Taifa limeondokewa na Msanii maarufu Bw. Lawrence Hinju (Pichani) ambaye kwa miaka mingi amekuwa mahiri katika kuandaa halaiki mbalimbali za maadhimisho na sherehe za kitaifa.

Bw. Hinju amefariki usiku wa kuamkia siku ya Alhamisi Tarehe 07/12/2011 nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Marehemu alianza kuugua Kifua wiki tatu zilizopita akiwa Uwanja wa Uhuru kwenye maandalizi ya Halaiki ya watoto kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

Mbali na ubobezi katika kuandaa halaiki hizo za matukio ya kitaifa, Marehemu alikuwa Mwajiliwa wa Baraza la Sanaa la Taifa toka Tarehe 01/07/1988 hadi mauti yalipomfika.

Aidha, Marehemu Lawrence Hinju aliteuliwa kuwa mjumbe wa Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa kuanzia mwaka 2005 hadi sasa.

Kwa niaba ya Baraza la Sanaa la Taifa, wasanii na wadau wa Sanaa hasa katika upande wa Sanaa za Ufundi, tunatoa pole kwa wote walioguswa na msiba huu.

Ni wazi pengo lililoachwa na Marehemu halitaweza kuzibika kamwe kwani amekuwa nguzo muhimu katika kufanikisha sherehe mbalimbali za kitaifa.

Mwili wa Marehemu unatarajiwa kusafirishwa Siku ya Jumamosi Tarehe 10/12/2011 kwenda kuzikwa nyumbani kwao Mkoani Ruvuma. Taratibu za usafiri zinafanyika nyumbani kwa dada yake Yombo Relini (Kwa Ali Mbowa).

Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi, Amen.

Ghonche Materego
KATIBU MTENDAJI
BASATA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kwanza kabisa Mungu amuweke mahala pema peponi marehemu. pili napenda kumkosoa huyo mleta habari hii kwako ankal Michu. ukitazama alieandika habari hii ni katibu mtendaji wa Basata. ni baraza linalohusika na sanaa ,lugha na utamaduni, wakati katibu mzima wa baraza anashindwa kuandika Muajiriwa anaandika mwajiliwa mmhhh ankal kweli tutafika na miaka hamsini hii?.

    ReplyDelete
  2. kwani ulidhani katibu ni MALAIKA? wacha utoto hakuna asiekosea hata baba yako anakosea

    ReplyDelete
  3. Inawezekana uandikaji muajiliwa badala ya muajiriwa ikwa makosa ya uchapaji, si unajua tena haraka haraka za majukumu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...