Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akimkaribisha ofisini kwake balozi wa Pakistan nchini Tanzania Tajammul Altaf mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Bunge leo jijini Dar es salaam.
Balozi wa Pakistan nchini Tanzania Tajammul Altaf (kushoto) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda (kulia) wakizungumzia masuala mbalimbali kuhusu uendelezaji na uimarishaji wa ushirikiano kati ya Tanzania na Pakistan katika Nyanja za elimu, Biashara, wataalam na ubadilishanaji wa uzoefu kuhusu shughuli za Bunge leo jijini Dar es salaam.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akitoa ufafanuzi kwa balozi wa Pakistan nchini Tanzania Tajammul Altaf kuhusu Zawadi ya saa aliyomuandalia balozi huyo yenye kumbukumbu ya picha za historia za maspika wa Bunge waliopita toka mwaka 1953 mpaka sasa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda (kushoto) akizungumza na ugeni kutoka nchini Canada uliomtembelea leo Ofisini kwake jijini Dar es salaam ukiongozwa na mbunge kutoka Bunge la Canada Mhe. Deepak Obhrai (katikati).
Mbunge kutoka bunge la Canada Mhe. Deepak Obhrai akimsikiliza kwa makini Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda mara baada ya kumtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...