Kamati ya maandalizi ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania nchini Netherlands, inaomba kuchukua nafasi hii kuwakaribisha wa Tanzania wote kuhudhuria sherehe hizo mnamo siku ya tarehe 10 Desemba 2011. Sherehe zitafanyika kwenye ukumbi wa Mundial ,Bleijenburg 11, 2511 VC mjini The Hague (Den Haag) kuanzia saa nane mchana mpaka saa tano usiku.
Ili kufanikisha shughuli za maandalizi, kamati inawaomba wale wote watakaopenda kuhudhuria wajiandikishe kwa kutuma majina yao
kwenye email address kamati50@googlegroups.com.
Asanteni na karibuni nyote.
Bulemo Francis Kweba
Mwenyekiti, Tanzania Association in the Netherlands (TANE)
uhuru wa tanganyika sio wa Tanzania.....wacheni ujinga huo wa kuwapoteza wenzenu.
ReplyDeleteSasa kwani Tanganyika sio sehemu ya Tanzania. Nikupe mfano mzuri Marekani wanasherekea uhuru wao mwaka 1776. Huo uhuru ulijumuisha majimbo 13 kati ya majimbo 50 yaliyopo. Inachomaanisha ni kuwa huo ndio ulikuwa ni mwanzo wa Tanzania uijuayo leo hii
ReplyDeletecomments za kipuuzi mara nyingi zinatoa huko ulaya kwa wakimbizi,baadhi ya wenzetu wamepumbaa akili kazi yao kukosoa wasilolijua badala ya kudiscus ya maana.Ndg zangu wa holland na uk badilikeni mnachokimudu ni umbeya mkiongozwa na gwiji la umbeya bint KABILA.
ReplyDeleteAnonymous wa pili kutoka juu umefanya kazi nzuri ya maelekezo: SEMINA HII IWAFIKIE WA ZANZIBAR WOTE NA WANAOJIITA WATANGANYIKA AMBAO NI WAGUMU KUJITAMBUA JUU YA DHANA HII...uhusiano kati ya Tanzania ya leo Zanzibar na Tanganyika.
ReplyDeleteMFANO WA PILI UNAWEZA KUZALIWA UKAPEWA JINA LA UNGO (LA UTOTO),,,HALAFU MTU HUYO HUYO BAADAE UKAPEWA JINA LA UKUBWA LABDA BAADA YA KUTAHIRIWA,KUVUNJA UNGO/ KUCHEZWA,KUBATIZWA, KUOA/KUOLEWA AU KUPATA MTOTO!
Sasa basi, endapo utamkuta mtu ktk zile jamii ambazo pana majina baada ya kutahiriwa,kuoa,kupata mtoto ukimwita jina la kabla ya kutahiriwa,kuoa,kupata mtoto (la zamani)atachukia na ataona umemdharau!
Wadau wa Pili, wa tatu na wa nne kutoka juu Pongezi sana kwa kumwelimisha Mdau wa kwanza ambae anawakilisha mamia kwa maelfu ya watu wenye akili finyu!....WAZANZIBAR ASILIA na WATANGANYIKA, pamoja na mamia kwa maelfu ya WASAFIRI AMBAO/ WAMEKWAMA NJE YA NCHI au WANAOOMBA UKIMBIZI HAWAJAFANIKIWA WANASUBIRIA na waliopata kwa muda UKIMBIZI huko Ughaibuni!
ReplyDelete__________________________________
HAIWEZEKANI MFANO TANZANIA YETU TUPO 45 MIL. KILA MTU KUWA NA AKILI, MINGI INAKUWA NI MINDONDO!
KUWA NA AKILI SIO KITU CHA MCHEZO NI MAJAALIWA YA WACHACHE NDIO MUNGU ALIVYOPANGA!
Hawa wenye mawazo ''mgando'' ambao wengi wao wapo nje ya nchi...hawa watu kiasili sio jasiri wa kukabiliana na maisha wamekimbia nchi.
ReplyDeleteKukimbia kwao ni sawa na mtu ukajificha mvua ya masika chini ya mti wa mwembe ambapo baada ya muda anajikuta umelowa.
UKIMBIZI:
1.Ni hadhi ya muda tu, na mara nyingi hufikia kikomo na watu wakarudishwa makwao au wakakatiwa msaada.
2.Kwa hali ya sasa ya matatizo ya kiuchumi duniani watu wajaribu kubadilika hata hizo serikali za huruma huko zitakuwa na roho mbaya na hawatakuwa wanafikiria watu tena.
3.Ni fedheha mtu ukuwa na akili zako timamu ukaondoka nchini kwako Tanzania ukawa unakula bure na kutunzwa Ugenini kama taahira na kwa saikolojia hii ndio utakuta wanachangia mawazo ''mgando''