeneo ambayo ni salama na sio kuruhusu ujenzi holela katika maeneo ambayo sio salama kwa makazi ya watu.
MUNGU IBARIKI AFRIKA NA MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Hivi kwa nini kila X-mass balaa hizi?
ReplyDeleteSerikali, nafikiri ahadi ya kuwapatia makazi salama imetoka kwa wahusika kupewa viwanja sehemu zingine.
ReplyDeleteSasa kwa kuwa wahanga wapo ktk makazi ya muda madarasa ya shule kadhaa huu ni muda mwafaka wa kupitisha trekta na kuharibu kabisa makazi hatari ya mabondeni kwa maisha ya binadamu ili tuwe na lengo jipya!
INAWEZEKANA MAJI YAKIPUNGUA WATAANZA KURUDI KULE TENA!
Hawa jamaa wakazi wa mabondeni wana asili ya ubishi na umjini mjini sana......baada ya kuvunjiwa,,,,,,mpango mzima ni kuwapimia viwanja MBAGALA na kwingineko na kuwawekea mahema ya muda huko ili wayatumie wakati wanajenga.
ReplyDelete